Orosso
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 962
- 2,308
Katika ajira ambazo hazikushindaniwa kwa usawa ni zile za mahakama, hizi za bunge kilichobadilika ni maombi tu kutimwa kwa katibubwa bunge, mwaka jana maombi yalielekezwa kwa katibu psrs, ni maboresho madogo.Unajua tume ya utumishi wa Bunge na Mahakama wanakuga na watu wao wanaofanya internship hivyo mara nyingi matangazo yao ya Ajira huwa ni kukamilisha ratiba tu, ndio maana unakuta wanatangazaga nafasi ambazo ukiangalia hizo kada unakuta zina watu ambao tayari walishafanyaga saili za PSRS na wapo data base, mfano miezi miwili nyuma walitangaza Accounts officer wakati huo watu walishafanya Accounts officer za Mda&Lga, pia jana wametangaza financial management officer wakati mwezi February kuna watu wamefanya nafasi hiyohiyo TPDC.
Pia mwakajana Tume ya utumishi wa mahakama walitangaza nafasi za Accounts officer ili hali pia nafasi hizohizo zikatangazwa na PSRS kwa upande wa MDA&LGA, ndipo hapo panaleta mkanganyiko kwa hizi taasisi za Serikali naona hapa kuna double standards baina ya taasisi za Serikali.
Za tume ya mahakama mwaka jana, walitumia portal yao katika website yao, kigezo kikuu kilikua ku-apload passport size photo, ajab ilikua, baada ya siku moja au mbili toka tangazo litoke, haikua inawezekana tena ku-upload photo, nyomi ikapunguzwa hapa.
Ikaja katika kuita usahili, wakaelekeza watu waende na PC zao, walichokutana nacho, kila mmoja alisema lake, kifupi ni kama walikua na watu tayari, kibaya walishindwa kuendesha mchakato katika usawa na uwazi, ilikua mchakato wa aibu mnoo kwa taasisi ya kusimamia haki kama ile, baada ya mchakato, wakatoa feedback ya uongo na kweli katika website yao kuonesha kuwa walisimamia ushindani kwa haki na usawa, aibu mnoo.