Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,005
- 4,664
Viongozi wa dini dua na sala zao zimeambatana zaidi na wana chama tawala. Na hata hao chama tawala siyo wote isipokuwa wale tu wenye madaraka. Ukishirikiana nao kisha ukapokonywa madaraka na wao wanakuacha na kuambatana na mteule mpya.
Maeneo mengi viongozi wa dini wanapokwekwenda kutoa huduma ya kiroho kwa wanasiasa lazima waitwe, hakuna siku wao kama wao wanathubutu kumkemea mwanasiasa.
Hakuna kongamano la dini lakukemea maadili linalowagusa wanasiasa moja kwa moja, kwao wanasiasa wasawi na wachafu wanaitwa watoto wa kaisari na wanaachwa wale ya kaisari.
Wapinzani wakianzisha vuguvugu la kudai haki viongozi wa dini lazima wabadili mahubiri na kuanza kutafsiri kama kuna uvunjifu wa amani mara tuheshimu viongozi waliowekwa na Mungu. Je Mungu alibariki binadamu waovu waachwe?
Shida ya viongozi wa dini nikukosa roho wa Mungu na kujawa na roho ya ajira na kutafuta mali au kupungukiwa maarifa ya elimu Dunia? Ni kawaida kabisa kukosekana kwa amani kwa kutotenda haki, wao panapokosekana haki badala wakosoe ubaki kusema Tuombee Amani. Je, ni wapi ambapo haki ilikosekana maombi yakaleta upatanisho? Kwanini wasioamini amani ni tunda la haki?