Sbabu ni uwezo mdogo wa kiakili. Chanzo cha uwezo mdogo wa kiakili ndio bado hakijajulikana ila huenda imechangiwa na mambo mengi ikiwemo lishe mbovu, kutawaliwa muda mrefu, matumizi ya bidhaa zenye ubora duni zinazoharibu uwezo wa kiakili n.k.
Watu wachache wenye akili nzuri wakizungukwa na watu wengi wenye akili mbaya matokeo jumuishi ni kuwa wote wataenda sawa, akili mbaya. Kama tungeweza, tungeweka utaratibu kama wa "Genius Visa", kwamba tunaweza toa visa ya mtu kuingia na kukaa nchini kwa exemptions fulani fulani as long as huyo mtu ana akili ya kitofauti ambayo tunaweza kuitumia kutatu matatizo yetu hapa nchini.
Kuna matatizo ya kawaida kabisa ambayo shida yake sio bajeti ila ni akili bunifu ambayo huenda tukiwa honest tukubali kuwa hatuna. Matatizo ya upatikanaji wa maji safi kwenye mikoa yenye vyanzo vikubwa kama Mwanza, Geita na Kagera, matatizo ya foleni, matatizo ya upatikanaji wa huduma za umeme. Imagine mkoa muhimu kama Dar kuna maeneo maji yanatoka kwa wiki mara moja, huu mwaka 2026.
Si umeona tu hata ujenzi wa mabarabara inabidi tulete wachina maana watanzania wenzetu wakijenga baada ya miezi sita mashimo yanajaa.
Umeona pia nchi kama South Africa ambayo wazungu walibaki na wameshika maeneo mengi muhimu ya kiuchumi na kiutawala, leo South Africa imejengwa kama Ulaya. Nchi kama Zimbabwe au Uganda ambayo walifukuza wazungu, nadhani wote tunajua zilivyo kwa maana ya hali ya maisha na upatikanaji wa huduma za kijamii.
Naomba kuwasilisha.