HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Katika ajira ambazo hazikushindaniwa kwa usawa ni zile za mahakama, hizi za bunge kilichobadilika ni maombi tu kutimwa kwa katibubwa bunge, mwaka jana maombi yalielekezwa kwa katibu psrs, ni maboresho madogo.

Za tume ya mahakama mwaka jana, walitumia portal yao katika website yao, kigezo kikuu kilikua ku-apload passport size photo, ajab ilikua, baada ya siku moja au mbili toka tangazo litoke, haikua inawezekana tena ku-upload photo, nyomi ikapunguzwa hapa.

Ikaja katika kuita usahili, wakaelekeza watu waende na PC zao, walichokutana nacho, kila mmoja alisema lake, kifupi ni kama walikua na watu tayari, kibaya walishindwa kuendesha mchakato katika usawa na uwazi, ilikua mchakato wa aibu mnoo kwa taasisi ya kusimamia haki kama ile, baada ya mchakato, wakatoa feedback ya uongo na kweli katika website yao kuonesha kuwa walisimamia ushindani kwa haki na usawa, aibu mnoo.
WW jamaa, muongo sana
 
Katika ajira ambazo walifanya poa ni za mahakama, system ilichuja kabisa ikachukua watu wachache wenye ufaulu wa juu ndio wakaitwa kwenye pepa ya mchujo (ilisaidia kuwapunguzia watu usumbufu na kupoteza nauli) na kwenye hiyo pepa ulikua unafanya mtihani uku unazijua max zako kabisa maana kama umekosea jibu palepale unaambiwa umekosea jibu kwahiyo walitoka wakijua max zao kabisa. Kuna jamaa nawafaham waliingia hadi oral na wawili walipata kazi bila kuunganishiwa na mtu inshort uwezo wao uliwabeba. Ingawa ile system watu waliokua wanajitolea mahakama iliwachinja maana wengi walikua na uhakika wa kuajiliwa kama ilivyokuaga miaka ya nyuma
mazaga one 👆 soma apo,
 
Umezuunguka, umerudi mule mule tu, mahakama haikutenda inavyopswa kutenda, haikusimamia haki wala usawa katika kushindanisha hizo nafasi.
Uelewe pia, hoja hapa sio tu kwa sababu mtu anajitolea, ikitokea nafasi apate nafasi, nchi hii, kupata tu nafasi ya kujitolea n lazima kuwa na connection yenye nguvu, hasa katika mamlaka kama hizo.
Mchakato uwe fair, sio kwa intern wala non-intern, nafasi zishindaniwe kwa haki.
SS kama walipata connection ya kujitolea, kuhusu ajira walishindwaje kupata connection ya kazi, ni
Sema hao wanaojitolea walikuwa wamebweteka wakijua wanapita Kwa sababu ya uzoefu wao wa kufanya kazi, kumbe mtihani is about theory na sio mpango kazi

Na siunajua Tena ukisha jitolea unajisahau kama bado ww sio mwajiri
 
Nchi ya ovyo hii ,kuna kitu nataka kufahamu hivi kukiwa na tofauti ya spelling kwenye birth certificate na vyeti vya taaluma je naweza tumia affidavit kuhudhuria usahili wa psrs au lazima niwe na deedpoll
Tusilaumu bure....wanapokwambia karekebishe majina yako wanamaana yao huko mbeleni usipate changamoto zikitokea tuwe tunakubali mapungufu/makosa mimi limeshawai kunitokea....
sasa hivi computer zinatema jina ukikosea
mfano.Benson kitamburisho cha taifa kimeandikwa
Ukija kwenye cheti wameweka Bensoni ....

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Group lishavamiwa na wafanyabishara sasa. Hii haikubaliki humu jamn fungueni uzi wa biashara au utafute uko ndiko patakufaa humu ni mambo ya Ajira tu na vipi tutafanikiwa kwenye izo Ajira.
Kbisa hii sio sawa
 
Group lishavamiwa na wafanyabishara sasa. Hii haikubaliki humu jamn fungueni uzi wa biashara au utafute uko ndiko patakufaa humu ni mambo ya Ajira tu na vipi tutafanikiwa kwenye izo Ajira.
I wish i could be Mudi
 
Kwakuongezea tu hapo, majibu ya aptitude test yalitolewa sakumi na moja alfajiri wakati oral inaanza sambili asubuhi siku hiyo hiyo, kada karibia zote zilifanyishwa oral interview na panel moja ya watu watatu, majina ya walioitwa kazin hayakutangazwa, walitumiwa SMS kwenye sim pamoja na kutumiwa e-mail
Ila Tanzania tunamambo ya ajabu sana watu wanafanya ubuni kama huo na wanachwa, majibu saa kumi na moja alfajiri paper saa mbili ni kuwatoa kwenye mchezo mfeli hayo mambo wanafanya wanazani wanafaulu sana kumbe wataulizwa siku moja mbele ya haki hizi kazi tutaziacha tutakufa unambania mtu bila sababu
 
Back
Top Bottom