HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hatukatai michakato kuendeshwa haraka ila mianya inayoweza kuchipuka ndio itakuwa kikwazo kwa baadhi yetu.

PSRS wako fair kwa asilimia kubwa hata kama wanakumbwa na ucheleweshaji wa michakato.

Taasisi au mashirika ya kiserikali yakipewa jukumu la wao kufanya michakato itakuwa kichomi kwa walalahoi/wasio na koneksheni.

Nimewaza hivi, je wadau mna maoni gani juu ya mawazo yangu haya?
Fair ni pamoja na kuruhusu APPEAL, kuna watu wanakosa nafasi kimakosa, hizo ni nafasi za kazi sio matokeo ya Chuo. Kwenye utafutaji wa KAZI uwazi lazima uwe mkubwa zaidi.
Waweke utaratibu wa matokeo ya wazi, kama vijana wetu wameona hawahatendewa haki, waweke mitihani hiyo wazi.

Utaratibu uliopo unatoa fursa kwa watu kupendelewa katika usahihishaji na umekaa kama utaratibu wa shule wakati ile ni kazi.

Ushauri wangu, wakomae sana na APTITUDE test with rondom pick ups. Yaan unafanya mtihani online na once unaposubmit majibu yanatoka na alama unaziona na majibu yake.

Bado naona UTUMISHI wako na room kubwa sana ya Upendeleo na uuzaji wa mitihani, sisemi kwamba wote wamepita hivyo ila majority wanapita kwa mipango.
 
Aisee, naomba msaada wa kutranslate kwa English hizo duties za Accounts Officer II. Kimsingi kiswahili ni kigumu mno
Screenshot_20230209-184802_Samsung%20Notes.jpg
 
Back
Top Bottom