Kwanini Waafrika Tunahitaji Misaada tuko nje ya Bara letu?

Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.
Ukiona siku tukianza kuvumbua na kugundua vitu vyetu wenyewe, kuacha unafiki, tamaa, ubadhirifu, ubinafsi, ukabila, visasa na udini hapo ndo tutaacha kutegemea misaada toka nje. Tunasumbuliwa na mambo mengi mno waafrika.
 
Tatizo huwa tunajua rangi ngeni ikiingia tu Tanzania hiyo ni pesa ndio maana maskini ya mungu wazungu wawatu wengine hali zao kama yangu tu ila akienda tu dukani ajiandae kuuziwa bidhaa bei ghari zaidi ya gharama yake
We Hujawahi Kusikia Msemo "Mzungu Akija Afrika, Mtalii Lakini Mwafrika Akienda Ulaya, Mkimbizi/Mhamiaji Haramu"
 
Kwasababu tumeshindwa kutumia rasilimali zetu.Mungu katupa kila kitu,kasoro dhamira ya kutumia kilicho chetu
 
Ukiona siku tukianza kuvumbua na kugundua vitu vyetu wenyewe, kuacha unafiki, tamaa, ubadhirifu, ubinafsi, ukabila, visasa na udini hapo ndo tutaacha kutegemea misaada toka nje. Tunasumbuliwa na mambo mengi mno waafrika.
Umeainisha matatizo. Je nani ayatatue?
 
Kwasababu tumeshindwa kutumia rasilimali zetu.Mungu katupa kila kitu,kasoro dhamira ya kutumia kilicho chetu
Kama tumeshindwa kuwa binadamu kamili wanaotumia akili zao kutatua matatizo yao na kutumia rasilimali zao kujiletea Maendeleo basi sioni hata kama tunastahili kupewa misaada.
 
Asante kwa kunielewa nadhani haya ni mambo tunahitaji wanafunzi wa kiafrika wafundishwe. Wakue wakifahamu kila tatizo ndani ya bara la Afrika lipo ndani ya uwezo wao kulisuluhisha. Viongozi wa Kiafrika waogope wananchi kuliko nchi za nje ya bara letu. Hebu fikiria kama pato la ndani lingekuwa linachangia asimilia 100 ya bajeti yetu? Unadhani serikali ingekuwa inajaribu kumfurahisha mzungu au wananchi?
Je wajua bara la afrika ndio bara tajiri duniani na pia ndio bara masikini kabisa duniani,hii vitu kaa cobalt ambayo inatumiwa na computer, smartphone, gari za umeme 90% yake inatoka dr congo,na acha hili tz tuna rotuba poa, bahari, kila kitu, kwanini tusilime na ukulima wa kisasa, tuprocess kahawa yetu, machai chai, samaki zetu, mboga na matunda, nyama za ngombe na mbuzi, tuuze taifa za nje, na utaona vile utajiri utamiminika tz, lakini kufanya hio inahitaji akili, elimu, na viongozi weye maarifa kabisa, swali ni tunnao viongozi kaa hawa?ona kazi yetu kununua wapizani, je hio ndio itaweka chakula mezani kwetu
 
Kama tumeshindwa kuwa binadamu kamili wanaotumia akili zao kutatua matatizo yao na kutumia rasilimali zao kujiletea Maendeleo basi sioni hata kama tunastahili kupewa misaada.
Misaada tunapewa ili tusiamke.....wanataka tuendelee kuamini sisi ni MASKINI huku wao wakiendelea kutukamua
 
Mi napenda kukujibu hivi Tanzania hatuna dira..hatuna muongozo wa kuufuata kila raisi ajaye ambapo kupitia huo muongozo ndio mafanikio..

Mbaya zaidi kila raisi anakuja nae sera zake atakama aliyetoka hakumaliza sera zake basi zitatupiwa kwenye dastbin..

Mfano sera ya kilimo ilikua nzuri sanaa.. baada mbaya kaondoka nayoe kikwete alivyokuja jpm kazika hii sera kaja na viwonder...

Viwonder vinahitaji raw material.. je tuta import toka nje... Ama tumalize hili swala la kilimo kwanza ndio tuje vi-wonder..

Kwa mantiki hiyo tz itabakia kua omba omba miakae yote kama tutaendelea kuishie bila dira...

Itengenezwe katiba ambayo tunaishi kupitia hiyo... Kila kitu raisi anacho fanya afuate katiba yenye dira.. kama ni kilimo basi kila raisi afuate kilimo tukishashamiri tunaweka vi-wonder sasa...

BILA DIRA NI NDOTO SA MCHANA KUACHA KUTEMBELEA BAKURI
 
Je wajua bara la afrika ndio bara tajiri duniani na pia ndio bara masikini kabisa duniani,hii vitu kaa cobalt ambayo inatumiwa na computer, smartphone, gari za umeme 90% yake inatoka dr congo,na acha hili tz tuna rotuba poa, bahari, kila kitu, kwanini tusilime na ukulima wa kisasa, tuprocess kahawa yetu, machai chai, samaki zetu, mboga na matunda, nyama za ngombe na mbuzi, tuuze taifa za nje, na utaona vile utajiri utamiminika tz, lakini kufanya hio inahitaji akili, elimu, na viongozi weye maarifa kabisa, swali ni tunnao viongozi kaa hawa?ona kazi yetu kununua wapizani, je hio ndio itaweka chakula mezani kwetu
Marekani kwasasa haina kiongozi mzuri lakini mbona jamii ya Marekani ina uwezo kumlazimisha afuate katiba japo yeye ana jeshi na polisi. Kwanini Jamii za kiafrika zinashindwa kusimamia viongozi wao? Haya maswali lazima ujiulize kabla hujalaumu viongozi kwasababu jamii ina jukumu lake la kuwasimamia viongozi kwa ajili ya manufaa ya nchi na bara la Afrika lakini hatufanyi hivyo.
 
Mi napenda kukujibu hivi Tanzania hatuna dira..hatuna muongozo wa kuufuata kila raisi ajaye ambapo kupitia huo muongozo ndio mafanikio..

Mbaya zaidi kila raisi anakuja nae sera zake atakama aliyetoka hakumaliza sera zake basi zitatupiwa kwenye dastbin..

Mfano sera ya kilimo ilikua nzuri sanaa.. baada mbaya kaondoka nayoe kikwete alivyokuja jpm kazika hii sera kaja na viwonder...

Viwonder vinahitaji raw material.. je tuta import toka nje... Ama tumalize hili swala la kilimo kwanza ndio tuje vi-wonder..

Kwa mantiki hiyo tz itabakia kua omba omba miakae yote kama tutaendelea kuishie bila dira...

Itengenezwe katiba ambayo tunaishi kupitia hiyo... Kila kitu raisi anacho fanya afuate katiba yenye dira.. kama ni kilimo basi kila raisi afuate kilimo tukishashamiri tunaweka vi-wonder sasa...

BILA DIRA NI NDOTO SA MCHANA KUACHA KUTEMBELEA BAKURI
Hata katiba ya sasa haifatwi na sisi wananchi tunaangalia Unadhani dira na katiba mpya zitafuatwa kama wananchi wenyewe hawajali? Tutalaumu viongozi lakini sisi tunamchango mkubwa sana kwenye kulea haya matatizo. Jamii haiwezi kuachia ustawi wake wote kwa viongozi. Wananchi wanajukumu la kuendeleza nchi na kuwasisimia viongozi wanapokosea na siyo kutegemea viongozi na mataifa ya nje kutusimamia na kutuletea maendeleo . Tuone nchi kama mali yetu tumewakodisha viongozi pale tunapoona wanaharibu mali tunakuwa wakali siyo kwasababu tunawachukia au kuleta siasa bali ustawi na uhuru wetu wa kujitegema ni muhimu kuliko jambo lolote.
 
Tatizo kubwa la Afrika ni uongozi.

Waliokosa upeo, ubunifu na uwezo, katika mataifa mengi ya Afrika, ndio wanaoongoza/kutawala huku wakiamini kuwa wana ufahamu na uzalendo kuliko wananchi wote wanaowaongoza.

Nchi za mabara mengine, kiongozi mkuu huwashirikisha kikamilifu wananchi waje katika kulioongoza Taifa lakini Afrika, kiongozi hulioongoza Taifa yeye pekee yake. Kwa hiyo ile faida ya kuwa watu wengi, vipawa mbalimbali, ujuzi na uwezo tofauti kutoka kwa watu tofauti, haipo. Nchi nzima mnabakia kutumia mawazo na matakwa ya mtu mmoja. Aghalabu huyu mtu mmoja, kamwe hawezi kuwa sahihi wakati wote.
Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.
 
Tunahitaji mafuta na gesi kujenga uchumi wetu mafuta na gesi yanauzwa kwa dola ...dola zinachapishwa Us....kuzipata inabidi kuuza bidhaa kwao kwa bei walopanga wao...usipokubali ushoga hawanunui....
 
Nyie ni Wajinga, Nyie Mna wivu wa kijinga, Nyie ni Wezi, Nyie Ni wabinafsi sana, Nyie siyo waaminifu. Kwa Hali hiyo hamtoweza chochote mtabaki kulaumiana mpaka mwisho.
Mkiingia madarakani mnatunga sheria ngumu ili tushindwe kuzimudu, hapo mnajiona wajanjaaa, Mmetukomoa. Hamjawahi kufanya biashara lakini mnajiona mnajua/fahamu sanaa, mnatutoza kodi kubwa, na tozo nyiingi ili tushindwe kufanya biashara , kisha mnajiona wajanjaaa, mmetukomoa. Tukifanya ugunduzi wetu wa kiasili mnaukataa manatuletea Sijui TFDA, mara Mkemia Mkuu, na Vibali ili tushindwe ,kisha mnajiona wajanjaa na mmetukomoa. Mnapoingia madarakani huwa masikini, mnaanza kuiba na kujilimbikizia mali za Umma kama zenu vile, Nyumba za Umma mnajiuzia kwa bei rahisi na manunuzi mnajitanguliza Nyie na Ndugu zenu, kasha sisi mnatuona mafala ,wajingaaa na mnaona mmetukomoa. Mkiingia madarakani mankuwa juu ya sheria,mnawateua ndugu zenu, mnaendeleza kwenu na kusahau misingi ya umoja wa kitaifa, mnasahau vipaumbele vya nchi mnatufanya wajiinga hatuelewi bali nyie ndio mnaakili peke yenu, kisha mnajenga uadui nasisi, nakutuwekea visasi, Na wanaofuata wanafanya kama nyinyi, ubinafsi, wizi, kulewa madaraka, nakutokufuata sheria, na wanofuata vile vile, kwa misingi hiyo mnadhani AFRIKA itaendelea kwa muujiza upi?!
Tuache Ujinga,Wizi, Elevi wa madaraka, tueshimu sheria, tuache ubinafsi, na tuwe waaminifu tukitumikia nafasi zetu kwa uadilifu. Mtaona Afrika inaendelea.
 
Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.

Kwasababu tumefungiwa kwenye box la chuma. Na kufuri zake zilishayeyushwa kwenye moto. Hilo ndilo jibu kwa kifupi na kwa ufasaha
 
Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.

Ww hapo ulipo umefanya nini mpaka sasa ambacho kimesaidia watu? Sana sana umepata elimu yako ya vyeti na kushia kuajiriwa. Huna chochote cha maana unachozalisha. Cha maana ni kufurahia ubazazi wa viongozi na kusujudu mawazo ya kisadikika. Katoe ajira hata 1,000 kwa wazo lako, kisha uje na verified id kwamba tusitegemee misaada kwani ww umeweza jambo fulani.
 
Ahsante lakini mada yangu inalenga Waafrika kama jamii na siyo viongozi tu. Nimegundua ni rahisi kuwanyooshea vidole viongozi lakini tumekuwa tunaacha kugusia vitu viwili. Kwanza, Viongozi wetu wote wanatoka kwenye jamii zetu na mara nyingi wanawakilisha aina ya watu waliopo kwenye jamii zao. Pili, hamna kiongozi anaweza kuongoza jamii yoyote bila kuwa na wafuasi wanaoshabikia uongozi wake.Kwahiyo bado nashauku kubwa sana kuelewa kwanini jamii zetu zilizopo ndani ya afrika bado tunapenda kuwa tegemezi.

Tunanyoosha vidole kwa viongozi kwanza, wengi wa viongozi wa kiafrika hupatikana kwa mifumi mibovu mfano halisi ni hapa kwetu. Nusu ya viongozi wetu wa kuchaguliwa hupatikani kwa dhuluma na wakishatangazwa washindi huhakikisha wanalinda mazingira yote ya dhuluma ili waendelee kukaa madarakani. Mfano hapa nchini utasikia kiongozi anasema katiba sio muhimu bali wananchi wanataka maji, afya nk. Anaipinga katiba ili atawale kwa mitazamo yake bila kushirikisha wengine, matokeo yake viongozi wazuri wa kuweza kuliongoza taifa hawapatikani kwani viongozi halisi hawawezi kutumia dhuluma kupata uongozi.
 
Tatizo ni wakoloni weusi, Africa bado haijapata mfumo sahihi wa uongozi, huu uitwao Uraisi ndo kuongoza wengi tutegemee umasikini zaidi.Ni hadi tubadili mfumo nchi zisiongozwe na MTU mmoja Bali kundi la watu.Mwafrica hana uwezo wa kumuongoza mwafrica mwenzake ataishia kumletea umasikini mwafrica mwenzake, atamfilisi,atamuuwa,atamteka,na madhila ya kila hali
 
Tatizo kubwa la Afrika ni uongozi.

Waliokosa upeo, ubunifu na uwezo, katika mataifa mengi ya Afrika, ndio wanaoongoza/kutawala huku wakiamini kuwa wana ufahamu na uzalendo kuliko wananchi wote wanaowaongoza.

Nchi za mabara mengine, kiongozi mkuu huwashirikisha kikamilifu wananchi waje katika kulioongoza Taifa lakini Afrika, kiongozi hulioongoza Taifa yeye pekee yake. Kwa hiyo ile faida ya kuwa watu wengi, vipawa mbalimbali, ujuzi na uwezo tofauti kutoka kwa watu tofauti, haipo. Nchi nzima mnabakia kutumia mawazo na matakwa ya mtu mmoja. Aghalabu huyu mtu mmoja, kamwe hawezi kuwa sahihi wakati wote.
Kwanini jamii zilizopo ndani ya nchi za Afrika zinakubali kuwa na viongozi wa aina hiyo. Je wananchi wenyewe wanakosaje kulaumiwa kwa kuvumilia kuendeshwa kama kuku wa bandani?
 
Yes ni madhara ya mfumo uuitwao uraisi, bila kuubadili mfumo huu tutakuwaomba omba na masikini milele,mfumo wa uraisi unafaa ulaya na marekani na sio Africa.

Back
Top Bottom