Wakuu nimeona mnalalamikia tangazo la kuitwa kwenye mkando Mzumbe lililowekwa leo kwenye website ya PSRS.
Naomba niwaambie hii sio mara ya kwanza kitu kama hiki kutokea kwa Chuo cha Mzumbe, kilitokea na Mwaka jana, watu walilalamika hivi hivi.
Ukiangaliwa hilo tangazo limeandikwa na Chuo cha Mzumbe na likatolewa na Makamu Mkuu wa Chuo na sio Katibu wa PSRS. Tukumbuke pia hizi Mamlaka za Vyuo vikuu wanaendesha sahili zao chini ya Usimamizi wa PSRS.
Kosa ninaloliona kwenye kuchelewa kutangazwa kwenye website ya PSRS ni uzembe/kosa la Chuo kutotuma tangazo mapema PSRS ili litangazwe, wao chuo huwa wanatangaza kwenye website yao ila wanasahau kulituma mapema PSRS na likatangazwe kule.
Pia MUCE mwaka jana walifanya uhuni kama huu wa kuchelewa kutoa placement badala yake watu walipigiwa simu wakaenda kuanza kazi kimya kimya halafu baadae ndio wakaja kutuma placement PSRS ili ikatangazwe. Muhanga wa hii kitu ya MUCE alikuwa ni
Ahmet , alifanya oral akawa anasubiri placement kumbe wenzio washaitwa kazini kimya kimya, placement ilipotoka na akawa hayumo ndipo akaja kujua kumbe watu waliitwa zamani kwa simu.
Hizi ndio taasisi zinazopigiwa chapuo na baadhi yetu humu ili zipewe mamlaka ya kurecruit na huu ndio uhuni wao wanaoufanya ingawa sio zote.
Nashauri endapo ukipata received ya Taasisi ya Chuo jitahidi kutembelea website zao mbali na website ya PSRS ili endapo wakichelewa kuleta tangazo PSRS ilihali tayari washalitangaza kwenye website yao uweze kuliona.