Kwanini Vitu Vinadondoka? (Newton vs Einstein)

Kuchwizzy

JF-Expert Member
Oct 1, 2019
496
1,000
Kwanini vitu vinadondoka?

Hili swali kwa muda mrefu nilikua nalichukulia poa (take for granted) lakini sasa nakili kuwa ni moja kati ya maswali magumu zaidi kuwahi kuulizwa na binadamu.

Ukiacha Programming kitu kingine ninachokipenda ni Modern Physics, nasoma basics tu niweze kuelezea ulimwengu ninao interact nao kila siku baada ya Computer

So nilikua naamini kabisa kuwa naweza kuelezea kwanini vitu vinadondoka? Kwanini jiwe linarudi chini ukilirusha juu?
Kwanini apple linaanguka juu ya mti?

Isaac Newton alitupa Formula sahihi(kiasi) ila maelezo ya "uongo" kuhusu kwanini vitu vinadondoka

Kwa mujibu wa Sir Isaac Newton, jiwe linadondoka kwasababu kwasababu ya nguvu ya uvutano kati yake na Dunia. nguvu hii ya uvutano ndiyo inayofanya jiwe livutwe chini kwa kasi ya mita 9.8 kwa kila sekunde ya kila sekunde (acceleration due to gravity)

Na hayo maelezo ya uongo nimekua nikiyaamini mpaka hapo juzi nilipopata nafasi ya kujifunza General Relativity. Na nilichogundua ni kuwa, siwezi tena kuelezea kwa nini jiwe au kitu chochote kinadondoka

Naamini kuna watu smart humu waliosoma General Relativity au kuielewa, wanaweza kutuelezea kwanini vitu vinaanguka..

Kwanini Newton hakua sahihi?

Newton hakua sahihi kwa sababu hii

Imagine umeshika chupa iliyojaa maji (umeinyanyua)
ukiachia hii chupa, itandondoka chini sio?

Hapana, chupa haitondondokaChupa haitondoka kwasababu hakuna nguvu yoyote inayoivuta hio chupa. Ku prove hili, tutoboe matundu mawili katikati ya hio chupa
Kipindi tumeishikilia (maji yatamwagika chini kupitia yale matundu) ila tutakapo iachia maji hayatomwagika tena hata kama chupa ina matundu. so hakuna force yoyote inayovuta yale maji tena.

hqdefault.jpg

Kwa mjibu wa Newton first law of motion, hii chupa itaganda pale pale kwasabau kama F=ma , m=mass ya chupa ya maji , a= acceleration na F= 0 (kwasababu hakuna nguvu yoyote inayoivuta) basi a=0 (haitodondoka)
kumbuka m > 0 (chupa always ina mass)

Sasa swali linabaki kwanini hii chupa tunaiona ikishuka kutoka juu mpaka chini?
Au kwanini vitu vinaonekana kudondoka?

UPDATE:
Wazee naona kama baadhi hamjaelewa swali au lengo la huu uzi

Swali ni hili "Kwanini vitu vinadondoka?"

NOTE: usitumie classical mechanics kujibu hili swali thus why nimeanza kuonyesha hapo juu kwanini classical mechanics haiwezi kujibu swali hilo
 

Kuchwizzy

JF-Expert Member
Oct 1, 2019
496
1,000
It's due to gravitational force that attracts all objects towards the center of the earth.
Hii ni kwa mjibu wa Classical Mechanics ambayo ina depicts gravitation as "force"
ila in reality hakuna force yoyote inayo act kwa kitu kinachoonekana kudondoka

Thus why sikutaka ili jibu la Classical Mechanics kwa sababu halipo sahihi

Gravitation sio force

Swali bado , kwanini vitu vinaonekana kudondoka

Kwa yoyote aliyenielewa
 

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
16,829
2,000
Hii ni kwa mjibu wa Classical Mechanics ambayo ina depicts gravitation as "force"....
Unavyosema kihalisia hakuna nguvu inayosababisha kitu kishuke chini unamaanisha nini?

Kwamba ni juhudi pekee ya hicho kitu ndio kinasababisha kushuka?
 

Kuchwizzy

JF-Expert Member
Oct 1, 2019
496
1,000
Kwenye ishu ya maji Mimi hapo kwa mtazamo wangu naona kilichofanyika hapo ni mechanism ya "water pressure"

Niko hapa kujifunza
Nimetumia mfano wa chupa ya maji kwasababu ni experiment rahisi unayoweza kuifanya hata ukiwa nyumbani

The moment umeiachia chupa hakuna force yoyote inayo act pale hence net force iliyokua inavuta maji chini inakua zero

Kama mfano wa chupa umekuchanganya.....imagine mtu anaye anguka kwenye lift (Elevator)
Huyu mtu ata feel weightless sawa sawa kabisa na astronaut aliye kwenye Space
In both scenarios hakuna force yoyote inayo act kwao

So kulingana na Newton first law(f=ma), kama net force ni 0, basi hata acceleration ni 0 (cause mass haiwezi kuwa zero)

Baadhi ya watu hapa bado wanatumia Classical mechanics kujibu hili swali bila hata kusoma nilichoandika

Swali ni kama F=0 na a=0 kwanini chupa inaonekana kushuka chini?
Ili swali limejibiwa na General Relativity lakini maelezo yake ni very confusing thus why nipo hapa kupata mtu aliyeelewa


Jibu ni , "Things fall because their future belongs to the ground"
Hapa ndio sielewi, yaani in short mda ndio unaosababisha vitu kuanguka but sijui jinsi gani walivyofika kwenye hii conclusion

Bahati mbaya hapa najibiwa na watu ambao hawajawahi kusoma hata hio General Relativity
Kwa yoyote atakayenielewa much thanks
 

Teknologist

JF-Expert Member
Oct 20, 2018
750
1,000
I am Newtonian fan sababu nitaiishi maisha yangu yote down to earth na hiyo chupa in classical mechanics ukiiachia inaanguka
Usichanganye Newtonian Mechanics na General relativity

Newtonian mechanics is correct at its own merit and conditions thus Newton’s laws of motion explain gravity to particle level physics and are obeyed to a high precision for velocities much less than the velocity of light, it is useful in determine the gravitational force of things that are in velocity that is less than velocity of light like a falling apple.

While general relativity is sub atomic particle physics relates to speed of light and is the theory that formulates gravity in terms of the curvature of spacetime, Since light moves at the speed of light, it sees equal amounts of space and time curvature, so it bends twice as far as the Newtonian theory would predict, its only useful in things like determining the behaviour of the Black Hole, or the trajectory of the Mercury around the Sun which Newtonian mechanics failed to do so.
 

Mr Tyang

JF-Expert Member
Sep 30, 2018
1,275
2,000
Mleta mada naona Kama bado una akili kidogo Sana ya ku argue na laws zilizochakatwa na kupitishwa na jopo la nguri wa sayansi, kama hizo "Newton law of Motion".

Nakuomba uendelee kujikinga na Covid19 tu sayansi bado u mweupe Sana hata Hilo swali tukikujibu bado hutaelewa Bali utazidi kuchanganyikiwa tu.
 

mwanaspotiapp

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
547
1,000
Watu wa modern Physics wana tumia energy kubwa sana kutafta namna za kuzi pruv wrong fomular na law za mtaalam newton

Kwenye physcs ukiwasoma vizuri utagundua kua Eistain ni Negation ya Newton au unaweza sema Opposite

Mechanical Physics ni Opposite ya Modern na zile newtons law zinaenda oppsite na principle of reletivity hadi kufika kwenye time traviling zote zina pishana na law za Isaav newton

Kama unahisi hukubatiani na newton na alitoa maelezo ya uongo basi tambua wewe c wakwanza wala si wamwisho na hata Eistein kaacha theory nyingi za kupruv zile law kua ni wrong lakini hazijatoboa


Kwenye list ya binadamu walio badiri maisha ya binadamu kwa muda wote yangu dunia ianze asie nabii wa wa mungu ninyeye pekeake kwenye tatu bora kiwa na Muhammad S.A.W na Yesu massiah...

Dont mess with isaac he is more than jus a genius ndio maana kuna baadh ya makabila huko uguriki wanaamini alikua ni binadamu asie wakawaida ...

Soma vizuri principle pf releativity ilivyo eleze free fall ndio utajua kwanini newton anabaki kua newton.
 

racka98

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
903
1,000
We jamaa usiku wote huu unaleta hizo theorem za relativity dah nazichukia balaa enzi zile mechanics kwenye advance physics ilinifanye niachane na hiyo kitu nkahangaika na bios na chem now ndio zanipa ugali
Jamaa inabidi arudie mambo ya relative motion na projectile motion kuhusu relative velocity na terminal velocity za free falling objcets ataelewa kwanini hyo logic ni flawed.

Maji bado yanadondoka ila yanakua na relative velocity against hyo chupa kupata resultant. Ila mwimgine anaweza argue kuwa hayo maji na chupa yata collide humo ndani kupata total momentum ambayo ita treat hvyo vitu viwili kma body moja.

Kuhusu hvo zimaji vinavyochuruzika nje hvyo nanvyo theory ya relative motion bado inakua applied. Velocity ya chupa ukiidondosha itakua kubwa kuliko ya maji yanayochuruzika. Hvyo yanachwa nyuma lakini bado yatadondoka tu. Kwani ukiidondosha chupa hayo maji yanayochuruzika hayafiki chini?

Ukitumia theory ya projectile motion of a free falling body utaona mass (uzito) unaathiri speed ya kitu kudondoka na speed yake. Unategemea kweli vitone vya maji vilivyotoka kwenye chupa (sasa vipo kma independent bodies) vitakua na velocity sawa na chupa yenyewe yenye uzito zaidi ya mara 10 ya vitonye?
View attachment 1724911
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom