Pole sana Mwanamtaa/kijiji, nyongo yangu ilikuwa imepanda ila baada ya kusoma kipande hicho imetelemka kidogo. Ugomvi wangu ni mtu kama Nape anayesema serikali mbili ziendelee. Kwa msimamo wako naweza kukubaliana nao ila Wazenj hawataki na kama hawataki basi solution ni serikali tatu........
Mimi napinga serikali tatu - naamini kama kweli watu wanataka tuimarishe Muungano basi ni kuunda nchi moja, serikali moja mifumo mbalimbali au utengano! Kwani nani kasema ni lazima tuungane? Hatutakuwa nchi ya kwanza duniani kuvunjika na watu kuendelea kuishi pamoja na ujirani mwema.
MM,
Tusidanganyane, tumebakiwa na option mbili tu, Kuwa na serikali moja au tatu. Serikali mbili haiwezekani tena. Hata ccm leo wakilazimisha itachukua miaka michache tutarudi kwenye tope la matatizo ya kero za muungano.
Na kwa kuwa Wazanzibari hawataki kuua utaifa wao kama sisi watanganyika tulivyoua tanganyika yetu, basi kama Yereck wa Nyerere anavyosema serikali tatu haikwepiki. Naishukuru Chadema kuliona hili mapema na kuiweka ktk sera yake.
Tatu, ktk dunia ya Leo kama ni kweli kwamba serikali tatu itavunja muungano na kama muungano utavunjika kweli miaka kadhaa ijayo, kwani kuna tatizo gani? watz hawatakuwa wakwanza kuvunja muugano wao, duniani kote mifano iko mingi ya miungano iliyovunjika, and by the way ndivyo tulivyokuwa kabla ya 1964.
Nne, Muungano uliopo hauwatendei haki watanganyika. Ni muugano wa chako ni chako, ila changu ni chetu sote. Yaani mimi siwezi kuwa waziri Zanzibar, ila mzanzibari anaweza kuwa waziri Tanganyika kupitia Serikali ya MUUNGANO. Leo hii mzanzibar ni waziri wa Afya wakati afya haiko ktk muungano. Zanzibar kuna waziri wa afya. Waziri wa afya wa Muungano kiuhalisia ni waziri wa afya wa Tanganyika. kwa hiyo waziri wa afya kutoka zanzibar anaongoza wizara ya Serikal ya Tanganyika iliyofutwa kiaina huko nyuma. SASA kwa nini iwe hivyo?
Tano, Ni jambo la bahati nzuri sana kwamba, wanaoongoza kuupinga muungani ni wazanzibar, na naomba tuwape haki yao. Wazanzibar wamediriki kusema wao hawataki kuwa koloni la Tanganyika. sisi tuna hofu nini?
Mwanasheria mkuu wa zbar kasema kero kubwa ya muungano ni kutokuwepo kwa serikali ya Tanganyika. We should not fear the unknown, we should face the challenges of 3 governments, na kama muungano utavunjika, tutakuwa kama tulivyokuwa kabla ya mwaka 1964, si vita.
Wazo zuri ila Wazanzibar hawahitaji kuelemishwa kuhusu muungano! tayari wanajitambua wanajua ni kitu gani wanataka, Zanzibar yao.Mi nadhani huu mjadala wa Muungano uahirishwe kwa miaka 20, na watu wa elimishwe, historia ya kweli iandikwe na ifundishwe mashulei Kizazi kijacho kiamue muungano uweje
Anayetaka kuungana na Zanzibar nani? .... tulikuwa tunakuja na passports huko, mkasema haina haja. Nyie ndo mmejazana huku. Msipende kuhalalisha mambo ambayo hayapo.Hivi wadanganyika hakuna nchi nyengine ya kuungana nayo lazima iwe zanzbr?
My perceptions ni kuwa Mwanakijiji ni mmoja kati ya watu ambao wanapenda muungano uvunjike ndio maana kaja na hoja ya serikali moja. Kwa mazingira ya sasa serikali moja haiwezekani kwani itapoteza Identity ya Zanzibar. Serikali mbili hatuzitaki kwa kuwa zinalalamikiwa sana na wazanzibari na pia zimepoteza Identity ya Tanganyika. Suluhisho ni serikali tatu maana imefikia hadi watu wa CCM wanaikana historia na kusema tisa disemba ni uhuru wa Tanzania Bara, hatuwashangai ni malimbukeni wa historia. Serikali mbili zimekumbatia sana ufisadi na pia wamekuwa waki adjust mambo ya muungano kwa faida zao binafsi. Pia suala la Rais wa Zanzibar kuchaguliwa Dodoma halitufurahishi watanganyika wengi kwa minajili kuwa Amiri jeshi mkuu wa nchi ya Zanzibar atachaguliwaje Tanganyika!?
Serikali tatu ndio suluhisho, tusiwaza katika misingi ya Rais wa Muungano hatakuwa na nguvu kwani tutengeneza taasisi na sio kuangalia maslahi binafsi ya wanaCCM kuwa ndani ya serikali tatu itakuwa vigumu sana kwao ku COVER ufisadi na wizi mkubwa waliolifanyia taifa kwa miaka 50 hivyo wanajua serikali mbili zitaendelea kuweka mambo kama ya EPA na Richmond chini ya kapeti. Ikija serikali tatu rais wa Tanganyika anaweza kufunua kapeti na kukuta uvundo na kufuatilia huo uvundo na kuwasweka Limande wanCCM waliohusika, ndio maana wanaCCM hawataki kusikia serikali tatu
Maswali yangu ni haya: je kwa nini zanzibar wao wawe na rais mwenye mamlaka kamili na sisi tusiwe na rais wetu mwenye mamlaka na Tanganyika? Je kwa nini kama tumeungana hajachaguliwa mtu toka bara kuongoza serikali ya zanzibar kama kweli tumeungana? Nashauri tuwe na uhuru zaidi wa kupambanua masuala haya. Sioni haja ya kuubeba muungano ambao hauko sawa!Aprili 30, 1992 aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais John Samwel Malecela alitoa hotuba ndefu Bungeni ambapo alipinga hoja ya serikali tatu. Kwanza alipinga kwa sababu tume ya Nyalali ilipata asilimia 49 tu ya watu 36299 waliotoa maoni walitaka serikali tatu. Kwamba watu karibu 17,000 ndio walitaka serikali tatu na kwa hilo tu tume ikapendekeza serikali tatu. Hata sasa suala la serikali tatu hatujaambiwa ni watu wangapi wanataka hilo kwenye tume ya Warioba hadi Tume iliingize kwenye rasimu ya Katiba. Na idadi hiyo inaendana vipi na wale wengine waliotaka mifumo mingine ya serikali.
Malecela alisema kwa uthabiti hivi:
Nyerere akielezea hili kwenye kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (UWHT) anasema hivi:
Nyerere aliona - na mimi nakubaliana naye - suala la kudai Tanganyika wakati ule kama ilivyo leo ni suala la tamaa ya uongozi na matokeo yatakuwa ni yale yale.
Nyerere aliona kuwa watu wa Tanzania wanachotaka ni kuwadhibiti viongozi wao. Yeye aliona kwa usahihi kabisa kuwa kuleta Tanganyika haitatatua tatizo la viongozi wahalifu kwani sasa utakuwa na viongozi wabovu kwenye Muungano na wengine kwenye Tanganyika na Zanzibar. Alisema suala basi ni kuweka utaratibu wa kuwawajibisha viongozi sawasawa.
Nyerere akaelezea vizuri kwanini wakati wa Muungano hatukwenda kwenye serikali moja au kwenda serikali tatu. Alisema hivi:
Ni vizuri kuangalia hizo namba leo hii; Zanzibar ina watu kama milioni 1.3 na Bara kuna zaidi ya watu milioni 45. Hivyo serikali tatu kwa mantiki ya Nyerere bado Tanganyika itabeba mzigo mkubwa zaidi - kuwa na serikail ya kuhudumia watu milioni 45 na pia kuchangia mchango mkubwa kwa serikali ya watu milioni 46.3.
Nyerere alikutana na viongozi wa chama na wabunge wa CCM na kuwashawishi kuipinga hoja ya serikali tatu na serikali nayo. Lakini alipoondoka kwenye Asia akiwa kwenye ziara ya Nchi za Kusini (alikuwa Mwenyekiti) huku nyuma serikali na viongozi wakashindwa kupinga kwa hoja maridhawa kabisa serikali tatu (kama tunavyoona sasa). Nyerere aliandika kwa ukali na uwazi hili tena kwa mshangao. Alisema:
Nyerere alifikia hitimisho ambalo hata leo tunaliona. Watu wanataka serikali ya Tanganyika kwa sababu wamechoka na Wazanzibari. Nyerere anasema hivi:
Muundo wa Muungano unabadilika na si lazima uwe serikali tatu
Mimi siamini katika serikali tatu kwa kiasi kikubwa kwa sababu zile zile za Nyerere. Lakini pia ninaamini kuwa wananchi ndio wana haki ya kuamua mfumo wa Muungano na hata uwepo wa Muungano wenyewe. Sasa hivi watu wanajadili serikali tatu kwa sababu wamekatazwa kujadili kuuvunja Muungano! Watu wamekubali kuwa ni lazima tuungane hivyo tutafute namna ya MUungano. Mimi naamini wananchi ndio wanapaswa kuamua kwanza kama Muungano uwepo na wakishaamua hivyo uwe wa namna gani.
Nyerere anasema hivi:
Na Hapa chini ndio msimamo wangu vile vile: Kwanini tunalazimishwa kujadili serikali tatu. Kwanini tumesalimu amri na kufikiria serikali tatu? Kwanini CCM wameamua tujadili serikali tatu na sisi tunajadili serikali tatu. Hivi kweli watu wanafikiria hili wazo la serikali tatu limetokana na wananchi kwenye maoni ya tume ya Warioba au ni carryover ya mjadala wa 1992?
Nyerere anasema:
Na maneno haya ya Nyerere yasikike kwenye masikio yaliyoziba ya watawala wetu walioshindwa!
Serikali tatu haitotatua matatizo ya Muungano itayaongeza tu. Tunaopinga serikali tatu hatupingi kwa sababu ya gharama tu - hili ni jambo dogo zaidi lakini tunapinga kwa sababu ya mantiki nzima ya kuwa na serikali tatu na nchi mbili! lakini wenzetu wanataka tuwe na nchi mbili na serikali tatu!
Mimi napinga serikali tatu - naamini kama kweli watu wanataka tuimarishe Muungano basi ni kuunda nchi moja, serikali moja mifumo mbalimbali au utengano! Kwani nani kasema ni lazima tuungane? Hatutakuwa nchi ya kwanza duniani kuvunjika na watu kuendelea kuishi pamoja na ujirani mwema.
Aprili 30, 1992 aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais John Samwel Malecela alitoa hotuba ndefu Bungeni ambapo alipinga hoja ya serikali tatu. Kwanza alipinga kwa sababu tume ya Nyalali ilipata asilimia 49 tu ya watu 36299 waliotoa maoni walitaka serikali tatu. Kwamba watu karibu 17,000 ndio walitaka serikali tatu na kwa hilo tu tume ikapendekeza serikali tatu. Hata sasa suala la serikali tatu hatujaambiwa ni watu wangapi wanataka hilo kwenye tume ya Warioba hadi Tume iliingize kwenye rasimu ya Katiba. Na idadi hiyo inaendana vipi na wale wengine waliotaka mifumo mingine ya serikali.
Malecela alisema kwa uthabiti hivi:
Nyerere akielezea hili kwenye kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (UWHT) anasema hivi:
Nyerere aliona - na mimi nakubaliana naye - suala la kudai Tanganyika wakati ule kama ilivyo leo ni suala la tamaa ya uongozi na matokeo yatakuwa ni yale yale.
Nyerere aliona kuwa watu wa Tanzania wanachotaka ni kuwadhibiti viongozi wao. Yeye aliona kwa usahihi kabisa kuwa kuleta Tanganyika haitatatua tatizo la viongozi wahalifu kwani sasa utakuwa na viongozi wabovu kwenye Muungano na wengine kwenye Tanganyika na Zanzibar. Alisema suala basi ni kuweka utaratibu wa kuwawajibisha viongozi sawasawa.
Nyerere akaelezea vizuri kwanini wakati wa Muungano hatukwenda kwenye serikali moja au kwenda serikali tatu. Alisema hivi:
Ni vizuri kuangalia hizo namba leo hii; Zanzibar ina watu kama milioni 1.3 na Bara kuna zaidi ya watu milioni 45. Hivyo serikali tatu kwa mantiki ya Nyerere bado Tanganyika itabeba mzigo mkubwa zaidi - kuwa na serikail ya kuhudumia watu milioni 45 na pia kuchangia mchango mkubwa kwa serikali ya watu milioni 46.3.
Nyerere alikutana na viongozi wa chama na wabunge wa CCM na kuwashawishi kuipinga hoja ya serikali tatu na serikali nayo. Lakini alipoondoka kwenye Asia akiwa kwenye ziara ya Nchi za Kusini (alikuwa Mwenyekiti) huku nyuma serikali na viongozi wakashindwa kupinga kwa hoja maridhawa kabisa serikali tatu (kama tunavyoona sasa). Nyerere aliandika kwa ukali na uwazi hili tena kwa mshangao. Alisema:
Nyerere alifikia hitimisho ambalo hata leo tunaliona. Watu wanataka serikali ya Tanganyika kwa sababu wamechoka na Wazanzibari. Nyerere anasema hivi:
Muundo wa Muungano unabadilika na si lazima uwe serikali tatu
Mimi siamini katika serikali tatu kwa kiasi kikubwa kwa sababu zile zile za Nyerere. Lakini pia ninaamini kuwa wananchi ndio wana haki ya kuamua mfumo wa Muungano na hata uwepo wa Muungano wenyewe. Sasa hivi watu wanajadili serikali tatu kwa sababu wamekatazwa kujadili kuuvunja Muungano! Watu wamekubali kuwa ni lazima tuungane hivyo tutafute namna ya MUungano. Mimi naamini wananchi ndio wanapaswa kuamua kwanza kama Muungano uwepo na wakishaamua hivyo uwe wa namna gani.
Nyerere anasema hivi:
Na Hapa chini ndio msimamo wangu vile vile: Kwanini tunalazimishwa kujadili serikali tatu. Kwanini tumesalimu amri na kufikiria serikali tatu? Kwanini CCM wameamua tujadili serikali tatu na sisi tunajadili serikali tatu. Hivi kweli watu wanafikiria hili wazo la serikali tatu limetokana na wananchi kwenye maoni ya tume ya Warioba au ni carryover ya mjadala wa 1992?
Nyerere anasema:
Na maneno haya ya Nyerere yasikike kwenye masikio yaliyoziba ya watawala wetu walioshindwa!
Serikali tatu haitotatua matatizo ya Muungano itayaongeza tu. Tunaopinga serikali tatu hatupingi kwa sababu ya gharama tu - hili ni jambo dogo zaidi lakini tunapinga kwa sababu ya mantiki nzima ya kuwa na serikali tatu na nchi mbili! lakini wenzetu wanataka tuwe na nchi mbili na serikali tatu!
Mmoja mifumo mbalimbali au utengano! Kwani nani kasema ni lazima tuungane? Hatutakuwa nchi ya kwanza duniani kuvunjika na watu kuendelea kuishi pamoja na ujirani mwema.