Kikubwa vijana wenzangu huu muda wa kulalamika humu ungetumiwa kujipanga Kwa ajili ya Usaili ingependeza sana...
Hawa Utumishi Mimi binafsi naona hawana shida,nadhani mwakani kila kitu kitaenda sawa tu.Mnajua huwezi kuajiri watu wengi Kwa mkupuo,unatoa Gape kidogo Kwa ajili ya kushughulikia mishahara nk........
Ndio maana unaona hata Leo hii,Wameanza Uhamiaji,Polisi hadi sasa Hakuna PDF,halafu baadae unaona JWTZ wametangaza kazi.....Ma gape lazimaa. Vivyo hivyo kwenye kukamilisha Taratibu za Ajira,watu wengine Wanaanza wanapewa malipo na wengine wanafuatia hivyo hivyo.....
Mimi nashauri wenzangu tutumie fursa hii ya kujisahihisha kutokana na saili zetu za Nyuma kufanya vibaya,iwe chachu ya kujiandaa vyema,kusoma Kwa Bidii na kufanya mazoezi ya Kuongea kila siku hata kujiangalia kwenye kioo,Yaani uwe vizuri kwenye kujiamini nk..
Naimani kila Mmoja wetu akifanya haya saili zijazo humu kila mtu atafanikiwa na tutaongea Lugha Moja na hamtalalamikia Tena PSRS,Binafsi mdau
Mwifwa kwangu alikuwa darasa tosha la kutokata tamaa,nilijifunza vingi nilijisahihisha na baada ya Oral nikasema Shida ya PSRS ni kuchelewesha Placements tu ila mengine ni Juhudi zako mtu mwenyewe.
Lakini pia baadae nikajipa muda wa Kujifunza pia,nikagundua Taasisi husika ndio huwa zinachelewesha baadhi ya michakato baada ya Usaili kwenda Kwa PSRS,Ukiona Taasisi yoyote placement imetoka haraka baada ya Oral basi ujue Taasisi hiyo imekamilisha kila kitu haraka mahitaji ya PSRS...
Ndugu Zangu,tuzidi kumuomba Mungu na hii mitandao tuitumie vizuri,tusome zaidi na Kujifunza mengi,Hakika wote tutalamba Asali.Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwake Ajira zinamwagwa za kutosha,Kikubwa mbinu kwetu vijana ni kufualu saili tu,maana Wasomi tupo wengi na ajira Zina ushindani sana.
Sekretarieti ya Ajira endeleeni kufanya kazi Kwa weledi,kufuata kanuni hivyo hivyo,Ili vijana wengi tushuhudie na tuwe mawakala Wazuri kwenu siku zote.Sisi tunasimana nanyi tunajua mlivyo Makini na mnajua vyema mmebeba dhamana za vijana wengi...
#Kazi Iendelee
#PSRS