Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,033
- 151,255
Baada ya CHADEMA kupitia Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe kutangaza maandamano, wazo lilionijia ni CCM kutafu mbinu ya kuzuia haya maandamano yasifanyike na mojawapo ni kuwatumia viongozi wa dini.
Alichofanya leo Padri Kitine ni hatua tu ya awali ila mipango itakuwa teyari imeandaliwa au inaandaliwa ambapo viongozi wa CHADEMA na wa Serikali wataitwa Ikulu Sambamba na viongozi wa dini kujadili namna ya kumaliza hayo maandamano.
Baada ya kikao hicho cha Ikulu, Waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na hata DG wa TISS wataondolewa kama sehemu ya makubaliano na hili litafanyika kuwaridhisha viongozi wa CHADEMA na pia CCM na Serikali yake watataka kuonekana wamechukua hatua.
IGP, Kingai na Mafwele, ndio watakuwa wa kwanza kuondolewa ila watafutiwa kazi zingine lengo kusitisha maandamano na kumuokoa Bi Mkubwa na madhara ya watu kuuwawa au kuumizwa kwenye maandamano.
Watakubaliano mambo mengi zaidi ya hayo, ila haya niliyoyasema, lazima yatakuwa miongoni mwa hayo makubaliano bila kusahau madai ya wapinzani kuhusu uendeshaji wa uchaguzi wa Serikali za mitaa ambayo nayo yatajadilwa siku hiyo au katika tarehe nyingine watayokubaliana na baada ya kikao, maandamano yatasitishwa.
Kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa, uchaguzi unaweza kusogezwa mbele na kesi ya kupinga TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa inaweza kuondolewa mahakamani au ikaendela sambamba na mazungumzo.
Pia, sheria inayowapa watu wa usalama wa Taifa haki na mamlaka ya kukamata watu na kuwaweka ndani huku wakiwa na kinga ya kutoshitakiwa, inaweza kuwa ni moja ya hoja itayojadiliwa. kwani utaratibu huu mpya unalamikiwa sana na unahusishwa sana na kukithiri kwa vitendo vya watu kutekwa na kupotea.
Kwanini Padri Kitine anatumikq/atatumika?
Wataalikwa viongozi wa dini zote, lakini lazima Padri Kitine awepo na sababu kubwa ni moja tu: ushawishi alionao kwa wapinzani kwasababu siku zote amekuwa upande wa haki akiungana na wapinzani kukemeo maovu yanayoendelea nchini, hivyo ni rahisi kuwashawishi wapinzani katika kufikia makubaliano ya kusitish maandamano na mambo menginyo.
Hata hivyo, CCM watatekeleza baadhi ya mamba tena kwa muda tu na baadae mambo yale yale yatajirudia tena.
Kutakuwa na athari gani?
Wananchi na wanaharakati mbalimbali watakuwa disappointed, na kwa upande wa CCM, wataendelea kupoteza imani ndogo wapinzani waliyonayo kwao na hivyo huko mbeleni, kuna hatari ya wapinzani kuja kukataa kabisa kukaa chini na viongozi wa CCM na Serikali yake kujadili jambo lolote mpaka maafa yatokee.
Huu ndio utabiri na pia ndio mtazamo wangu wa mambo.
Nimemaliza, muda utaongea.