Mkuu hadi nakuja kuandika hapa najua kila kitu kuhusu watu kuitwa kikanda, kwahiyo kuhusu Ku search jina la muhusika nilifanya hivo kote na sikuliona
Kitu kingine, me pia nilikuwa ni mkandwaji japokuwa nilifanikiwa kufika Oral ila najijua kuwa sikufanya vizuri, kwahiyo sitoshangaa kama nitakosa hiyo Ajira
Sipo hapa kutetea secretariat ya Ajira, bali nilikuwa najaribu kuweka mambo sawa, maana ata Mie nilivoona post ya Kada yangu namie nika react kama ilivo kwa watu wengine
ila ili kujiridhisha ndomana nikaamua Ku search hilo Jina, ndomana pale juu nikashauri
yesamrich ajaribu Ku search nayeye, me sikujua kama kashacheki
Sioni mantiki ya kuanza kubishana kama watoto inashangaza sana, Kwa kutumia busara tu ilikuwa ni easy tu, kujibiwa kuwa nimeshacheki na Jina lilikuwepo sidhani kama ingemcost chochote
Kuna maisha baada ya hizo Ajira za utumishi, kama ni kazi wote tunzitaka ila tunajua fika kuwa hatuwezi kupata wote, tujifunze kukubali na kuridhika, tujiandae kisaikolojia mapema maana wengine wanahisi wanastahili kupata hizo kazi kuliko wengine