Kuna Dini na Taasis za kidini.
Dini ni mfumo wa maisha.
Taasisi za kidini ni taasisi zenye taratibu zake kwa mujibu wa sheria.
Taratibu za taasisi wakati mwingine sio taratibu za kidini... Mfano matoleo walitoa mara moja hasa wakati wa mavuno kwa mujibu wa biblia..
Na matoleo unapaswa kuleta pale unapokuwa umepata..kila mtu kwa namna anayoona amewiwa.
Mfanyakazi anafanya kazi mpaka mwisho wa mwezi unamdai sadaka Ibada ya Jama5 jioni, Alhamis jioni, Ijumaa jumamosi na jumapili... Yaani kila akija kwa ibada yoyote alipe sadaka.. as if anakuja kununua Uhusiano na Mungu!
Worst enough akiwa hana uwezo hawi kipaumbele.. wale wanaoleta fedha nyingi ndio wanakuwa wapendwa na wanapata all the attention.. maombi nk. Maana yake uzima na wokovu unauzwa sasa!
Tatu Mungu Hakuwa Mjinga kupanga watu waende ibadani mara moja kwa wiki.. ili mpate muda wa Mchungaji kuchunga na Waumini kupractice walichojifunza. Sasa kama unashinda kanisani Jumatatu mpaka Jumapili ..asubuhi mpaka jioni hao watu wanafanya kazi siku sita zipi!? Na upendo, uvumilivu, kuwajali wengine wanawajali saangapi ikiwa muda wote wako kanisani!?
Watu wamehijack a beautiful thing for personal benefits.. Na hawa ninaamini Mungu Atashughulika nao.
Sent from my Infinix X650 using
JamiiForums mobile app