zoga
JF-Expert Member
- Jul 6, 2016
- 780
- 1,532
PSRS unajua imewekwa kwa ajili gan Kiongozi kama tunaongea kwa style hiyo...PSRS ndio wanaofanyisha usaili kwa niaba ya waajiri kwenye utumishi wa umma. Kwa maana hiyo ni lazima PSRS watoe matokeo rasmi ya usaili wao, na kuwajulisha wahusika rasmi. Katika ngazi ya mtu mmoja ni lazima apewe barua ikimwarifu kufaulu usaili na kuitwa kazini. Waajiri lazima wapewe taarifa pia ya usaili maana psrs ilifanya kwa niaba yao. Usichanganye utumishi kama wizara na PSRS kama kitengo ndani ya utumishi. Waajiri huomba kibali utumishi cha kuajiri, utumishi ina jukumu la kuangalia kama serikali ina nafasi ya kugharimia ajira hizo, kwa maana ya mchakato wote na mishahara ya waajiriwa wapya. Utumishi wakijiridhisha kuwa fedha ipo, hutoa kibali kwa waajiri cha kuajiri. Hapo ndipo psrs wanapewa jukumu la kutangaza, kufanya usaili na kuchagua waajiriwa kwa niaba ya waajiri. Anachopewa mwajiriwa na PSRS si kibali cha ajira bali ni wito wa kuripoti kazini (kwa mwajiri) baada ya kufaulu usaili.
Samahani
mfano :ww ni agent wa Bia ....unapoagiza idadi ya Bia kiwandani...Kiwanda wanakutumia picha wakati wanapakia au wanakuletea idadi uliotaka!