HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Mbona wengine ni 80,000 hii imekaaje kitaalam?
Kitaalamu ni kwa mujibu wa nyaraka za serikali. Rais Samia alipandisha kiwango cha chini toka 80,000/= hadi 100,000/= na alipandisha kiwango cha juu toka 120,000/= hadi 250,000/=. Hakuna anayepaswa kulipwa chini ya 100,000/= na hakuna anayepaswa kulipwa zaidi nya 250,000/=, Ona hapa:

Dkt. Ndumbaro amesema kutokana na kibali hicho cha Mhe. Rais, posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma kwa kiwango cha juu imepanda kutoka shilingi 120,000/= hadi 250,000/= na kiwango cha chini kutoka shilingi 80,000 hadi 100,000/=.
 
Kwa maana hiyo, tulioandikia barua za kuomba posho ya kujikimu kwa kiwango cha 80,000 na degree holder tumejila sio[emoji38]
 
Mfano Veta hela ya likizo unalipwa kutokana na mshahara na sio umbali
Hicho kitu hakipo na bila shaka hujajua undani wake. Iko hivi: Pesa ya likizo inaweza kutofautiana kati ya watu wawili wanaofanya kazi kituo kimoja na wanakwenda likizo sehemu moja kama ngazi zao za mishahara zinatofautiana sana. Sababu yake ni kwamba:
1. Hadhi ya tiketi hutofautiana kati ya mtu na mtu kutokana na ngazi ya mshahara wake. Kuna wanaoruhusiwa kusafiri kwa ndege kutokana na kiwango chake cha mshahara na huyo atapewa nauli sawasawa na gharama ya tiketi ya ndege. Kuna mwingine hana hadi ya kupewa tiketi ya ndege lakini ana hadhi ya kusafiri kwa daraja la kwanza. Na kuna mwingine ngazi yake ya mshahara inamruhusu kusafiri daraja la pili na ndilo daraja la mwisho wa watumishi wote wa umma. Mtumishi wa umma hawezi kusafiri kwa daraja la tatu (tunaishukuru serikali kwa hilo.
2. Mtumishi wa umma apokwenda likizo anapaswa kulipwa half per diem kama safari yake inazidi masaa 6. Posho hii ya njiani hutofautiana kutokana na ngazi ya mshahara.
3. Mtumishi wa umma anapokwenda likizo hugharimiwa yeye, mke wake (kama anaye), watoto wanne (kama anao). Hawa wategemezi hulipwa kutokana na kiwango anacholipwa baba yao. Kuna ngazi zingine za mshahara mtu hugharimiwa hata na mtumishi wake.

Kwa kuwa malipo yote hayo hulipwa kama pesa ya likizo, ni dhahiri kwamba yatatofautiana kutokana na kiwango cha mshahara wa mtu hata kama hao watu wanakwenda likizo sehemu moja. Bila shaka umeelewa!!
 
Weiting for answer too
Inategemea na mshahara wako. Kiwango cha chini ni 100,000/= na kiwango cha juu ni 250,000/=.

Dkt. Ndumbaro amesema kutokana na kibali hicho cha Mhe. Rais, posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma kwa kiwango cha juu imepanda kutoka shilingi 120,000/= hadi 250,000/= na kiwango cha chini kutoka shilingi 80,000 hadi 100,000/=.
 
Kwa maana hiyo, tulioandikia barua za kuomba posho ya kujikimu kwa kiwango cha 80,000 na degree holder tumejila sio[emoji38]
Kwa kawaida unatakiwa kuandika barua kuomba kulipwa pesa za kujikimu kama waraka husika unavyoainisha kama stahili ya mwajiriwa mpya. Usitaje idadi ya siku kama huna hakika nayo, na usitaje kiwango kwa siku kama huna uhakika nacho (Lakini ni vizuri zaidi kutaja kama una uhakika nazo). Kwa kawaida mwajiri HAWEZI kukulipa chini ya kiwango na akawa hana hatia. Lakini ukitaja kiwango cha chini mwenyewe kwa ridhaa yako, anaweza naye kuridhia kukupa kiwango ulichoomba na asiwe na hatia, (japo anaweza kukupa kiwango sahihi na asiwe na hatia pia). Tatizo ni maafisa utumishi huwa hawtoi elimu hii kwa waajiriwa wapya japo ni moja ya majukumu yao. Piaa wengi wamo humu wakisubiri kulamba asali, lakini wakipata hugeuka miungu watu na kuanza kuwatesa wenzao!
 
Ni kweli kabisa mkuu, hatupewi elimu jinsi mambo yanaenda.
 
Inatolewa kwa uzingatia
a)Taasisi
b)Elimu
Naomba niweke sawa: Stahiki zote za watumishi wa umma kwa maana ya serikali kuu na taasisi zake na serikali za mitaa hutolewa kwa mujibu wa Government standing orders na nyaraka za serikali. Hakuna taasisi ya umma itakayoweza kulipa posho kama inavyotaka yenyewe. Japo kuna taasisi ambazo ziko vizuri na hiyo posho hutoka kwa wakati bila usumbufu lakini zingine ziko choka mbaya na hutoa hizo stahiki kwa mbinde na mikiki mikiki hadi mtu akomae kudai sana. Pili posho hutoka kwa kuzingatia ngazi ya mshahara na siyo elimu (japo mara nyingi elimu ya juu huendana na mshahara wa juu pia, lakini kigezo ni mshahara.)

Yako mazingira ambayo mwenye elimu ndogo ana ngazi kubwa ya mshahara kuliko mwenye elimu ya juu, na kwa hiyo posho yake ya kijikimu inaweza kuwa kubwa zaidi. Moja ya mazingira hayo ni uzoefu kazini. Mtu wa elimu ya chini labda ana diploma lakini ana muda mrefu sana kazini na ameshakuwa principle officer kwenye kada yake na ngazi yake ya mshahara labda ni TGS G. Na mwingine ana digrii na ameajiriwa hivi karibuni mshahara wake ni TGS D. Huyo wa diploma bado atapata posho kubwa kwa mujibu nwa ngazi yake ya juu kuliko huyo wa digrii ambaye bado ngazi nyake ni ya chini.
 
Nimesoma majibu yote uliyojibiwa kuhusu jambo lako, mimi nakushauri hivi pia.

Tafuta hela ya kutosha inayoweza kukukalisha kule kwa angalau siku 5.

Ukiripoti waulize watatumia muda gani kukuita rasmi ukaanze kazi, wakikuambia haijulikani ila watakupigia simu, nakushauri urudi nyumbani uje usubiri hiyo simu. Nauli ya Kasulu - Kibaha haiwezi kuwa kubwa na gharama utakayotumia kukaa kule kwa siku angalau 3.

Au kwa kusamaraizi, karipoti halafu rudi nyumbani, nauli ya kwenda na kurudi haiwezi kuwa kubwa ukilinganisha na gharama utakayotumia kukaa kule kwa angalau siku 3.

Reference: Case study.

Kuna mlamba Asali wa JKCI alitoka mkoani akapeleka barua, akaambiwa asubiri kupigiwa simu akakaa Dar kusubiri, zikapita wiki 2 bado hajapigiwa, hadi akakaukiwa mfukoni akaanza kulalamika(alileta uzi humu), tukaanza kumwambia alikosea, alitakiwa kurudi nyumbani kwanza.

Na wewe usije ukafanya hilo kosa.
Shukran sana mkuu 🙏🏼
Nmepata kitu hapa
 
Pesa yote kimsingi hutoka hazina. hata kama ikikusanywq na halmashauri mwisho wa siku hiyo pesa inaingia kwenye mfuko mkuu wa serikali lakini hesabu inaonesha kila halmashauri imekusanya kiasi gani. Matumizi ya halmashauri ni kwa mujibu wa bajeti yao na hutoka hazina (zikiwamo hizo hizo walizokusanya wao).
Okay nimekuelewa. Nashukuru.!
 
Inategemea na mshahara wako. Kiwango cha chini ni 100,000/= na kiwango cha juu ni 250,000/=.

Dkt. Ndumbaro amesema kutokana na kibali hicho cha Mhe. Rais, posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma kwa kiwango cha juu imepanda kutoka shilingi 120,000/= hadi 250,000/= na kiwango cha chini kutoka shilingi 80,000 hadi 100,000/=.
Naona hii iko too general hivi hakuna sehemu iliyoandikwa may be mwenye scale flani kiwango chake ni kiasi flani katika hiyo range?
 
Naomba niweke sawa: Stahiki zote za watumishi wa umma kwa maana ya serikali kuu na taasisi zake na serikali za mitaa hutolewa kwa mujibu wa Government standing orders na nyaraka za serikali. Hakuna taasisi ya umma itakayoweza kulipa posho kama inavyotaka yenyewe. Japo kuna taasisi ambazo ziko vizuri na hiyo posho hutoka kwa wakati bila usumbufu lakini zingine ziko choka mbaya na hutoa hizo stahiki kwa mbinde na mikiki mikiki hadi mtu akomae kudai sana. Pili posho hutoka kwa kuzingatia ngazi ya mshahara na siyo elimu (japo mara nyingi elimu ya juu huendana na mshahara wa juu pia, lakini kigezo ni mshahara.)

Yako mazingira ambayo mwenye elimu ndogo ana ngazi kubwa ya mshahara kuliko mwenye elimu ya juu, na kwa hiyo posho yake ya kijikimu inaweza kuwa kubwa zaidi. Moja ya mazingira hayo ni uzoefu kazini. Mtu wa elimu ya chini labda ana diploma lakini ana muda mrefu sana kazini na ameshakuwa principle officer kwenye kada yake na ngazi yake ya mshahara labda ni TGS G. Na mwingine ana digrii na ameajiriwa hivi karibuni mshahara wake ni TGS D. Huyo wa diploma bado atapata posho kubwa kwa mujibu nwa ngazi yake ya juu kuliko huyo wa digrii ambaye bado ngazi nyake ni ya chini.
Mkuu per diem za safari ni mapato ya ndani, taasisi ikiwa vizuri inaongeza tu hio per diem hata hawajali. Mfano kuna sehem ma juniour officer graduate wanaanza na 170k per diem, na pesa ya kujikimu ilikua 1.5M.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona hii iko too general hivi hakuna sehemu iliyoandikwa may be mwenye scale flani kiwango chake ni kiasi flani katika hiyo range?
Hizi ndio perdiem mpya kulingana na scale za mshahara
Screenshot_20230512-143531.jpg
 
Mkuu per diem za safari ni mapato ya ndani, taasisi ikiwa vizuri inaongeza tu hio per diem hata hawajali. Mfano kuna sehem ma juniour officer graduate wanaanza na 170k per diem, na pesa ya kujikimu ilikua 1.5M.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo kitu hakuna na haiwezekani kwenye utumishi wa umma. Yatakuwa ni malipo mengine na si subsistance allowance!! Labda kama ni masurufu na mwisho wa siku itabidi ayarejeshe akionesha alivyotumia. Hakuna taasisi inayoruhusiwa kulipa zaidi ya viwango vilivyoainishwa na huwa kuna external auditing kubaini kama matumizi yanalingana na taratibu na nyaraka za serikali zilizopo. Kinyume cha hapo ni ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma. Rejea post ya Mwifwa hapo juu!!
 
Back
Top Bottom