Database mwisho ni miezi 6 tu.
Afu haina maana yoyote, yaani kwamba waliopo kwenye Database wanauwezo kuliko wengine? Mwaka mmoja ni muda mrefu kwa akili ya binadamu kuweza kuchakata vitu kwa usahihi.
Huu utaratibu hauna maana, ukikosa umekosa, hii hoja ya DATABASE nani anaikagua kujua kuwa waliopo ni sahihi?
Usaili una kufaulu na kufeli, KUFAULU ni KUPATA KAZI, na KUFELI ni KUKOSA KAZI.
Hii ya kuweka Database ya nini? Nchi ina wahitimu zaidi ya 100,000 uweke watu Database kisa nini?
Huo utaratibu ufutwe haraka sana. Ukifanya usaili iwe imeisha, watu waanze upya na maandalizi mapya.
Huu utaratibu unawanyima watu fursa ya kujiuliza wapi walikosea kwa maana hawapati nafasi ya kuomba nafasi au nafasi kupunguzwa.