Kwanini Waafrika Tunahitaji Misaada tuko nje ya Bara letu?

Kwanini Waafrika Tunahitaji Misaada tuko nje ya Bara letu?

Kwenye demokrasia siyo kazi ya serikali kukwamua mwananchi bali kumwekea mazingira mazuri ili mwananchi aweze kujikwamua. Pia ni kazi ya wananchi kuisimamia siyo lazima wapinzani wafanye kila kitu hata wananchi bila kujali vyama vyao wanauwezo kuandamana kudai haki zao au jambo fulani kwa ustawi wa Nchi yao.
Tumeaminishwa kuwa serikali in a wajibu wa kila kitu juu ya Marsha ya mwanainchi. Tubadili fikra zetu tutasonga
 
sawa ni swala la kihistoria, hilo hatukatai. je hatuwezi tukaipindua-pindua historia hii na kuanza upya?.

nadhani tukiamua tunaweza labda tukose dhamira ya dhati ya kujitoa katika minyororo hii ya kupenda kupewa misaada na wazungu.
Mkuu tunaweza tena sana tu, tatizo letu ni kukosa utashi na kutojiamini. Historia ndio msingi wa makosa yetu, lakini pamoja na mawapungufu yetu yaliyotajwa na wadau humu, tukijirudi na kuunganisha nguvu zetu, inawezekana kabisa kupindua historia.
 
Ningependa na sisi tunaopokea misaada ya kimitegeo tuanze kujitadhimini lazima tutakuwa na shida kuanzia viongozi wetu hadi wenyewe la sivyo hali zetu hazitabadilika.
ukweli wanajua wao na Mungu, yani mie naisi vyama ni vyao na viongozi nawao yani vibaraka wao, sie tulio kua njee ya mfumo tuna uchungu na tuna marifaa mengi au tuna maono mazuri ila haya chukuliwi maanani ndo ujue ni watu wao.
 
Tatizo kubwa la Afrika ni SIASA na UZOEFU wa umaskini uliokithiri
Siasa
Viongozi wetu wa kisiasa ndio pekee wamepewa fursa ya kwenda popote duniani kuona na kujifunza wengine wanaishajie na waliwezaje. Wao wakienda wanakula posho tu, wakirudi wanawaangalia maskini na kuridhika nao
Uzoefu Katika Umaskini
Viongozi na wataalamu wa nchi hwakereki na umaskini kwani wameuzoea sana. Wanajiangalia wao ilhali wakiwaacha maskini wakiendelea kuteseka kwa kukosa ajira na kuishi maisha duni. Kila kiongozi na wataalamu wa nchi hii wana ndugu zao wanaoteseka na umaskini hawawajali sembuse watanzania wengine

Tunahitaji mapinduzi ya siasa na kifikra.
 
Muulize Hamu na baba yake.
Kuna mtu aliambiwa utakuwa mtumwa wa ndugu zako, kile kizazi kilichoambiwa kitakuwa kitumwa kwa wenzake ndo sisi Waafrika.
Mpaka dunia itakwisha Mwafrika atatumikishwa na Mwarabu, Mzungu na kila kizazi cha mataifa ya nje ya Afrika.
Leo hapa dar ukimwona mzungu anaokota makopo hata wewe mwandishi utasimama na kuanza kushangaa, why?
Kwasababu yeye ni mfalme wako.
 
Mungu alipoiumba hii dunia aliumba pia ile hali ya mmoja kumuhitaji mwingine. Hakuumba ile hali ya mimi nije kwako halafu kwangu usipoajue.

Mungu hakubaliani na kwa mfano kinachofanywa na Donald Trump kwa kuwaita wavamizi wale watu wa nchi za Amerika ya kusini, wanaokwenda Marekani kutafuta maisha bora.

Huwezi kukwepa kutegemea maarifa ya mwenzako. Ndio maana Marekani na mbwembwe zake zote imejaa wataalam wa hesabu na sayansi kutoka India.

Ulaya ina miezi michache ya jua kuonekana, kwa mzungu kujaa kuwatazama simba na pundamilia ni sisi kwenda Ulaya ni sehemu ya hali ya asili ambayo haikwepeki.
 
Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.
Hata wazungu wasingekuja bado tusingeendelea mpaka kuwa sawa na wazungu. Tungebakia na tamaduni zetu za jadi ambazo nazo mpaka kufikia sasa zisingeweza kutuletea maendeleo sawa na wazungu. Tena bila ya kuja wazungu kutawala tungekuwa nyuma sana kimaendeleo kuliko hivi. Ni angalau sasa tumeendelea kwa kiasi hiki ksbb wazungu walituletea elimu ndani ya elimu kunazaliwa ustaarabu. Sasa angalau huo ustaarabu umeleta kila mmoja kuheshimiwa,(japo kwa hali ile ile niliyozungumzia hapo kwamba tusingeendelea kabisa bila wazungu,-ona watawala wengi wa kiafrika mpaka sasa walivyo na dhuluma ya wazi kwa wananchi wanaowaongoza. Nikizungumzia dhuluma ina mapana yake sana. Kubwa kabisa kwa sasa Tunashindwa kuendelea ksbb ya Uongozi mbovu. Tunaendalea kuwategemea wao ksbb wametutangulia na wametengeneza mazingira kuwateka kututeka kifkra,tunaamini bila wao hatuwezi. Tumebweteka kabisa tunasubiri tecknorojia yote watuletee. Tu unatakiwa uongozi wa kama Mwalimu Nyerere,Kwame Nkuruma,n.k
 
Back
Top Bottom