HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Unafika mwaka wa 5 upande unasikia uhakiki wa watumishi hewa utalia. Watu wanakaa hadi miaka 8
[emoji1787][emoji1787][emoji1787], daaah...kweli lazima ulie tuu...hakuna namna utaimba wimbo tuu hata kama upo nchi ya ugenini.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mkuuu hali ni tete aisee....nimeishangaa sanaa serikali si ingesema mapema tuu kwamba nafasi kwa kila mkoa zipo kadhaa ili mtu ujue kwa nafasi hizi, nikitoa kada wa sisiem, wale uncle kanituma, unajua hapa nafasi yangu haipo. Wala haujisumbui kupoteza hela ya ku-print forms.
 
Kutoka TGS D laki 7.5 unatakiwa kufanya kazi miaka 5 ndipo upande daraja kwenda TGS E laki 9.9
Hali ni mbaya halmashauri na wizarani
nina mwnangu yuko hpo treasury ,mshahara alinambia haufiki hata 1M,ila sasa yuko njema ana subaru,ardhi na mjengo. mianya ni mingi safari na semina posho niyakufa mtu mkuu. by the way usifananiahe ukoko wa halmashauri na wizara. vp afsa upo halmashauri ya busisi nini
 
Acha tu Kaka Maisha yenyew ndy haya Gharama za Usahili mpk ndg akushike Mkono na ushindani ilivyo Mgumu kikando ikiwa Mingi wanaweza kukutenga Imagine Kwa Mwaka umeenda interview 6 na Kila Interview sio Chini ya 200k Kwa Sisi tunaokaa Mbali na Dodoma. Ni lzm kukubali tu kudeal na Course uliyosomea Neema inaweza kuwepo
Inaumiza sana aisee...
 
Jamani kazi ni hizi hizi na mishahara haijawahi kutosha duniani kote hata kama utalipwa Mil5 sasa hivi..

Niko kwenye Wakala moja ya Serikali ingawaje hapa sisi kazi zetu ni za mikataba na tunarenew kila baada ya miaka miwili..

Mshahara na marupurupu ya hapa na pale si haba ingawaje mara ya kwanza ukipewa ile contract inaona kazi si ndo hii, lakini unapoanza kulipwa ule mshahara utaona kuwa hauwezi kutosha kwa maisha ya sasa halafu mbaya zaidi kwa Familia zetu hizi Extended family na ikiwa ww ndo atleast umetoboa huwezi kuishi kwa mshahara..

Kikubwa ndugu zangu Mungu akijaalia mpatapo mrija wa Asali pia ni muhimu kuzingatia namna ya kujiongezea kipato kwa sababu pia maandiko yanasema "Binadamu hatoishi kwa mkate tu"..

Naamin Mwenyezi Mungu kampangia kila mtu wapi atapata mrija wake wa asali, haiwezekani wote tukaenda sehemu moja hivyo basi hata kama utapangiwa Halmashauri kamwe usije ukakosa kwenda kuna watu wanafanya mambo makubwa na huwezi kudhani anafanya kazi halmashauri.
Ni kweli kabisa mkuu, nakushukuru sanaa kwa nasaha zako hapa jukwaani. Kiukweli hapa ni kama tunachangamsha kijiwe ili vijana tusiwe wanyonge kusubiria mkeka wa placement maana hapa hadi mikeka mingine ije nahisi ni mpaka wiki ijayo kesho sidhani...Tunaondoana stress na kutiana nguvu kiaina...[emoji3][emoji3]
 
Nasisitiza tena ukipata chaka ww zama usiangalie habari ya mshahara! Mshahara hujawahi kutosha duniani..

Kuna jamaa hapa tulikuwa nae mshahara aliokuwa analipwa hapa kwa level ya diploma ndo akaenda kulipwa huko Manispaa kwa level ya degree TGS E.

Alikuwa anasita sita kwenda kule na bado hapa tunafanya kazi kwa mkataba! Tukamwambia nenda, saiv anatukumbua kwa namna anavyoogelea kwenye dimbwi la asali ingawaje ni local government..
Duuu, kongole kwake...
 
Back
Top Bottom