HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hizi kazi za TRA, wengine kwenye attachments hasa Barua na CV tumeweka in docs/word na sio PDF na sijaona sehemu ya picha.
Hii inaweza kuleta shida?
 
Mie ndo ww mkuu..nahisi kama ntatemwa maana sikuattach picha.
Sasa pale unaattach wapi? Mfumo ni mbovu sana ule, Currrent Salary ya nini mule ndani?
Ukiomba kazi, hata kama ulikosea kupandisha attachment huone sehemu ya kuedit na kuondoa ulichokosea na kuweka kile ambacho kiko sawa.
Pamoja na mapungufu ya PSRS lkn kwenye Portal yao imekamilika sana.
 
Sasa pale unaattach wapi? Mfumo ni mbovu sana ule, Currrent Salary ya nini mule ndani?
Ukiomba kazi, hata kama ulikosea kupandisha attachment huone sehemu ya kuedit na kuondoa ulichokosea na kuweka kile ambacho kiko sawa.
Pamoja na mapungufu ya PSRS lkn kwenye Portal yao imekamilika sana.
Wangetumia tu portal ya psrs kuappy then mengine wafnye wenyewe mfumo bdo unachngmoto
 
Siku hizi hakuna anayeulizia database[emoji23], TRA wametuchanganya kwa kweli.. Jaman vp leo inatoka au matumain tuweke lini.. Pia kaka yetu makofia yuko wapi atupe za ndaniin kabisaaaaa
Leo bado patupu ,,database [emoji1787] iache tushakua hoves
 
Hizi kazi za TRA, wengine kwenye attachments hasa Barua na CV tumeweka in docs/word na sio PDF na sijaona sehemu ya picha.
Hii inaweza kuleta shida?
Nadhani inabidi tufungue Uzi WA job Tra,
 
"365 ZA KUJIVUTAVUTA"

View attachment 2637528


Leo ni tarehe 28/05/2023, ni mwaka mmoja kamili tangu sekretarieti ya ajira PSRS itangaze nafasi za kazi MDA&LGA (maarufu kama mkeka wa taifa) mnamo tarehe 28/05/2022.

Tukiwa katika maadhimisho haya mujarab ya kusherekea siku 365 za PSRS "kuendelea na mchakato" wa ajira tajwa hapo juu, ninakuletea makala "fupi" pamoja na maoni yangu ya jumla kuhusu kinachoendelea (ucheleweshaji wa michakato ya ajira).

Utangulizi:-
Rais wa awamu ya sita alipoingia madarakani, pamoja na mambo mengine, alifanya tathmini ya rasilimali watu serikalini na kugundua kuna upungufu mkubwa wa watumishi. Kwa kuanzia aliridhia kutangazwa kwa ajira 32,000 ili "kuziba magepu".
Katika ajira hizo, sekta za elimu na afya ndio zilikua na uhitaji mkubwa zaidi. Hayo yalielezwa na waziri wa utumishi wa wakati huo Mh Jenista Mhagama mnamo 6/4/2022.
View attachment 2637532

Wiki moja baadae Mh. waziri Mhagama alitoa mchanganuo kama ifuatavyo:-
View attachment 2637536
Hapo juu ni ajira za afya na elimu ambazo zenyewe zilitolewa kwa uratibu wa TAMISEMI.
Hadi sasa watu hao tayari wapo kazini na wameshakula mishahara zaidi ya nane.

View attachment 2637542
Hapo juu ni nafasi za kada zingine ambazo ziliratibiwa na PSRS. Kada hizi ndizo zilizozaa tangazo la kazi la MDA&LGA la 28/05/2022 (mkeka wa taifa) ambalo leo ndio tunalifanyia ANNIVERSARY au BIRTHDAY ya kutimiza mwaka 1 bila kukamilika.
"365 za kujivutavuta"
View attachment 2637562
Na huu ndio mwisho wa utangulizi.

Hadi sasa:-
PSRS hadi dakika hii na sekunde hii bado hawajakamilisha mchakato mzima wa kuwaajiri watu 2057 kwa mujibu wa tangazo tajwa hapo juu.
Sababu zinaweza kuwa nyingi, hata milioni zikafika, zinaweza kuwa zinawahusu wao au haziwahusu wao, lakini FACT ON THE TABLE ni kwamba ni mwaka sasa na bado hawajakamilisha zoezi hilo.

Maoni yangu:-

1. Nawapongeza PSRS kwa utendaji wao wenye "muonekano wa kutokua na upendeleo", lakini sifurahishwi na kasi ndogo ya utendaji wao. KUJIVUTAVUTA.

2. Mimi nitakua mtu wa mwisho kuamini kwamba utendaji wa PSRS hapa ndipo ulipoishia. Kwamba hakuna namna inayoweza kufanyika kuboresha utendaji wao. Na kama wao wanaamini "this is the best we can expect from them", basi kama taifa tutakua tupo kwenye shida kubwa mno.

3. Kuna madai kwamba PSRS "wanacheleweshwa na waajiri". Mimi nasema "if PSRS are innocent, then they are not smart". (They cannot be both)
Taasisi yoyote ile katika utendaji wake, inapaswa kutoa huduma bora ili "ijijengee reputation" yake. Kama wao PSRS wanabeba makandokando ya waajiri, yanayopelekea wao kuonekana wanatoa huduma mbovu, then they are not smart.

4. Aina ya utendaji wa PSRS inatoa mwanya kwa "wajanja" (taasisi zinazotaka kuajiri zenyewe) ziweze kuruhusiwa kufanya hivyo. Aina hii ya utendaji wa kutumia mwaka mzima kuajiri watu elfu mbili, ina suggest kwamba taasisi hiyo "imezidiwa na kulemewa" na hivyo inahitaji zaidi "kusaidiwa kazi" badala ya "kuongezewa kazi zingine."
Nimeona TRA jana wamefanya, endapo TPA nao wakitaka kufanya hivyo, inakua easy kuwashinda PSRS (kwa hoja mbele ya third party, awe Rais au PM) hata kama TPA watawakilishwa na bibi yangu mzaa baba katika kikao hicho.
Reputation ya utendaji ya PSRS kwa siku za hivi karibuni inawatafuna wenyewe.

Vipimo vyangu vya kutoridhishwa na kasi ya PSRS ni hivi hapa:-
A. Wanalalamikiwa na wanaowahudumia (job seekers). Ndio maana leo tuna huu uzi (Kwanini utumishi wanachelewesha.....)

B. Wanalalamikiwa na mkuu wa nchi. (Hakuna kitu kibaya kama hiki). Rais Samia ameshawahi kusikika akisema kwamba michakato ya ajira inachukua muda mrefu mno kukamilika. Na tangu siku hiyo mimi binafsi sijaona mabadiliko yoyote ya kasi ya utendaji wa PSRS katika hilo.

C. Ajira hizi (MDA&LGA) ni sehemu ya package ya ajira 32000 ukijumuisha na afya na elimu ambazo ziliratibiwa na TAMISEMI. Ukweli kwamba afya na elimu wao walishakamilisha michakato yao kwa zaidi ya miezi 8 iliyopita. Ukweli huu unawaweka PSRS katika mazingira magumu sana kuaminika kwamba kasi yao inatosha na inapaswa kutumainiwa.

D. Muda ni mali, kwa vyovyote vile iwavyo, umeshapita mwaka sasa bado PSRS hawajakamilisha zoezi hili. (28/05/2022 hadi 28/05/2023).

Nawatakieni nyote weekend njema na maadhimisho mema ya "365 za kujivutavuta".

Ulumbi.
Cio Tra pekee Bali na taasisi nyingine zitafanya saili zake, huku psrs wakiendelea na michakato Yao isiyo isha
 
Back
Top Bottom