Kwanini Tanzania hamna migahawa ya McDonalds?

Kwanini Tanzania hamna migahawa ya McDonalds?

Huwa najiuliza kwanini hamna migahawa ya McDonalds maana kama mtaji mbona kuna fast food restaurants nyingine kibao zilizoanzishwa kama Franchise za nje, hasa Dar es salaam... kuna KFC kibao, Subway, Pizza hut akina Mb na nyingine nyingi

Hivi sabab ya kutokuwa na McDonalds ni ipi? nauliza nataka fahamu
Arusha ulikuwepi kipindi fulani then ukabadilishwa jina, kwa Dar sijui ila Aruaha uliwahi kuwepo
 
Waliwai kuja miaka ya 2000 mwanzaoni, marketing Survey yao iliwaambia kuwa Chips Vumbi ni cheap kuliko Chips zao hivyo awatopata faida- so Wakaamua achana na Deal ya kufunguwa hapa Tanzania! Steers walijaribu na Nandos Wakafirisika na kufunga Virago . Labda sasa kutokana na population ya vijana ni kubwa wanaweza kuja tena! Iwapo mtu anataka funguwa Mac Donald Restaurant anatakiwa awe na kati ya 500M to 1B.
Arusha ulikuwepo, baadae wakabadilisha jina wakaandika Mc Mood's kama sikosei na wale nal naona wameshindwa tena kwa sasa ni Duka la Nguo au nini vile
 
Hayo mavyakula hayana swagger, unapiga zako makange au changamoto swaafi kabisa
 
Arusha ulikuwepo, baadae wakabadilisha jina wakaandika Mc Mood's kama sikosei na wale nal naona wameshindwa tena kwa sasa ni Duka la Nguo au nini vile
We jamaa umeingia chaka vibaya mno....ile ya Arusha maeneo ya stendi ya mabasi inaitwa MACFOOD na sio MAC MOOD, nimekula sana hayo maeneo kama KEFLA AZIZ na sehem nyinginezo...hakuna Macdonald iliyowahi kuwepo Arusha labd kama alicopy jina tu la hao jamaa!!
 
Nando’s Pia hawapo bongo [emoji848][emoji848]

Kwanini? [emoji2369][emoji2369]

Nando’s kuku wao na ile pili-pili yao tamu sana jamani!
Walikuwepo zamani, sasa hivi Nandos wapo Angola, Botswana na South Africa.
 
Afrika nzima nchi zenye McDonald's hazifiki 5
 
Mwaka 2015 nilikuwa Uingereza nilikuwa nasafiri kutoka Cambridge kwenda Coventry nikiwa nimepewa lift na kijana mmoja wa Kiingereza, basi tulipita sehemu tukaona kibanda cha McDonalds, nikamwambia yule jamaa kuwa kwetu Tanzania hawa jamaa McDonalds hawapo kabisa! Jamaa alifurahi huku aamini kama nasema kweli, nikamuuliza kwanini amefurahi kusikia vile, akanijibu kuwa " aaah hawa jamaa wanaringa sana na kujidai wako kila mahali hadi kwenye mwezi, kumbe Tanzania hawako!
Kumbe na wazungu wenye roho za kwanini wapo?
 
Huwa najiuliza kwanini hamna migahawa ya McDonalds maana kama mtaji mbona kuna fast food restaurants nyingine kibao zilizoanzishwa kama Franchise za nje, hasa Dar es salaam... kuna KFC kibao, Subway, Pizza hut akina Mb na nyingine nyingi

Hivi sabab ya kutokuwa na McDonalds ni ipi? nauliza nataka fahamu
Tuko level za mihogo koko na chips za edo

Tusijikweze jaman.. tanzania ni nchi moja masikin sanaaaa. Yaan tunaruka sana step za maisha sabab ya utandawaz.. ila ki uhalisia.. ni nchi moja masikin na wamanchi wake wameridhika na umaskin huo kias cha kwamba hata wanasiasa wanaweza wafanyia chochote wananchi na wananchi wasifanye chochote
 
Lakini siyo mac tu kuna taco bell, denny's, etc hawapo Tanzania.

Tatizo kubwa ni watanzania wengi ( 96 percent) ni lower class, hawana uwezo wa kununua big Mac kwa tsh 25k.

Middle class nayo iko hoi toka alipoingia jiwe ilipungua kutoka 30% mpaka 2%
1. Hayo madude sio kila mtu anaona ya maana.

2. Watu wengi sana wanaweza clear bills za bia za 100k ila hajawahi kula hayo madude.
 
Waliwai kuja miaka ya 2000 mwanzaoni, marketing Survey yao iliwaambia kuwa Chips Vumbi ni cheap kuliko Chips zao hivyo awatopata faida- so Wakaamua achana na Deal ya kufunguwa hapa Tanzania! Steers walijaribu na Nandos Wakafirisika na kufunga Virago . Labda sasa kutokana na population ya vijana ni kubwa wanaweza kuja tena! Iwapo mtu anataka funguwa Mac Donald Restaurant anatakiwa awe na kati ya 500M to 1B.
Nandos aliimba Mh temba kwny nampenda yeye2005
 
Kwanza wasiliana nao ujuwe vigezo halafu ujuwe ni nini cha kutafuta. Pesa za biashara hazitafutwi, zinakutafuta. Unafikiri kazi za mabenki ni nini?

Tena hao mchanganuo wa biashara wanakupa wao wenyewe, wewe unabadili kutokana na nchi yako tu. Ukiupeleka benki hunyimwi pesa. Dhamana anza kwa mwenyekiti wako, babu yako akikunyima kuweka dhamana nyumba zake na mashamba yake, akikuzinguwa nenda kwa diwani wako, akikuzinguwa kwa mbunge wako.

Nyie badala ya kuwapelekea wanasiasa wenu biashara kama hizi mnawapelekea kesi za kufumaniana tu.
Eti eeeh? Umenipa wazo
 
Niache Kula mihogo Na utumbo wa Kuku nikale ngano iliyojazwa spice?
 
Back
Top Bottom