Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Author

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
1,709
8,007
Huwa kuna sababu mbalimbali ambazo humfanya mtu kutokupenda kuhudhuria ibada siku ya Jumamosi au Jumapili (kutokana na dhehebu).

Mimi sababu ilinifanya nisiwe nahudhuria kanisani ni pale mchungaji alipokuwa anahubiri kuhusu sadaka na matoleo tu kwa ibada tatu mfululizo.

Nini sababu yako?
 
Wachungaji matapeli kama Ngwajiboi..wachungaji kutafuna kondoo zao hadharani..mahubiri yasiyo na wokovu wala kukemea dhambi wao ni kupanda na kuvuna..wachungaji wasaka pesa..michango makanisani iliyokithiri we uliona wapi pipi kununuliwa kwa milioni kama sio kuongezeana umaskini.

Viongozi wa dini kutokemea na kushirikiana na wanasiasa wanafiki na wauaji.

Ila mahubiri ya mchungaji mgogo yananivutia sana hope nikianza kusali ntaaza kwenye kanisa analohubiria.

#MaendeleoHayanaChama
 
Carleen Ungekuwa muumini wa kanisa la Gwajiboy ungeendelea kwenda kanisani.. kwa sasa akiwa ni mchungaji/mwanasiasa. Ukijumuisha na swala la wazi lililotokea Kawe linalovunja amri ya 'Usiibe' na 'Usiseme uongo'....Kuna msemo unasema 'hauwezi kuwa mwanasiasa bila kusema uongo'
 
Ibada inafanyika kokote penye utulivu... sadaka iliyo kamili ni ile unayo itoa kwa moyo...ata ukimtumia mdogo wako pocket money shule kwa moyo basi ni sadaka sio lazima kujengea mapadri ma castle while kwenu mnakula ugali na chumvi uo kingreza inaitwa

Burden
 
Ibada inafanyika kokote penye utulivu... sadaka iliyo kamili ni ile unayo itoa kwa moyo...ata ukimtumia mdogo wako pocket money shule kwa moyo basi ni sadaka sio lazima kujengea mapadri ma castle while kwenu mnakula ugali na chumvi uo kingreza inaitwa

Burden

Ni kweli kabisa, “asiyewajali wa nyumbani mwake ni mbaya kuliko asiyeamini”... nimenukuu maandiko.
 
Back
Top Bottom