Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Nawaambia ndg zangu,tatizo la waislam kwa sasa tunapenda ndogo twapenda saana ndogo mpk shetan anatukwepa huko jehanam-Ustaadhi.
Ndogo ndo Nini?....Kama Wewe unapenda hayo Mambo...unwajumuishaje wote..
 
YESU ALIKWENDA KANISANI MARA NGAPI.
Ninyi endeleeni tu kutokwenda kanisani kwa amani, hakuna anayewahukumu, japokuwa naamini hapa yenyewe nafsi zenu zinawasuta ndiyo maana mnajifanya kutafuta justification tu ya matendo yenu hamna lolote..!
 
Kuokoka ni kitendo gani..?
KUOKOKA ni kule kujijua kuwa wewe ni mwenye dhambi kisha ukachukua hatua ya kumwamini Yesu ya kuwa alikufa msalabani na kufufuka siku ya tatu kwa ajili ya dhambi zako. Unapomwamini Yesu dhambi zako zote zinafutwa na unaaanza maisha mapya na Bwana, maisha ya ushindi!

Huku ndiko kuzaliwa mara ya pili ambako hatima yake ni uzima wa milele.

Karibu kwa YESU mkuu, kuna raha ambayo akili ya mwanadamu haiwezi kuielelezea.

YESU NI BWANA NA MWOKOZI
 
Sijui mm natatizo gani yaani nikiacha kwenda tu kanisani hata wiki moja nahesabu maumivu, lazima nipate shida kama sio hasara kwenye biashara lazima litokee jambo litakalo niumiza au kunirudisha nyuma
So nimeshatengeneza uoga ikifika jpili saa 11 asubuh hatakama naumwa ,niko njiani nawahi misa ya kwanza ndio nakuwa na amani ya moyo
 
Maana yake mlipata mil 50 lakini alikosea angesubiri mpaka apate mgao wake ndo angeenda kutoa zaka...hapo alikosea. Lakini hii isikufanye kuacha kwenda kanisani...Mungu amekupa vingi vinavyozidi hiyo Mil5
Yes tulichomlaumu yeye ni kutosubiri mgao wake halafu miezi km minne Mchungaji akata kufanya uzinifu na sister hadi wa leo hajawahi kanyaga kanisani hapo
 
S
Dahhhh.....
Ila kwetu michango imezidi mnoooo.....
1. Zaka
2.Sadaka
3. Mavuno
4. Utoto mtakatifu
5. Ujenzi wa nyumba ya Paroko
6. Ukarabati wa kanisa
7. Mfuko wa parokia
8. Wageni wa kanisa
9. Viti vya jumuiya
Hii imechangia sana kwa upande wangu hata jumuia siendi
 
Dahhhh.....
Ila kwetu michango imezidi mnoooo.....
1. Zaka
2.Sadaka
3. Mavuno
4. Utoto mtakatifu
5. Ujenzi wa nyumba ya Paroko
6. Ukarabati wa kanisa
7. Mfuko wa parokia
8. Wageni wa kanisa
9. Viti vya jumuiya
Saidia Jimbo
Kuchangia radio tumaini
Bado radio maria
 
Huwa kuna sababu mbalimbali ambazo humfanya mtu kutokupenda kuhudhuria ibada siku ya Jumamosi au Jumapili (kutokana na dhehebu).

Mimi sababu ilinifanya nisiwe nahudhuria kanisani ni pale mchungaji alipokuwa anahubiri kuhusu sadaka na matoleo tu kwa ibada tatu mfululizo.

Nini sababu yako?
Mh!
 
Back
Top Bottom