HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Very fact.!
Naomba niongezee kidogo hapa, takwimu zinasema, vijana takribani milioni 1 huhitimu mafunzo mbalimbali kwa mwaka. Kati ya hao, vijana 40000 hupata ajira serikalini na vijana 350000 hupata ajira katika sekta binafsi. Hivyo soko la ajira lina ushindani mkubwa sana.
Tuendelee kupambana na kusali, Mungu atatusaidia.
 
Takwimu zinaonyesha wenye GPA kubwa Huwa wanakula sana ndoige hawapatagi mchongo mapema na wanakula sana ndoige kwenye sahili
Hii haina uhusiano wowote na kufaulu usaili labda tuu uwe umeamua kubeza watu wenye GPA kubwa.

Lakini pia utambue katika kufaulu usaili au kupata mchongo ni zaidi ya performance ya darasani labda kama umeamua other factors kuziweka constant.

Kama unakumbuka kuna watu (wenye GPA ndogo na GPA kubwa) wameshafanya usaili taasisi A hawajapata lakini wakaja kufanya taasisi B wakapata pia.

Takwimu hizo unazozungumzia umeziona wapi? Nani alizitoa? Au ni assumptions? Inatakiwa unapopata kazi au kufanikiwa uwe na positive mindset kwa watu ambao hawajapata ili ufurahie mafanikio yako na yao pindi watakapo pata wao pia.

Kumbuka, katika kufanikiwa kuna wakati sahihi wa Mwenyezi Mungu ambao amekuandalia uje ufanikiwe na pia ujue wewe unaweza ona hao wenye GPA kubwa hawana mchongo au hawafaulu kumbe Mungu wetu Mkuu amewaandalia fungu na sehemu bora zaidi maishani mwao.

Shukuru Mungu kwa mafanikio yako lakini bila kubeza mapambano ya watu wengine. Ni hayo tu.
 
Tangazo huwa linatoka siku ya J4 ili jumamosi na j2 ni usajiri na j3 kuanza training TRA
Screenshot_20230309-131203.png
 
Wat tumesoma uko uko na sa hv ni employees wa TRA we wa udsm Bado unasaga rumba hahah
Mambo haya ya kutambiana umesomea wapi yalishapitwa na wakati. Una uhakika gani kama na yeye anasaga rumba? Una uhakika gani ni graduate wa UDSM na sio vyuo vingine?

Kama umepata kazi TRA furahia bila ya wewe ku attack chuo/vyuo vya wengine. Kitu kizuri ungetakiwa umueleweshe kuhusu dhana potofu ya kutambiana vyuo.

Maana kutokana na statement yako Kuna graduate wa hivyo vyuo/chuo wanaweza kujisikia vibaya kama wewe ulivyojisikia vibaya maana haya maisha ni game of chance, una weza graduate sehemu yoyote hapa nchini na still ukakosa kazi so bado point yako na yake haina mashiko.

Tushukuru kwa Mungu muweza yote kwa kutupatia nafasi ya kutimiza malengo yetu lakini pia isiwe sababu ya kubeza watu ambao wanapambania malengo yao. #SeeYouAtTheTop,[emoji120][emoji471][emoji3577].
 
Duh kumbe ni 2019... mwaka huu wameambiwa wakae na simu karibu
Kwani wakitoa Tangazo utumishi kunashida gani la kuripoti kutuo cha kazi kuliko kupiga simu mwisho wa siku lawama au IT hapo utumishi kufanya update kwenye application zao nayo ni ngumu...Tz tupo nyuma sana kidigitali
 
Tushavuta sana kaka
28/11/2022
28/12/2022
28/01/2023
23/02/2023
09/03/2023.......................
Noma sana,kama kijeshi tumeshaiva,Sifa uvumilivu Waziii !.....
Na uvumilivu unatamani kujua kama upo au haupo basi!!!!
Wee ongeza 28 za kutosha hapo walau mpaka wa 6 hivi[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom