Inaweza ikawa ni mtu wa kujifunza kweli, lakini katika hili, pamoja na kupata kwako taarifa hakujasaidia lolote katika uzi huu, uzi unahoji nini kinachopeleka kuchelewa placement badaada ya oral, limeongezeka lingine hapa, nini kinakwamisha kutolewa kwa pdf la database ilhali deadline imeshapita toka waziri atangaze.
Ingekua una lengo lankutia moyo watu humu, ilifaa, utueleze hapa, jamani kwa maaelezo niliyopata toka psrs/moja wa watumishi psrs ni kuwa, placement huchelewa kwa sababu kadhaa, moja,.... Pili,.... Tatu... Hapo ungekua umesaidia wengi humu, sio kwa hoja zako za kipindi hiki, watu wakihoji, jibu kuweni wavumilivu, mara watu wajiandae vya kutosha, mara wtau watenge muda kujisomea yaani iwe ratiba kabisa kama walevi walivyojiwekea ratiba kupata vitu vyao.
Kuna mengi watu wanahitajibkujifunza kupitia uzi huu, dodoso la kinachoendelea baada ya oral, kinachopelekea kucheleweshwa sana placement, na sasa limeongezeka, nini ni kikwazo dhidi ya pdf la database.
Hizi mambo za kukata tamaa sidhani kama zina uzito kutolewa ma mtu kama wewe, ndio maama kila sahili watu wanahudhuria pamoja nankuwa wanakandwa, nasisitiza, umesema wewe ni mtu wa kujifunza, na ukaitumia fursa ya kukutana na psrs kuzungumza nao, na wamekueleza mengi, ni wasaa sasa kutueleza hapa nasi tujifunze na kufaham hasa kinachopelekea kuchelewa kwa placement.