mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 14,192
- 19,118
Haina haja hiyo mzee naongea hivyo kulingana na experience yangu, maana nina majina mawili kwenye vyeti vyangu vyote vya taaluma ila matatu kwa Nida + cheti Cha kuzaliwa.
Tangu 2019 nafanya interview bila shida yoyote
Ni kweli busara inaonesha kuwa hapo hakuna shida yoyote. Lakini katika jamii si kila siku utakutana na watu wanaofuata busara!! Kuna mtu mwingine atakuambia kuwa katika kazi tunafuata sheria kwanza kabla ya busara!! Kisheria, Ahmed Mugisha ni mtu tofauti kabisa na Ahmed John Mugisha. Kisheria kinachoweza kufanya hao awe mtu yule yule ni deed poll na si vinginevyo. Japo busara inaweza kuonesha kuwa kama cheti cha kuzaliwa kina majina yote matatu ie Ahmed John Mugisha basi ni mtu yule yule, japo anayefuata sheria anaweza kusema hiyo ni coincedence tu au anaweza kusema hicho cheti cha kuzaliwa kimechezewa!!. Sasa kama mko wawili mnagombania nafasi moja, mmoja hana kabisa utata na majina, na mwingine kisheria kuna utata japo ki-busara hana utata, nadhani watamchukua yule ambaye hana utata kabisa!! Katika mazingira ya kusaka asali yenye ushindani mkubwa ni busara kuondokana na hata na harufu tu ya utata!!