Kontelo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 572
- 161
Ukiangalia hiyo video utaelewa kweli bongo tunapigwa. Kariakoo imekuwa ni sshemu ya upigaji kwa wachina tu. Protector ya 1$ eti ilinde simu na crackHonestly, kama kuna kitu wabongo wanapigwa basi ni screen protectors.
Hivi ni mara ngapi umeweka screen protector kwenye simu halafu ukaangusha na bado screen ikavunjika?
Hivi unadhani protector nzuri yenye uwezo wa kulinda simu yako itauzwa sh. 2000 au sh. 3,000?
Hivi unatambua kwamba kuna screen protectors zinafika mpaka $100?
Unadhani quality yake itakuwa sawa na hizo za 2000 au elfu tatu?
Eti protector imeandikwa 9H halafu inauzwa 2000. Hivi nyie mnaijua hardness level 9 nyinyi?
Hardness level 10 ni diamond, Sasa rudi hatua moja nyuma kwa ugumu. Halafu ndo uuziwe buku 2
Hell no.
Halafu Bongo mtu ananunua simu ya 2m ina kioo kizuri, gloss finish, akitoka hapo anaenda kuweka screen protector nyeupe kama vioo vya zile simu fulani... Ni ushamba au ni nini?
Hebu angalia hii video ya Mr. Whosetheboss. Kwa wanaomfatilia huyu jamaa huenda wameshawahi kuiona.