Kwanini Tundu Lissu aliitwa ‘Chief Whip‘ Opposition Leader ndani na nje ya Nchi?

Bush Dokta

JF-Expert Member
Apr 11, 2023
12,152
20,321
Wakuu tukirudi nyuma kidogo kwenye siasa za Bongo hapo nyuma kulikuwa na siasa za Weka chuma niweke Ugoko.

Jambo moja ninalokumbuka huyu bwana anayeitwa Tundu Lissu alitambulika na kupata umaarufu na hatimaye Vyombo vya habari vya ndani na nje ya Nchi vilimtambua kama Chief Whip Opposition leader.

Kwa tafsiri isiyo rasmi Whip ni Mjeledi. Mjeledi ni rimba ndefu laini mithiri ya mpira yakni kitu kinachoweza kupinda na kuvutika. Inasemekana mtu akipigwa viboko kwa rimba hii maumivu yake ni balaa.

Hata website ya serikali yaani ya Bunge la Tanzania lilimtambulisha hivyo.
 
Screenshot_20230513-223054_Chrome.jpg
 
Ndugu mtoa mada point yako ni nini hapo?

Mnadhimu mkuu wa upinzani ni cheo tu katika vyeo vya bunge, kama ambavyo pia kuna mnadhimu mkuu wa serikali humo bungeni ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia sera uratibu na bunge.

Mnadhimu mkuu wa upinzani anateuliwa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, na kwa cheo hicho anakuwa pia mjumbe wa kamati ya uongozi ya bunge inayoongozwa na spika.

That's why alikua akiishi kwenye nyumba za viongozi kule area D kwa sababu ya hicho cheo.
Yeye sio mnadhimu wa kwanza na hatakua wa mwisho ni utaratibu tu wa kibunge.

So huo u-chief whip hakupewa na vyombo vya habari kama unavyodhani.
 
Okay asante. Ndio maana ya GT
 
Lakini si angeweza kuitwa Chief Opposition leader? Hicho kivumishi cha Whip😅😅
 
Akiitwa chief opposition leader maana yake anakua kiongozi mkuu wa upinzani ambaye tayari yupo, sio yeye. Huyu chief whip ni kama mtunza nidhamu ya wabunge wa upinzani. Yupo chini ya kiongozi wa upinzani bungeni. Kwa upande wa serikali, kiongozi mkuu wa serikali bungeni ni waziri mkuu na chini yake ndo kuna mnadhimu wa serikali.
 
Unachanganya title zake mbili tofauti

‘Whipping system’ ni siasa za bungeni (specifically bunge la uingereza) kwenye utaratibu wa uhuru wa kuchangia na kupiga kura bungeni wanaopewa wabunge na vyama vyao.

Mfano kuna sera za kitaifa ambazo mmbunge wa chama fulani uruhusiwi kuwa na mtazamo tofauti na serikali (mawaziri) na kuna sera ambazo mmbunge una uhuru wa kuchangia unavyodhani kwa maslahi ya jimbo lako au mtazamo wako kwenye moral issues.

Vivo ivyo kwenye kupiga kura kuna maelekezo ya kupiga kura ya mambo fulani kwa mlengo wa chama au serikali; na kuna mambo ni bipartisan unaweza piga kura unavyodhani sahihi.

Kwenye hizo kura za mlengo wa kichama au hoja za kichama ndio ‘whip’ inapotumika. Whips ni wabunge ambao chama imewateua jukumu lao ni kutoa taarifa kwa wenzao agenda na misimamo ya chama ambayo lazima wafuate kwenye kuchangia au kupiga kura.

Whips pia wanajukumu la kuhakikisha siku ya kupiga kura wanapata quorum inayotakiwa. Kwa ivyo wanajukumu la kuwapigia simu siku kadhaa kuhakikisha wabunge wao wote popote walipo na kuwataarifu kuna kura sio ya kukosa bungeni ili kupitisha agenda ya serikali na upande wa pili ni ivyo ivyo kwenye kujaribu kuzuia.

Chief whip ndio kiongozi wa hizo shughuli bungeni; mmbunge anaekosa kuhudhuria hivyo vikao muhimu bila ya taratibu zilizopo za kufanya ivyo (hiyo ni story nyingine tena) anapewa whip (onyo) zikizidi wanaweza kukuzuia kuhudhuria vikao vya bunge kama mwanachama wao; ukikaidi zaidi unafukuzwa chama.

Opposition leader ni kwa sababu Lissu pia ni kiongozi wa taasisi ya CDM makamu mwenyekiti. Kwa ivyo ‘Chief whip’ na ‘opposition leader’ ni nafasi zake mbili tofauti.

Kibongo huko kwenye kuitana whips ni kupenda titles tu, ila siasa zetu hazina mfumo huo. Jenista Mhagama ni chief Whip wa CCM miaka mingi lakini atumii hiyo title.
 
Akiitwa chief opposition leader maana yake anakua kiongozi mkuu wa upinzani ambaye tayari yupo, sio yeye. Huyu chief whip ni kama mtunza nidhamu ya wabunge wa upinzani. Yupo chini ya kiongozi wa upinzani bungeni. Kwa upande wa serikali, kiongozi mkuu wa serikali bungeni ni waziri mkuu na chini yake ndo kuna mnadhimu wa serikali.
Na kiongozi rasmi wa upinzani kwa bungeni ni mwenyekiti wa chama kama na yeye ni mmbunge.
 
Akiitwa chief opposition leader maana yake anakua kiongozi mkuu wa upinzani ambaye tayari yupo, sio yeye. Huyu chief whip ni kama mtunza nidhamu ya wabunge wa upinzani. Yupo chini ya kiongozi wa upinzani bungeni. Kwa upande wa serikali, kiongozi mkuu wa serikali bungeni ni waziri mkuu na chini yake ndo kuna mnadhimu wa serikali.
Wewe ndio angalau umehiti kwenye Point.👏👏
 
Unachanganya title zake mbili tofauti

‘Whipping system’ ni siasa za bungeni (specifically bunge la uingereza) kwenye utaratibu wa uhuru wa kuchangia na kupiga bungeni wanaopewa wabunge na vyama vyao.

Mfano kuna sera za kitaifa ambazo mmbunge wa chama fulani uruhusiwi kuwa na mtazamo tofauti na serikali (mawaziri) na kuna sera ambazo mmbunge una uhuru wa kuchangia unavyodhani kwa maslahi ya jimbo lako au mtazamo wako kwenye moral issues.

Vivo ivyo kwenye kupiga kura kuna maelekezo ya kupiga kura ya mambo fulani kwa mlengo wa chama au serikali; na kuna mambo ni bipartisan unaweza piga kura unavyodhani sahihi.

Kwenye hizo kura za mlengo wa kichama au hoja za kichama ndio ‘whip’ inapotumika. Whips ni wabunge ambao chama imewateua jukumu lao ni kutoa taarifa kwa wenzao agenda na misimamo ya chama ambayo lazima wafuate kwenye kuchangia au kupiga kura.

Whips pia wanajukumu la kuhakikisha siku ya kupiga kura wanapata quorum inayotakiwa. Kwa ivyo wanajukumu la kuwapigia simu siku kadhaa kuhakikisha wabunge wao wote popote walipo na kuwataarifu kuna kura sio ya kukosa bungeni ili kupitisha agenda ya serikali na upande wa pili ni ivyo ivyo kwenye kujaribu kuzuia.

Chief whip ndio kiongozi wa hizo shughuli bungeni; mmbunge anaekosa kuhudhuria hivyo vikao muhimu bila ya taratibu zilizopo za kufanya ivyo (hiyo ni story nyingine tena) anapewa whip (onyo) zikizidi wanaweza kukuzuia kuhudhuria vikao vya bunge kama mwanachama wao; ukikaidi zaidi unafukuzwa chama.

Opposition leader ni kwa sababu Lissu pia ni kiongozi wa taasisi ya CDM makamu mwenyekiti. Kwa ivyo ‘Chief whip’ na ‘opposition leader’ ni nafasi zake mbili tofauti.

Kibongo huko kwenye kuitana whips ni kupenda titles tu, ila siasa zetu hazina mfumo huo. Jenista Mhagama ni chief Whip wa CCM miaka mingi lakini atumii hiyo title.
Umetoa elimu ya kutosha bilashaka umefaidisha wengi kwenye jukwaa hili
 
Ndugu mtoa mada point yako ni nini hapo?

Mnadhimu mkuu wa upinzani ni cheo tu katika vyeo vya bunge, kama ambavyo pia kuna mnadhimu mkuu wa serikali humo bungeni ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia sera uratibu na bunge.

Mnadhimu mkuu wa upinzani anateuliwa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, na kwa cheo hicho anakuwa pia mjumbe wa kamati ya uongozi ya bunge inayoongozwa na spika.

That's why alikua akiishi kwenye nyumba za viongozi kule area D kwa sababu ya hicho cheo.
Yeye sio mnadhimu wa kwanza na hatakua wa mwisho ni utaratibu tu wa kibunge.

So huo u-chief whip hakupewa na vyombo vya habari kama unavyodhani.
Msome Mayor Quimby ametoa elimu murua.
 
Back
Top Bottom