Kwanini Waafrika Tunahitaji Misaada tuko nje ya Bara letu?

Walnut Creek

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,712
6,033
Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.
 
Hilo Nadhani Litakuwa Ni Swali Lenye Jibu Gumu! Yaani Hata Hilo Jibu Utakalopewa Kulielewa Ni Shida!
 
Waafrika tumepungukiwa vitu flank kutokana na kuzaliwa alafu mazingira yakaongezea. Tunauvivu wa kufikiri,roho ya kutaka mwenzio kushindwa,akili za kuelewa polepole na kutojali...itachukua miaka mingi kushinda haya matatizo
 
Mkuu majibu ya maswali yako yote yanapatikana katika historia ya dunia na matukio yote makuu yaliyoikumba dunia aidha kuchagizwa na viongozi wa zamani au hata wa sasa, ambao walikubali kushirikiana na mabeberu katika kutekeleza azma ovu ya kulinyonya bara Afrika kwa kutumia nchi tajiri au taasisi kubwa za kitaifa na kimataifa zinazofahamika kwa sheria walizozitunga wao.

Ili uweze kuelewa madhara yaliyotukuta nakushauri kwa wakati wako, utenge muda wako ukisome kwa makini kitabu cha historia cha mwandishi Gervas M. Zombe kilichosheheni nukuu za kihistoria kwa maelezo ya hatua kwa hatua. Ukiisha kisoma chote, nina hakika utaelewa kanuni zilizotumika kudumaza fikra za waafrika. Yanoendelea katika zama hizi ni muendelezo tu wa ubeberu.

Soma kitabu hiki:.. Major events in the world history
History paper 2 notes
Advanced Level Form 5&6
 
Blaablaa na kutokuwa na viongozi wazalendo . Kupiga dili ni kazi yetu na tumebobea kwa hilo . Mf. Mtu una shida ya maji ila water table ipo karibu ni kiasi tu cha uongozi thabiti ili kutoboa maji . Pesa ikipatikana anaitumia kiongozi kwa mambo yake . Kwa kifupi " chukua chako mapema "
 
Kwa maneno mengine sisi Waafrika hatupo sawa na binadamu wenzetu toka mabara mengine. kwahiyo ni sawa wakituona tupo chini yao. Unaamini hivyo?
 
Ahsante lakini mada yangu inalenga Waafrika kama jamii na siyo viongozi tu. Nimegundua ni rahisi kuwanyooshea vidole viongozi lakini tumekuwa tunaacha kugusia vitu viwili. Kwanza, Viongozi wetu wote wanatoka kwenye jamii zetu na mara nyingi wanawakilisha aina ya watu waliopo kwenye jamii zao. Pili, hamna kiongozi anaweza kuongoza jamii yoyote bila kuwa na wafuasi wanaoshabikia uongozi wake.Kwahiyo bado nashauku kubwa sana kuelewa kwanini jamii zetu zilizopo ndani ya afrika bado tunapenda kuwa tegemezi.
 
Ninarudi pale pale kwenye suala la kuwa tegemezi ,kwanini kijiji cha watu mia 500 au 600 kinasubiri kiongozi mmoja aje awachimbie kisima wakati wao wanapata taabu ?
 
Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.
Shinda ni hii mkuu HATUNA VIONGOZI WENYE AKILI TIMAMU,angalia swali la korosho, kiongozi gani mweye akili timamu anaweza fanya vile huyu kiongozi wetu amefanya?badala la kutatua tatizo kwa kutumia akili, tunatatua tatizo kupitia mabavu na vicha tupu,hio ndio shinda mkuu
 
Kwa maneno mengine sisi Waafrika hatupo sawa na binadamu wenzetu toka mabara mengine. kwahiyo ni sawa wakituona tupo chini yao. Unaamini hivyo?
Tupo chini yao _ yes,hatupo sawa na wenzetu _ true,nisawa wakituona tukochini yao _ correct!! Hawatakiwi kutudharau na kutuibia wakati sisi tunatakiwa kujiendeleza kwa bidii. Vitabu pia vinaeleza hivyo. Labda utueleze we unadhani shida ninini? Hakuna nchi ya afrika iliyoweza kutoboa ninishida?mfano unakuta mmasai anang'ombe miatano lakini hata haogi?
 
Shinda ni hii mkuu HATUNA VIONGOZI WENYE AKILI TIMAMU,angalia swali la korosho, kiongozi gani mweye akili timamu anaweza fanya vile huyu kiongozi wetu amefanya?badala la kutatua tatizo kwa kutumia akili, tunatatua tatizo kupitia mabavu na vicha tupu,hio ndio shinda mkuu
Upo sawa lakini nachojaribu kuelewa kama Waafrika tunafahamu tuna viongozi wabaya lakini tunakaa chini tunasubiri "utegemezi" watu wengine "wazungu" waje watusaidie. Hiyo inatengeneza picha gani kuhusu sisi?
 
Nimekuelewa sasa, yaani pia sisi waafrika ni wakulaumiwa kabisa, badala ya tutatue matatizo yetu tunangoja mzungu saidia, eu wewe fikiria hii karne ya21 century bado taifa letu linaomba hata misaada ya condoms na net, ajabu hio, nafikiri uelewa wetu ni mdogo na ndio tunashangilia na kuchagua viongozi ambao hamna akili kabisa
 
Tupo chini yao _ yes,hatupo sawa na wenzetu _ true,nisawa wakituona tukochini yao _ correct!! Hawatakiwi kutudharau na kutuibia wakati sisi tunatakiwa kujiendeleza kwa bidii. Vitabu pia vinaeleza hivyo. Labda utueleze we unadhani shida ninini? Hakuna nchi ya afrika iliyoweza kutoboa ninishida?mfano unakuta mmasai anang'ombe miatano lakini hata haogi?
Hadi naanzisha hii thread nimejiuliza haya maswali na nimekosa majibu. Nimegundua tumekuwa tukitafuta scapegoat kwenye kukabili matatizo yetu kuanzia kuwa na viongozi wabovu, kushindwa kujiletea maendeleo , kushindwa kupambana na watu mabara mengine kwenye Nyanja za uchumi na teknolojia na hata kushindwa kutetea utu wetu kama Waafrika.
 
Nimekuelewa sasa, yaani pia sisi waafrika ni wakulaumiwa kabisa, badala ya tutatue matatizo yetu tunangoja mzungu saidia, eu wewe fikiria hii karne ya21 century bado taifa letu linaomba hata misaada ya condoms na net, ajabu hio, nafikiri uelewa wetu ni mdogo na ndio tunashangilia na kuchagua viongozi ambao hamna akili kabisa
Asante kwa kunielewa nadhani haya ni mambo tunahitaji wanafunzi wa kiafrika wafundishwe. Wakue wakifahamu kila tatizo ndani ya bara la Afrika lipo ndani ya uwezo wao kulisuluhisha. Viongozi wa Kiafrika waogope wananchi kuliko nchi za nje ya bara letu. Hebu fikiria kama pato la ndani lingekuwa linachangia asimilia 100 ya bajeti yetu? Unadhani serikali ingekuwa inajaribu kumfurahisha mzungu au wananchi?
 
Ahsante lakini mada yangu inalenga Waafrika kama jamii na siyo viongozi tu. Nimegundua ni rahisi kuwanyooshea vidole viongozi lakini tumekuwa tunaacha kugusia vitu viwili. Kwanza, Viongozi wetu wote wanatoka kwenye jamii zetu na mara nyingi wanawakilisha aina ya watu waliopo kwenye jamii zao. Pili, hamna kiongozi anaweza kuongoza jamii yoyote bila kuwa na wafuasi wanaoshabikia uongozi wake.Kwahiyo bado nashauku kubwa sana kuelewa kwanini jamii zetu zilizopo ndani ya afrika bado tunapenda kuwa tegemezi.
Kuwa tegemezi kunaanzia kwenye familia na familia zote zina viongozi wanaofanya maamuzi iwe kwa ushawishi wao wenyewe ama kwa kulazimishwa. Viongozi wana mchango mkubwa katika ustawi wa jamii, na katika jamii yoyote sehemu kubwa ya maamuzi hufanya na viongozi, hakuna namna inayoweza kuwatenganisha viongozi na ustawi usioridhisha.
 
Viongozi wanatoka ndani ya jamii huwezi tofautisha jamii husika na viongozi.
Kama Kiongozi ni mbovu au anapenda kuwa tegemezi basi hata jamii yake ina tabia hizo hizo.
 
Mi nafikiri Ni njaa tu mkuu thus why tunapitisha bakuli
Tatizo huwa tunajua rangi ngeni ikiingia tu Tanzania hiyo ni pesa ndio maana maskini ya mungu wazungu wawatu wengine hali zao kama yangu tu ila akienda tu dukani ajiandae kuuziwa bidhaa bei ghari zaidi ya gharama yake
 
Back
Top Bottom