Kwanini Waafrika Tunahitaji Misaada tuko nje ya Bara letu?

Kwanini Waafrika Tunahitaji Misaada tuko nje ya Bara letu?

Hili suala ukiliangalia kwa mtazamo wa siasa za Nchini tu utapata shida kulichambua kuna msg yapo juu nimeshajibu kwamba kuna Nchi zaidi ya tano Afrika zimebadilisha vyama vilivyokuwa vinatawala lakini hadi leo hizo Nchi zinategemea misaada toka nchi za mabara mengine.

Hao walioingia madarakani walitaka kuwakwamua wananchi wao au walitaka tu madaraka?
 
Mkuu

Ni kwamba kila kitu kina maandalizi. maandalizi ya akili nayo pia huhitajika ili ujikomboe kama mtu mmoja au kikundi na hatimaye taifa kwa ujumla wake.
Sisi kwa ujumla hatukuandaliwa, au niseme tumeandaliwa kushindwa.
Kwanza ni vitu tunavyojifunza shuleni vinatuandaa kuwa wanyonge mbele ya wengine, namaanisha hii historia. Inatufunza kuona kuwa kuna watu wanatuzidi kwa kila kitu hivyo mpaka maamuzi juu yetu.
Mfano mzuri wa hilo ni hata viongozi mbadala wa waliopo, utaona ukikwaruzana na watoa misaada, wao ndo wa kwanza kusema tutanyimwa misaada na taifa litaangamia. Sijawahi kuona kiongozi asiyesifia misaada na hili limeenda mbele zadi kwamba lazima uwe na chama rafiki huko ili kikusaidie kupata madaraka.
Pili ni tamaa ya viongozi wenyewe, namaanisha kuwa siasa ni kama ajira sawa na ajira nyingine. Mbaya mwanasiasa anataka awe na nguvu kuliko wale waliomuweka madarakani. Kuwa na nguvu lazima uwanyanyase na kuwatisha walio wanyonge ili wakusujudia, hapa huhitaji kwenda GYM, lazima uwe na peas kuwazidi, tena kwa mbali. Hapa ndo mwanasiasa anapotafuta pesa kwa njia yoyote ile ili awe SUPERIOR kuliko wengine. Wale ambao ataona kuwazidi kifedha hataweza, anaungana nao kuwanyayasa walio wanyonge,NDO MISAADA inapoanzia.
Kwa ujumla mwanasiasa hatashughulika na matatizo ya wananchi mpaka atosheke yeye, na nakuhakikishia hatatosheka mpaka na hivyo ataenda mbali zadi kuhakikisha anajenga urafiki nje ya mipaka kwa kutumia rasilimali za nchi kujiimarisha, huu ni MWANZO WA MISAADAya kimataifa.
Tatu ni mataifa yatoayo misaada kunufaika kwa mgongo wa nyuma, waweza kudhani ni wema sana, la hasha, bali nyuma ya pazia akitoa moja moja anapata mbili. Naye kwa upande wa pili atajitahidi kwa hali na mali kukuaminisha kuwa wewe huwezi bila yeye na yupo tayari kukusaidia ili wewe usiishughulishe akili.
Namalizia kwa kukili kuwa kuna mikataba inayoyalazimisha mataifa yale yatusaidie, na ndo hiyo hiyo inawapa fursa ya kuchukua mali gafi kwa bei poa na kutuuzia kwa ghali baada ya kuboresha.
Ukweli mtupu tutatokaje kwenye hii minyonyoro kwasababu nimegundua hata wasomi wanaamini bila Nchi za Ulaya na Asia hatuwezi hadi kuna muda unaanza kujiona inferior kama Mwaafrika
 
Kuna jamaa yangu aliwahi kusema Africa inabidi tunyimwe misaada na mikopo yote, Nadhani tunaweza kupiga hatua mbele zaiidi.
 
Mkuu majibu ya maswali yako yote yanapatikana katika historia ya dunia na matukio yote makuu yaliyoikumba dunia aidha kuchagizwa na viongozi wa zamani au hata wa sasa, ambao walikubali kushirikiana na mabeberu katika kutekeleza azma ovu ya kulinyonya bara Afrika kwa kutumia nchi tajiri au taasisi kubwa za kitaifa na kimataifa zinazofahamika kwa sheria walizozitunga wao.

Ili uweze kuelewa madhara yaliyotukuta nakushauri kwa wakati wako, utenge muda wako ukisome kwa makini kitabu cha historia cha mwandishi Gervas M. Zombe kilichosheheni nukuu za kihistoria kwa maelezo ya hatua kwa hatua. Ukiisha kisoma chote, nina hakika utaelewa kanuni zilizotumika kudumaza fikra za waafrika. Yanoendelea katika zama hizi ni muendelezo tu wa ubeberu.

Soma kitabu hiki:.. Major events in the world history
History paper 2 notes
Advanced Level Form 5&6
sawa ni swala la kihistoria, hilo hatukatai. je hatuwezi tukaipindua-pindua historia hii na kuanza upya?.

nadhani tukiamua tunaweza labda tukose dhamira ya dhati ya kujitoa katika minyororo hii ya kupenda kupewa misaada na wazungu.
 
Hao walioingia madarakani walitaka kuwakwamua wananchi wao au walitaka tu madaraka?
Kwenye demokrasia siyo kazi ya serikali kukwamua mwananchi bali kumwekea mazingira mazuri ili mwananchi aweze kujikwamua. Pia ni kazi ya wananchi kuisimamia siyo lazima wapinzani wafanye kila kitu hata wananchi bila kujali vyama vyao wanauwezo kuandamana kudai haki zao au jambo fulani kwa ustawi wa Nchi yao.
 
Kuna jamaa yangu aliwahi kusema Africa inabidi tunyimwe misaada na mikopo yote, Nadhani tunaweza kupiga hatua mbele zaiidi.
Huu ni ukweli. Misaada inatupofusha kuona umuhimu wa kujitegemea.
 
Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.

hakuna nchi yoyote duniani ambayo inajitosheleza kwa kila kitu.Na siyo afrika tu ndo inayohitaji misaada pekee bali ni nchi zote zinahitaji misaada. Jua kwamba always resources are so scarce so such a scarcity needs someone to fill it.unahitaji kujenga barabara lkn fedha hakuna au haitoshi unahitaji kukopa au kuomba msaada kwa mwingine.hata nyumbani kwako leo huna chunvi,sukari nk unaenda kwa jirani ili akusaidie.ukisoma nadharia za uchumi utajua kwa nchi huwa zinakopa.
 
Kwenye demokrasia siyo kazi ya serikali kukwamua mwananchi bali kumwekea mazingira mazuri ili mwananchi aweze kujikwamua. Pia ni kazi ya wananchi kuisimamia siyo lazima wapinzani wafanye kila kitu hata wananchi bila kujali vyama vyao wanauwezo kuandamana kudai haki zao au jambo fulani kwa ustawi wa Nchi yao.

Wananchi kuandamana!? Kwa post hii nimejua unaongea nadharia tu huna lolote ujualo. Unafahamu maandamano yanachukuliwaje nchi hii? Uliona vyombo vya dola vilikuwa vinafanyaje maandamano yalipotangazwa? Baki na elimu yako ya makaratasi huna jipya unaloweza kuleta nchi hii zaidi ya kuabudu ajira. Endelea kushangaa sisi kutegemea misaada wakati hata kuelewa uhalisia wa mazingira yanayokuzunguka umeshindwa.
 
Waafrika tumepungukiwa vitu flank kutokana na kuzaliwa alafu mazingira yakaongezea. Tunauvivu wa kufikiri,roho ya kutaka mwenzio kushindwa,akili za kuelewa polepole na kutojali...itachukua miaka mingi kushinda haya matatizo
Jibu limeshapatikana. Asante sana.
 
Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.

fikiri mara mbili
sio wazo baya lakini jiulize leo hii

hii mada usingeleta hapa kutushawishi wana jf bila ya hao wenzetu

au nakosea MODS
 
Ikiwa unafahamu kuwa tunategemeana, iweje usione umuhimu wa taifa moja kwa lingine?
Taifa lipotegemea kupewa zaidi ya asimilia 40 ya bajeti yake huwezi kusema inategemeana na mataifa mengine utacheza na lugha lakini huo ndiyo ukweli wenyewe.
 
Wananchi kuandamana!? Kwa post hii nimejua unaongea nadharia tu huna lolote ujualo. Unafahamu maandamano yanachukuliwaje nchi hii? Uliona vyombo vya dola vilikuwa vinafanyaje maandamano yalipotangazwa? Baki na elimu yako ya makaratasi huna jipya unaloweza kuleta nchi hii zaidi ya kuabudu ajira. Endelea kushangaa sisi kutegemea misaada wakati hata kuelewa uhalisia wa mazingira yanayokuzunguka umeshindwa.
Hivi uliona Mubarak vifaa alivyotoa watu walipoanza kuandamana unaweza kufananisha na hivi vya hapa? Mbona watu waliendelea kuandamana. Watanzania hawakuandamana kwasababu hawaku shawishika kuandamana wangekuwa wameshawishika hata vile vifaa wasingeviogopa na hiyo siyo nadharia.
 
Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.
Swami juu ya swali, hayo maisha tuliyoyaishi yalikuwaje? Tulikuwa wengi hivi? Changamoto za leo zilikuwepo?
Ukipata jibu tuliruhusuje kutawaliwa na hao waarabu na wazungu utakuwa umepata mwanga wa wapi pa kuanzia
 
Hivi uliona Mubarak vifaa alivyotoa watu walipoanza kuandamana unaweza kufananisha na hivi vya hapa? Mbona watu waliendelea kuandamana. Watanzania hawakuandamana kwasababu hawaku shawishika kuandamana wangekuwa wameshawishika hata vile vifaa wasingeviogopa na hiyo siyo nadharia.


Mkuu hebu acha utani basi. Unafananisha uelewa wa Wamisri na Watz?
 
Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.
Mkuu umeuliza swali la msingi kabisa hapa,ingawa kama ilivyo kawaida yetu maada kama hizi huwa na wachangiaji wachache.
Kikubwa ninachoweza kusema ni kuwa kushindwa kwetu kujiendesha bila misaada ni moja ya mitego mikubwa iliyowekwa na hao hao watoa misaada.
Africa kama bara limeshikwa kiakili sana na hawa tunawaita "wadau wa maendeleo/wahisani"kupitia mashirika yao makubwa na aina ya sera wanazotulazimisha kuzifuata hata kama hatuzitaki,ndio maana ukiangalia kwa undani zaidi,utagundua vitu kama IMF,World bank,sijui sera za utandawazi,UN nk vimeundwa kwa ajili ya wao kuitawala zaidi dunia (Africa ikiwemo) kiliko kusaidia.
sio rahisi kwatu kujinasua kutoka kwenye makucha yao,lakini si kusema haiwezekani kama tukiamua kwa pamoja.leo hii Tanzani kama Tanzania ikiamua kupambana na mabepari peke yake katu haitakuja kufanikiwa,ila Africa kama Africa ikiamua kwa dhati kabisa kujitoa katika makucha ya hawa watoa misaada,tutafanikiwa.
Tunapaswa kukata mahusiano na hawa watu kwa asilimia kubwa tu,halafu tushirikiane sisi kama sisi kwa ukaribu sana.kwa sababu mpaka dakika hii sisi tunaishi uongo,hatuna cha maana tunachozalisha lakini tuna kila aina ya bidhaa zinayozalishiwa viwandani kwenye masoko yetu,hatuna cha maana tulichogundua lakini tunao uwezo wa kupata vyote vilivyogunduliwa kwenye nchi zetu,sasa kwa msingi huo tutaweza vp kuzalisha au kugundua ikiwa kila kitu tunapata?....
Kwa mfano;kabla ya kupika unahitaji kuwasha moto,lakini moto huo utauwashaje?ndipo hapo utakapoumiza kichwa ili ugundue kiberiti,sasa ikiwa viberiti vimetapakaa kibao kwenye nyumba yako,ingawaje haujui vinatengenezwa vp,je utakuwa na wasaa wa kuumiza kichwa iil ujue viberiti vinatengenezwa vp?haiwezekani hata kidogo,tunalemazwa akili tunafanywa kuwa tegemezi kwa kila kitu kutoka kwao ili waendelee kutuongoza mpaka milele,bila sisi kuwa na viwanda vyetu,bila sisi kuwa na ugunduzi wetu,bila ya sisi kuwa na sera zetu bila ya sisi kuwa aina ya elimu yetu ambayo kwanza itasadifu mazingira yetu,hatutaweza kujikomboa bali tutabaki kulaumiana na kupigana wenyewe kwa wenyewe mpaka mwisho.
Mtoto anaanzaje kukimbia kabla hata ya kuanza kukaa mwenyewe? Ndio aina ya maisha tunayoishi waafrica hii leo,tunataka kuishi kama wao,bila kuangalia wapi tulipo,(chanzo cha ufisadi) tunataka kumiliki kila kitu cha wanachomiliki wao bila hata kuzalisha chochote (chanzo cha kuwa wapumbavu),tunakubali kuwa na soko la pamoja kati ya bidhaa zao na zetu (chanzo cha viwanda vyetu kufa).
Ili tupate maendeleo ya kweli lazima tukubali kurudi nyuma,tutake tusitake,lazima tukubali kuumia sisi kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Lakini sisi kama jamii tuna matatizo makubwa kama ambavyo umekuwa ukisisitiza,tunayataka mabadiliko kwa maneno lakini tunayaogopa kwa matendo,unakumbuka ilisemwa mitumba itapigwa chini baada ya muda fulani,sasa uliona hizo kelele zilizopigwa humu?ndio jamii yetu hiyo ilivyo,ubinafsi mwingi,maneno mengi,ujuaji mwingi.leo hii itangazwe kuwa smart phone zote marufuku kwa kila mtanzania kwa sababu kuna kampuni ya watanzania imeanza kutengeneza simu,kama yale manokia au Siemens za mwanzo kabisa (mche wa sabuni), wangapi humu watakubaliana na jambo hilo?kwamba tuanze tena kutumia miche ya sabuni? Pasi kutaka hata kujua hatua hiyo imelenga nini,Aiseeh utaiona kazi!!!!!
Bila kufunga masoko hatutaweza kushindana nao kwa bidhaa zenye ubora,bila kukataa sera zao(ambazo zipo kwa manufaa yao),hatutaweza kutunga zetu kwa manufaa yetu,bila kuwa na changamoto zinazotusumbua,hatuweza kutafuta ufumbuzi (kuendelea kuwa wapumbavu),kwa maana si tunaletewa kila kitu na misaada juu tunapewa.
Hebu niambie tangu niambie tangu tumeanza kuwapigia magoti hao wawekezaji wa kigeni,ni uwekezaji gani mkubwa waliyoufanya ktk bara hili?madini?gesi?mafuta?aiseeh kweli wajinga ndio waliwao!!!! Acha tu niishie hapa,maana na nitaandika mpaka kesho kutwa hapa.ila tu ili tusiwe tegemezi,lazima tubadilike,na kwenye safari hiyo ya mabadiliko lazima tutubu,je tupo tayari kutubu sisi kama waafrica kuanzia watawala mpaka watawaliwa?tutakubali kuacha haya mambo mazuri mazuri kutoka kwa ndugu zetu wanaotupenda na kututhamini sana kwa misaada ya kifedha na kisera mengineyo?
 
Upo sawa lakini nachojaribu kuelewa kama Waafrika tunafahamu tuna viongozi wabaya lakini tunakaa chini tunasubiri "utegemezi" watu wengine "wazungu" waje watusaidie. Hiyo inatengeneza picha gani kuhusu sisi?
Waafrica tunafahamu fika kuwa tuna viongozi wabaya. Lakini hatua tunazochukua kwa njia ya sanduku la kura hazina maana kwa watawala. Mwenye kuamua nani awe kiongozi ni mwesabu na mtangaza matokeo ya kura na siyo mpiga kura.
 
Back
Top Bottom