Screen Protector kwenye simu ni aina nyingine ya Upigaji

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,058
2,000
Hii Simu nilinunua mwezi wa 9 mwaka jana, mpaka inafika mwezi wa 12, nilikua nshaweka screen protector 3 (ya elfu 5, elfu 7 na elfu 10).

Ukisahau 100 mfukoni, au ukaichanganya na funguo, unakuta ishapasuka.

Nilikua najiuliza sana, inawezekanaje hii gorila glass iwe protected na plastic cover? Kuanzia mwezi wa 12 mwishoni niliachana na huo wizi wa kununua protector, na simu yangu sasa haina michubuko na inaonekana kama mpya, mwonekano wa kiwandani kabisa.

Wakuu, achaneni na hizi protector, ni aina nyingine ya wizi, CAG na au TBS wanapaswa kuchunguza. Hazina viwango na sidhani hata kama hata zinafikia hardess/kiwango cha gorilla glass 0.5. Kwanza hizi protector zinaharibu mwonekano wa simu.
 
racka98

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
970
1,000
Screen protector zililetwa kuzuia michubuko kwenye kioo cha simu kwasabab ukiipasua au ukiiscratch kuibadilisha ni bei rahisi kuliko kubadili kioo hali cha simu kikiwa scratched.

Zina umuhim wake kwa wasiotaka kuscratch kioo cha simu kwasababu utakiscratch tu siku moja. Ni swala la muda
 
thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,447
2,000
Gorilla 5 ni ngumu kupasuka kulinganisha na screen protectors.

Wenyewe wanadai kioo kinaweza kisivunjike ikiwa simu imeanguka kwa mita 1.2

Lakini gorilla 5 ni rahisi pia kupata michubuko midogo(micro scratch) ukiweka simu kwenye angle nzuri michubuko hiyo utaiona.

Hivyo, binafsi screen protector bado ni muhimu hasa tempered glass screen protector kuzuia scratches.
 
At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
3,593
2,000
Hii Simu nilinunua mwezi wa 9 mwaka jana, mpaka inafika mwezi wa 12, nilikua nshaweka screen protector 3 (ya elfu 5, elfu 7 na elfu 10).

Ukisahau 100 mfukoni, au ukaichanganya na funguo, unakuta ishapasuka.

Nilikua najiuliza sana, inawezekanaje hii gorila glass iwe protected na plastic cover??
Kuanzia mwezi wa 12 mwishoni niliachana na huo wizi wa kununua protector, na simu yangu sasa haina michubuko na inaonekana kama mpya, mwonekano wa kiwandani kabisa.

Wakuu, achaneni na hizi protector, ni aina nyingine ya wizi, CAG na au TBS wanapaswa kuchunguza. Hazina viwango na sidhani hata kama hata zinafikia hardess/kiwango cha gorilla glass 0.5. Kwanza hizi protector zinaharibu mwonekano wa simu.
Tangu ninunue ni mwaka sasa sijawahi weka hio protector.
Sema niliacha ile Karatasi inayokuja na simu kwa ajili ya kuzuia scratch.

Ni utunzaji tu.
 
mzee74

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
10,697
2,000
Hii Simu nilinunua mwezi wa 9 mwaka jana, mpaka inafika mwezi wa 12, nilikua nshaweka screen protector 3 (ya elfu 5, elfu 7 na elfu 10).

Ukisahau 100 mfukoni, au ukaichanganya na funguo, unakuta ishapasuka.

Nilikua najiuliza sana, inawezekanaje hii gorila glass iwe protected na plastic cover??
Kuanzia mwezi wa 12 mwishoni niliachana na huo wizi wa kununua protector, na simu yangu sasa haina michubuko na inaonekana kama mpya, mwonekano wa kiwandani kabisa.

Wakuu, achaneni na hizi protector, ni aina nyingine ya wizi, CAG na au TBS wanapaswa kuchunguza. Hazina viwango na sidhani hata kama hata zinafikia hardess/kiwango cha gorilla glass 0.5. Kwanza hizi protector zinaharibu mwonekano wa simu.
Protector ni wizi mtupu.Ni kutupilia mbali.Na kuna ile liquid protector ambayo inaharibu kabisa screeen na ni WIZI MTUPU
 
KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,058
2,000
Screen protector zililetwa kuzuia michubuko kwenye kioo cha simu kwasabab ukiipasua au ukiiscratch kuibadilisha ni bei rahisi kuliko kubadili kioo hali cha simu kikiwa scratched.

Zina umuhim wake kwa wasiotaka kuscratch kioo cha simu kwasababu utakiscratch tu siku moja. Ni swala la muda
Mfano Una gorilla 5, ukiweka hako ka karatasi ni value for money!?
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
25,000
2,000
Kinachopasua kioo ni vumbi, kama unaishi mazingira yasiyo na vumbi Hakuna haja ya Screen protector,

Gorilla glass ina Mohs scale ya 7, kitu kama Chuma hakiwezi kuscratch, ila vumbi lina Quartz ambayo inaweza kuscratch Gorilla Glass.

Unaweza kuangalia Video za JerryRigeverything YouTube huwa anaelezea sana karibia kila scratch test anayo fanya.
 
Wakipekee

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
416
1,000
Screen protector n ujambazi sio wizi tu coz mi sijazoea kuweka protector sasa kuna siku nikajichanganya kuweka kwa bahati mbaya kwa huku juu ikawa kama inaachia ikajaribu kuibana palepale ikapasuka aisee nilimaindi kichizi nikaitoa na kuitupa huu mwezi karibia wa kumi sina protector na simu yangu iko bomba vibaya mno
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
3,700
2,000
Nina Gorilla Glass 5 protector nina mwaka umeisha huu. Ila huwezi kuwa na lisimu la Tecno au Infinix ambazo zina plastic sijui imefunika LCD ukaacha kuweka protector. Screen za Tecno ukiizima inakuwa angavu na mwanga unauona ndani, ukiigusa inabonyea. Hizi lazima uweke protector
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom