HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hongereni sana walamba asali wote, karibuni sana utumishi wa umma.
Naamini wengine zamu zao zonakuja ziko njiani ni suala la muda tu. Naomba tuwe inspirations kwa kila mmoja, hakuna kukata tamaa katika harakati za kusaka asali ya taifa.


#HII NI YETU SOTE.
 
Mazaga one tupe feedback ya status
Je Jana ulipigiwa simu au kutumiwa message kabla placement haijatoka
Kwa kweli niliingia Whatsapp nikaona hongera nyingi na PDF Juu,ikabidi niende faster kwenye Web kudownload tangazao jipya.
Lakini Wakati huo Kuna simu nyingi za wadau zikawa zimepigwa na wengine nilikuwa sijawasiliana nao muda mrefu kidogo.
 
My Eyes full of joyful tears with this shocking news, congratulation brother!

Ulituanzishia uzi, ukawa ni Lulu miongoni mwetu katika hii safari ya kuusaka mrija wa Asali.

Wengi tumeingia kwenye mrija wa Asali na tunaendela kuingia kupitia uzi huu na leo wewe una ungana nasi kwenye mkongo wa Taifa wa Asali.

Karibu sana kwenye Utumishi, uvumilivu uliouonesha hapa ukawe nguzo kwenye Utumishi wako.

Wale ambao bado mnaendelea kusubiri mrija wa Asali, msife moyo tupo pamoja nanyi. Tunaingia kwenye mrija wa Asali makundi kwa makundi na kila kundi lina muda wake. Tuwe na subira!
Amen brother
 
Ndugu Zangu nawashukuru sana,tuendelee kupambana,nami ni mojawapo niliyepata placement Jana.Sio Kwa uwezo wangu ila najua ni Kwa uweza wa Mungu pekee.
Tusikate tamaa,mapambano yaendelee.
Napenda kuwatakia kazi njema watumishi wote wa
Sekretarieti ya Ajira.Hili ndio kimbilio letu wasaka Ajira wote.Sina connection nilipambana baada ya kufeli saili kadhaa bila kwenda Oral.Ila sikuchoka niliamini kama ipo na ipo.Hatimaye siku imefika.
Wale wote mnaosubiri placements pia msikate tamaa,Kikubwa ni kuombea mchakato wako kila siku,Mungu ni mwema sana.

#Tusikate Tamaa.
#Kazi Iendelee
Hongera mkuu
 
Tangazo kwa waajiriwa wapya TRA linaweza kutoka tarehe 14 March 2023alafu tarehe 18-19 March jumamosi na j2 ni usajil na j3 tarehe 20 March tukaanza training.
Uwakika au....maana ule mkeka ulitoka haraka sana kiasi kama walisahau watu wengine kuendeleza
 
Sawa mm nikafikiri utumishi kabla hawajashusha pdf wanakutafuta kwanza.

Status inasomekaje
Hahaha Mkuu Yaani umefanya usaili na kufika Oral ushindwe kuwa unachungulia Placements pale ilhali ndio mchongo unaokuwa unausikilizia......
Hata akina na wengine wote ambao tulifika/walifika oral,muda wote walikuwa wanachungulia sehemu ya placement pia..
yesamrich
mfwende sawadogo

Status ni Selected For Oral Interview,Web and App...
 
- nani kakudanganya maswali yale manne/ matano Ndio kipimo Cha U-Genius?
-kwa hiyo wewe wa IFM unajilinganisha na wa Harvard,? Vigezo vya kujiunga IFM division hadi Three, Harvard je?

Tangazo kwa waajiriwa wapya TRA linaweza kutoka tarehe 14 March 2023alafu tarehe 18-19 March jumamosi na j2 ni usajil na j3 tarehe 20 March tukaanza training.
Umetoa wap hzi habar kiongozi
 
Hahaha Mkuu Yaani umefanya usaili na kufika Oral ushindwe kuwa unachungulia Placements pale ilhali ndio mchongo unaokuwa unausikilizia......
Hata akina na wengine wote ambao tulifika/walifika oral,muda wote walikuwa wanachungulia sehemu ya placement pia..
yesamrich
mfwende sawadogo

Status ni Selected For Oral Interview,Web and App...
Ubaya wa selected for oral ni hujui kama utakuepo au lah,tofaut na NOT mtu akiona anajua kabisa shughuli ishaisha.
Anyways wacha tusubri.
 
Back
Top Bottom