HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Wakuu na mimi naingia oral kwa mara ya kwanza, sema nafasi ni moja, hii ne green light kwangu kwa mwaka huu.

Pia niwatie moyo wale ambao wanasema utumishi hawasaishi pepa, nilifanya pepa ya UDSM hizi za juzi kati, na mimi pia nilijibu vizuri tu.

Nilipokuja jifanyia tathmini baada ya pepa niligundua maswali mawili sikuyajibu vizuri, hivyo yale malalamishi yangu ya awali kwa Sekretarieti ya Ajira juu ya usahaishaji nimeyafuta.

Hii oral yangu ya kwanza, kwakweli pepa yake ya written nilifanya vizuri na nilijua lazima nizame oral na imekuwa hivyo, ngoja nikapambanie hiyo nafasi moja.

Wakuu msikate tamaa.
20230208_110100.jpg
 
Mm sielewi wakuu nimepiga Pepa Interview zote mbili A MDSs & LGA, Accounts Officer (kwangu ilikuwa rahisi mnoo..) na Auditing Officer II (ilikuwa ngumu kiasi) maajabu sijaitwa hata accounts officer na nauhakika nimeifanya vizuri mnoo
 
Wakubwa Hivii Oral ya AFISA MIFUGO - MDA & LGA ni tarehe ngapii?

Mm naona selected for oral niki view timetable sioni oral timetable, nisaidienii??
 
Ndugu mimi toka 2018 nimekuwa naomba na naishia kupata marks hizo za 49 sikuwahi kupita kwenda oral toka mwaka huo mpaka mwaka jana mwishoni nilipoingia oral ya TRA ambayo ndo ilikuwa ya kwanza kwangu(imagine toka 2018 hadi 2022) na sikuwahi kukata tamaa, nikiitwa naenda na silalamiki hata nikikosa, niliamini wakati wangu bado. Hizi za MDA nimezifanya pasipo kujisomea maana nilikuwa sijui nisome nini, ila kwa knowledge niliweza kujibu na Mungu mwema zote nimeitwa oral. Imagine toka 2018 sijawahi kuitwa ila ndani ya miezi miwili nimeitwa oral tatu. Amini wakati wa Mungu ni wakati sahihi
Hongera sanaa mkuu
 
KWA KUWA, Mashirika ya umma yanayojiendesha kibiashara yanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi katika kujiendesha kwake kutokana na kutegemea mchakato wa ajira unaoendeshwa na Sekretarieti ya Ajira ya Utumishi wa Umma katika kupata watumishi;
NA KWA KUWA, Changamoto hiyo inaathiri tija ya uwekezaji na manufaa yaliyotarajiwa kupatikana, kutokana na kukosa watumishi wanaostahili kwa wakati hata pale ambapo Shirika la Umma linapokuwa na uwezo wa mapato wa kuwalipa mishahara
KWA HIYO BASI, Bunge linaazimia kwamba, Serikali iweke utaratibu maalumu wa kutoa vibali kwa taasisi zinazojiendesha kibiashara ili ziweze kuajiri zenyewe ajira za moja kwa moja na kuweza kuendena na soko la ushindani wa kibiashara.

from kamati ya bunge hapo jana
Hii imekaa vzr japo mchakato ukirudishwa huko kwenye taasisi kujuana kutakua kwingi sana naona
 
Back
Top Bottom