Nimesoma mijadala mingi ya watu kukosoa utumishi wengine kuwatetea ila kiukweli kuna sehemu hawa jamaa wanazingua big time.
Haiwezekani mchakato wa ajira kuanzia tangazo la kazi hadi placement lichukue zaidi ya miezi 9, lazima kuna sehemu haipo sawa.
Ngoja nielezee kisa kimoja hivi.
Mwezi wa 3 2022 utumishi walitangaza nafasi za ajira ya mkataba wa miezi 3 (wizara ya ardhi), wataalamu tukaomba fresh.
Ilipofika tar 26 April, majina ya interview ya oral yakatoka, usaili unaonesha tutafanya tar 2 May Singida Lake secondary.
Wataalamu tukakata ticket ili kuanza safari hiyo tar 1 May. Nakumbuka nipo kwenye bus la Singida saa 1 asubuhi ndo tunaingia kibaha, napigiwa simu na rafiki yangu anasema utumishi wameweka tangazo lingine kwamba hakuna interview bali tunatakiwa kuripoti tar 9 May kwenye vituo vya kazi tulivyopingiwa(waliainisha kwenye tangazo).
Imagine tangazo la mabadiliko limetolewa saa 12 asubuhi May 1, kuna watu walikua wanatoka Mtwara hawa walishanza safari tangu April 30, wanakuja kupata taarifa kama hii.
Wengi tulilalamika sana kuchomeshwa nauli zetu, ila ndo hivyo hatukua na jinsi.
Ndo kama ishu iliyotokea leo, Tangazo linaonesha ni la tar 10 ila limetolewa leo tar 15 likionesha interview tar 16[emoji119]
Sent using
Jamii Forums mobile app