Kwanini si muumini wa Serikali Tatu...

Kwanini si muumini wa Serikali Tatu...

Hizi sintofahamu zote zinakuja kwa sababu tulichagua njia isiyo sahihi katika safari yetu ya kuutafuta utaifa na mshikamano ambazo ndiyo nguzo za Muungano.

Kwa sasa tuko katikati ya safari tunashindwa kuamua kama tuendelee na safari au turudi mwanzo.

Ni vigumu sana kurekebisha jambo la kisiasa ambalo mwanzo wake ulifanyika kimakosa. Hiki ndiyo tunachokiona kwa sasa.

Kama Tume ya Jaji Warioba isingekuwa imefungwa na hadidu za rejea kuhusiana na Muungano, basi ninatumaini tungekuwa kwa sasa tunafahamu nini wananchi wanataka kuhusu hili 'dudu' muungano kwa ustawi wa 'mataifa' yao. Kitu cha kushangaza kwa sasa tunasema tunataka serikali tatu wakati hata hiyo serikali ya pili haijulikani muundo wake na hata wananchi wake sijui wanaishi wapi.

Kura ya maoni ndiyo mzizi wa fitina na kuwepo kwanza kwa nchi ya pili ndiyo mwanzo wa usawa katika kutafuta political legitimacy kwenye negotiation table.

Serikali tatu kwenye political environment hii iliyopo ni hukumu ya kuvunja muungano lakini katika gharama kubwa ambayo ingekuwa offset na kura ya maoni.
 
My perceptions ni kuwa Mwanakijiji ni mmoja kati ya watu ambao wanapenda muungano uvunjike ndio maana kaja na hoja ya serikali moja.
Hajabadilisha "kauli mbiu" yake LET ZANZIBAR GO! amekuja kivingine tu.

Karibu Wakijiji katika jahazi letu la wale ambao tupo kwenye upande wa kuuvunja Muungano.
 
Naona unashindwa kutetea hoja zako na kuanza kung'ang'ania kitu ambacho ni tofauti na kinachoongelewa hapa.

EAC SIYO SHIRIKISHO!

Sifa za shirikisho la kisisa
1. Ngazi mbili za serikali zinazoongoza watu na ardhi moja. Na,

2.Kila ngazi ya serikali ina suala angalau moja ambalo ina uhuru kamili wa kujiamulia, na

3.Kuna uhakika kikatiba na uhakika huo ni guaranteed kuwa uhuru huo unaweza kutekelezwa kwenye eneo la ardhi/mipaka ya ngazi moja ya serikali.


Muhimu zaidi ya yote hayo, ngazi. Ngazi inamaanisha eneo moja yaani serikali moja ni ya juu zaidi ya serikali nyingine. Lazima kuwe na katiba ambayo ni ya juu ya katiba nyingine.

KATIBA YA EAC, KAMA IPO AU ITAKUWEPO .... HAINA NGUVU JUU YA SUALA LOLOTE KWA SERIKALI YEYOTE. Kwa kifupi haina maana na hatuna haja ya kuisikia hapa.
Huyu Mtu wa Pwani hana hoja ni wa kumwacha.
Kila anachosema hana tofauti na mwanasheria wake.
EAC si shirikisho bado hajui hilo na hata sasa hakuna usawa kuna big 3 wenye veto hajui hilo.
Huyu sasa ndiye ametumwa kutoka znz kutetea znz, te te teh huu muungano uvunjike maana tunaungana vitu viwili tofauti.
 
Last edited by a moderator:
Hizi sintofahamu zote zinakuja kwa sababu tulichagua njia isiyo sahihi katika safari yetu ya kuutafuta utaifa na mshikamano ambazo ndiyo nguzo za Muungano.

Kwa sasa tuko katikati ya safari tunashindwa kuamua kama tuendelee na safari au turudi mwanzo.

Ni vigumu sana kurekebisha jambo la kisiasa ambalo mwanzo wake ulifanyika kimakosa. Hiki ndiyo tunachokiona kwa sasa.

Kama Tume ya Jaji Warioba isingekuwa imefungwa na hadidu za rejea kuhusiana na Muungano, basi ninatumaini tungekuwa kwa sasa tunafahamu nini wananchi wanataka kuhusu hili 'dudu' muungano kwa ustawi wa 'mataifa' yao. Kitu cha kushangaza kwa sasa tunasema tunataka serikali tatu wakati hata hiyo serikali ya pili haijulikani muundo wake na hata wananchi wake sijui wanaishi wapi.

Kura ya maoni ndiyo mzizi wa fitina na kuwepo kwanza kwa nchi ya pili ndiyo mwanzo wa usawa katika kutafuta political legitimacy kwenye negotiation table.

Serikali tatu kwenye political environment hii iliyopo ni hukumu ya kuvunja muungano lakini katika gharama kubwa ambayo ingekuwa offset na kura ya maoni.
Tena ikifika wakati wa suala la muungano hata wasomi wanakuwa na akili za ajabu sana

Salim Ahmed amesimamia kura kule Dar, anajua mzozo wa Timor na ameshiriki kule Eritria.
Baregu ni profesa ambaye anatapswa kuangalia mambo kuliko mtu mwingine ndani ya tume
Sengondo Mvungi ni nguli wa sheria hasa Katiba
Warioba alishakuwa makamu wa rais na PM na anaelewa vema matatizo

Sasa sijui ni pesa au ni ulevi gani. Tuliwaambia kura ya maoni kwanza ili tujua hatima ya hili dude.
Ni wazi kuwa hatuna sababu za kuungana tena hasa Watanganyika ambao hawana sababu za kutaka muungano
Wasomi hawa badala ya kukaa na kufuata misingi ya kitaaluma, wakasomewa hadidi za rejea na akina Nape Nnauye sasa hivi hawajui waendelee vipi.

Utashangaa eti kuna SMZ sasa sijui inajadiliana na nani maana Tanganyika haipo!

Hapa option ni kura ya maoni
Ikishindikana vunja muungano
Ikishindikana lete serikali 3 asiyetaka kuwa mkubwa au mdogo aanze mwenyewe!


Hakuna upuuzi wa muungano wa ulinzi na usalama, huo mwisho chumbe.
Wakitaka muungano waeleze wanaleta nini mezani, hatutaki maneno na yani yani, suala ni kuwa wanachangia nini.

Kama hawana wanatulia mamlaka yanachukulilwa na Tanganyika. Huwezi kuchangia 0 mwenzako 10 ukasema umechanga.
Mwenye 10 ni majority share holder na ndiye anaamua mustakabali wa oganizeshi. Hilo wajue
 
MM
Hii haingii akilini hata kidogo,pamoja na maneno na hotuba nzuri za Mwl Nyerere bado suala la kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano hauwezi kuliepusha hata kidogo.Vp inawezekanaje nchi yenye Idadi ya wananchi wasiozidi milioni 2 kuwa na Serikali yao na nyingine yenye idadi ya wananchi inayozidi zaidi ya milioni 40 isiwe na Serikali yake,kwa sababu tu eti Muungano utavunjika,nani anautaka na toka ulipoanza Tanganyika inafaidika na nn?Leo hii siijui nchi yangu na wkt mwingine nashindwa kuwaelezea watoto wangu juu ya uwepo wa Serikali ya Tanganyika.Hii haipo akilini hata kidogo namuunga mkono Rev.Mtikila kwa hoja yake ya utanganyika.
 
MKJJ, hebu niambie, wakati tunaungana na zenji mwaka 1964, tuliua serikali ya Tanganyika kisheria?

Kama hoja ni idadi ya watu, kwa nini, tusikubaliane kurudisha majimbo and so Zanzibar becomes one of the majimbo. Majimbo yanakuwa na tawala zake then tuwe na Federal Gov. Kwa maoni yangu seriklai mbili haziwezekani tena!!
 
Ukimsoma Baba wa Taifa ukamwelewa vizuri utashangaa jinsi tunavyofikiri sasa!! Mwalimu alikuwa anajadili muungano bila kujifunga na serikali mbili tu lakini unaona anashangaa wanaong'ang'ania serikali tatu bila kujadili alternative zingine tena bila majadiliano rasmi kuhusu aina zingine zote za muungano kabla hatujasimama na kutaka serikali tatu tu ambayo inakwenda kuvunja muungano taratibu.

Natamani kuona maoni ya wanasiasa wa sasa hasa kwa kupangua hizi hoja za Mwl Nyerere zilizowekwa hapa (maana wote wanataka serikali tatu).

CC Zitto , John Mnyika , Wilbroad Slaa , Nape Nnauye , Tundu Lisu bila kumsahau Mchambuzi

Mfumo wa sasa wa muungano ni wa Chama tawala kinachoongoza Serikali iliyoshindwa kutawala. Katika zama hizi, hHakuna taifa linaloweza kutawaliwa na chama na serikali kwa wakati mmoja. Ni wale tu wasioelewa ukweli huu ndio watapinga mfumo wa muungano kufanyiwa marekebisho.
 
Zanzibr ipo katika hatua nzuri ya kujirejeshea mamlaka yake kamili tatizo ni kwa watanganganyika hawajui wapi pa kuanzia,nawashauri watanganyika wajaribu kusahau mawazo ya mfu nyerere na waje na mawazo yao kama wao ili tanganyika ipate mamlaka mapya.
 
Point niliyopata kwenye uzi wote ni kwamba, wakati tunaungana tulikuwa mara 40 ya Zenj, sasa ni mara 28 tu! Jamaa wanazaliana kweli!!!
 
We can't let ONE person think and decide on behalf of all the Tanzanians. Mtu mmoja tena of all the people, NYERERE, hawezi kuwa the center and the only quotation and encyclopedia for the fate and destiny of this nation.

Come on guys, let us step ahead and let the bygone be the bygone. If we want any form of a government, its upon us to go for it in anyway we want.

Kumfanya Nyerere kuwa Mungu and the only person to decide for us ni kuendekeza utoto kwamba lazima mama au baba atuamulie.

Nyerere ashaondoka na kuzikwa, mwacheni aende. Mawazo yake ya 1960's hayawezi kuwa valid for all eternity!

Afterall, Nyerere didn't have all the answers!
 
Mwanakijiji kwanza nataka nikuulize maswali yangu ukiyajibu utakuwa umenishawishi nikubaliane na hoja yako.

Nitajitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu bila maneno mengi sana.

1. Kwa nini mpaka sasa kuna serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati Katiba ya Tanzania inasema Tanzania ni nchi moja

Hapa kidogo umechanganya mambo; nchi moja haizuii kuwa na serikali zaidi ya moja au mifumo zaidi ya mmoja ya utawala. Hivyo, kuwa nchi moja kunaweza kuruhusu serikali mbili, tatu au hata mifumo mingine ya utawala wa nchi (serikali) iwepo.
2. Kwa nini wanasema Zanzibar ni nchi katika katiba yao ya Zanzibar

Well, kwa sababu utawala wa Muungano umekubali usaliti wa Katiba ya Muungano bila kujali matokeo (impunity). Tungekuwa na viongozi makini wa Muungano Zanzibar isingejitangaza nchi na mipaka yake na kila kitu halafu ikabakia ndani ya "Tanzania".
3. Kwa nini wana wimbo wa taifa, wa bendera, wana Majeshi yao na Rais wao ni Amrijeshi wa majeshi hayo.

Angalia jibu la swali la pili.
4. Kwa nini Wao Zanzibar na sisi Tanzania Bara au Tanzania na wala siyo tanganyika

Wao pia wanajulikana kama Tanzania Zanzibar na Tanzania Visiwani; sisi kujiita Tanganyika ni suala la hisia tu lakini sidhani kama lingebadili yanayotokea. Kinachogombewa siyo jina.
5. Kwa nini chao ni chao na chetu ni chao pia, mfano madini ya muungano mafuta na gasi ya Zanzibar?

Kwa sababu ya sera mbovu za Chama cha Mapinduzi - Bara na Visiwani.

6. Kwa nini mpaka sasa hatuna mawaziri katika wizara zao ila wao wana wiziri kwenye wizara zetu mfano wizara ya Afya

Kwa sababu kila Mzanzibari ni Mtanzania (ana haki zote za Mtanzania) lakini siyo kila Mtanzania ni Mzanzibari!

7. Kwa nini waitwe Wazanzibar na sisi tusiitwe Watanganyika wakati neno Zanzibar na Tanganyika vilistaili kurokuwepo bali Tanzania

Angalia jawabu la swali la 4.

8. Kwa nini mpaka sasa tuwabebe kwa kuchangia pato wakati tukijua wao uchumi wao ni mdogo wakitegemea karafuu zao ambalo sasa kiuchumi haina kitu wakiwa wameua uchumi wa utalii kwa uendawazimu wao wa utamaduni

Angalia jibu kuhusiana na sera mbovu za CCM.
 
Mzee Mwanakijiji Maswali magumu unatoa majibu mepesi,kwani muasisi wa sera mbovu si ndio huyo Nyerere?
Usione taabu kusema Nyerere ndie alietengeneza hili bomu.
 
Last edited by a moderator:
Maswali magumu unatoa majibu mepesi,kwani muasisi wa sera mbovu c ndio huyo nyerere?usione taabu kusema nyerere ndie alietengeneza hili bomu.

Ah wapi Nyerere aliwaachia kitu kizuri bahati mbaya yeye peke yake alikiamini uzuri wake...
 
Nyerere alifikia hitimisho ambalo hata leo tunaliona. Watu wanataka serikali ya Tanganyika kwa sababu wamechoka na Wazanzibari.
Ukweli ndiyo huo. Ila kuchokana si dhambi .. ni hulka ya binadamu. Na watu wanapochokana ukiwalazimisha kukaa pamboja wanataishia pabaya zaidi. Ndiyo maana kuna taratibu kama talaka, n.k. zinazosaidia watu waachane kwa amani. Hii ndiyo mantiki zilizofuatwa na nchi kama Ethiopia/Eritrea; Czech/Slovakia; Russia & nchi zilizokuwa za kisovieti, etc. Nchi zilizojaribu kung'ang'aniza muungano kama Serbia & FYR (za Croatia, Bosnia, Montenegro, n.k.) au Sudan/Sudan Kusini ziliishia kupigana vitani. Tusilazimishe muungano kama tumechokana. Tuige mfano mzuri wa Scotland ambao wamewachoka sana England; na wameamua wananchi waamue wenyewe kwenye ballot box mwaka 2015.
 
"Muungano ni kama koti, ukiona linakubana shurti ilivue." Abedi Amani Karume
 
Zanzibar huwa kuna "Waziri wa Nchi" ........ Hapo kwenye "nchi" wanakuwa wanamaanisha nchi gani?

Kwa mfano, kuhusiana na Zanzibar, nitakuwa sahihi kama nikisema

Waziri wa Tanzania, Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora.
Waziri wa Tanzania, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum
Waziri wa Tanzania, Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma
Waziri wa Tanzania, Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar
 
Ah wapi Nyerere aliwaachia kitu kizuri bahati mbaya yeye peke yake alikiamini uzuri wake...

Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-lao-na-hatima-ya-muungano-7.html#post6994499

Rais Ali Mwinyi alisema "watanzania ni kichwa cha mwendawazimu"

EAC italeta shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki. Kuendelea na muungano wa ukiini macho/mazingaombwe ni kuchelewesha matatizo na kuongeza utata tu.
Ushauri wa Mwl.Nyerere alioutoa katika kitabu ulichomnukuu Baba ya Le Mutuz unapuuzwa lakini puuzo hilo litaongeza utata tu pale serikali ya Muungano itakapojipa madaraka ya kuziwakilisha nchi wanachama wa muungano wa Tanzania katika mambo ambayo si ya Muungano.

Tumezoea kuunga kamati/tume lakini mapendekezo yao yanawekwa chini ya zulia.

Mzee Mwanakijiji, Muungano wa Tanzania una wanachama wangapi?
 
Mi nadhani huu mjadala wa Muungano uahirishwe kwa miaka 20, na watu wa elimishwe, historia ya kweli iandikwe na ifundishwe mashulei Kizazi kijacho kiamue muungano uweje

Mimi siku zote naamini kwamba muungano wowote duniani lazima utokane na ridhaa ya wananchi wa nchi zinazoungana. Je huu wa kwetu ridhaa hiyo ipo? ukweli ni kwamba haipo na ndiyo maana malalamiko hayaishi kila upande tokea umeanza. Suluhu ni moja tuu kupata ridhaa ya wananchi kupitia kura ya maoni. Mnaweza kuhangaika saaanaa kumbe kuna upande hawautaki huo muungano, mtalazimisha kwa sababu za kisiasa na uchu wa madaraka? au kutowaudhi kakikundi kadogo ka wateule VS wananchi waliowengi? watu wana argue ooh serikali tatu gharama bora ziwe mbili, kwa nini isiwe moja basi? Ukisema Zanzibar itamezwa kwa serikali moja, je haijamezwa kwa kuifanya kama mikoa kwenye serikali mbili? Narudia wananachi wa nchi hizi mbili waulizwe kama kwa dhati kabisa wanahitaji muungano au la, wakijibu NDIYOOOO then waulizwe tena uweje? (serikali 1, 2 au 3?)
 
Hoja ya Mwalimu kwamba serikali moja ingeliimeza Zanzibar naona hii ni hoja potufu ilio na dhamira ya kuwakaanga watu kwa mafuta yao wenyewe. Wakati ule kulikuwa na wazanzibar laki 3, na Tanganyika watu milioni tisa, ration ya 1:30, hivi sasa ni milioni moja Zanzibar na milioni 40 bara, sawa na ration 1:40, ardhi ndio ile ile, kwa ufupi kama hoja ilikuwa valid wakati ule sioni kwa nini isiwe valid kwa sasa? Jengine kama hoja ya Mwalimu ilikuwa imejengwa kuilinda dhamira kutopoteza utamaduni na utaifa wake kwa nini hakukekemea sera ya CCM ya serikali mbili kwenda moja? Au khofu yake hii ilikuwa ya muda tu? Kama ilikuwa ya muda, kitu gani alichokuwa akikisubiri mpaka hii khofu ya kuonekana serikali moja haitoimeza Zanzibar iondoke? Jee kwa sasa hio khofu ya sayidna Mwalim, imeshakuwa neutralised na kwamba kuna mabadiliko hata hii khofu iwe haipo?


Kuhusu gharama kwa serikali ya muungano kuwa kubwa, iweje mambo saba ya muungano yawe na gharama zaidi kuliko 22 ya sasa? Kama uchangiaji Zanzibar itatakiwa ichangie nusu kwa nusu katika shughuli za uendashaji wa muungano, jee mgawo wa mapato nayo Zanzibar itafaidika kwa kupewa nusu ya mapato? Turudi kwenye logic, ni vipi gharama za nchi yenye watu milioni arobaini iwe sawa nan chi ya watu milioni moja? Jee nafasi za serikali ya muungano ikiwa Zanzibar itatakiwa kuchangia nusu kwa nusu, vipi na nafasi za wafanyakazi wa serikali ya muungano zowe nusu kwa nusu? Vipi bunge la muungano nalo liwe nusu kwa nusu? Turudi tena kwenye gharama, kwa mfano uendeshaji wa jeshi la muungano, ni nani hasa atakaetumia facility za jeshi zaidi kati ya ukubwa wa karibu kilomita za mraba laki tisa na ile ya kilomita za mraba 2000? Kinachoshangaza ni malalamiko makubwa juu ya Zanzibar kuchangia nusu katika bajeti ya serikali ya muungano, lakini mgawo ni wa asilimia 4% kwa Zanzibar, hii haikubaliki kwa logic yoyote.


Maneno mengi yamezungumzwa kuhusu Mwalimu kama ndie alieamua tuwe na serikali mbili, na kwa jinsi Mwanakijiji anavyoeleza inaonekana Mzee karume ndie alietaka serikali moja lakini Mwalimu alikataa kwa sababu ya khofu yake ya kuimeza Zanzibar. Hii hai make sence kabisa, tuangalia circumstantial evidence kwa upande wa Mzee Karume hasa kwa vile nae ndie mdau mkuu kama ilivyo kwa Nyerere katika muungano wake alisemaje juu ya serikali moja. Kwanza hakuna documentation yoyote inayomueleza Mzee Karume kama ni muumin wa serikali moja, au contraire zipo evidence zinazoenyesha hakuuamini hata muungano wenyewe. Azimio la Arusha, Kwa kauli ya Mzee karume ni kwamba mwisho chumbe, kauli yake ya muungano kama koti likikubana ulivue, inaonyesha imebase katika serikali moja? Alipowarejesha wanajeshi kutoka Zanzibar kwa kuwa hakukubaliana na Mwalimu katika azma yake ya kusaidia ukombozi wa nchi jirani tutasema kwamba alikuwa ni mpenzi wa serikali moja? Hata kupitia marais wote waliopita baada ya Mzee Karume hakuna aliekubaliana na hoja ya serikali moja. Huwezi kulazimisha umoja kwa kudharau maoni ya wananchi, jee kuna utabiri wowote uliofanywa wa kitaaluma unaofavour serikali moja hususan kwa ukuswanyaji wa maoni kutoka Zanzibar?


Twende katika sehemu ya mwisho ambayo naiona ni muhimu zaidi, jee TRA, BOT, financial institutes, fiscal institutes, World Bank, IFM na taasisi zilizoindependent zimewahi kufanya research ya argument ya gharama za serikali tatu na zikawafavour wanaosema uuendeshwaji wa serikali tatu ni gharama? Huwezi kubase ideology ya gharama kwa kutumia mantiki matupu, kunatakiwa kuwe na back up ya hoja hasa zinazojengwa na gharama kupitia studies independent sio logic ya hesabu za trilioni ngapi zitatumika wapi bila ya mchanganuo wa kisomi.
 
Back
Top Bottom