Kwanini si muumini wa Serikali Tatu...

Kwanini si muumini wa Serikali Tatu...

Nguruvi3,

..Watanganyika tutapata serikali yetu.

..Hiyo itatupa nafasi ya kuwa na chombo kinachotusemea kuhusu masuala ya muungano.

..Wazanzibari wakidai wapewe 21% ya ajira za muungano, basi atakuwepo Mtanganyika atakayeuliza kwanini iwe hivyo.

..sasa hivi Makamu wa Raisi ni Mzanzibari. Ofisi yake ndiyo inashughulika na kero za muungano. Waziri wa nchi mwenye portfolio ya muungano naye anatokea Zanzibar. Sasa unategemea wa-Tanganyika tutatendewa haki hapo??

cc Mzee Mwanakijiji, Mchambuzi
Kuntu! Ndio maana tunasema sauti, jeuri na dharau ya znz ni kwa kuwa Tanganyika haipo. Narudia tena na tena mfano huu, wiki iliyopita kamati ya maridhiano ya Zanzibar ilitoa mapendekezo na moja kati ya hayo ni kuwepo na uraia wa kila nchi huku passport za kusafiria zikiwa Tanzania-Tanganyika na Tanzania-Zanzibar. Zanzibar ilikataa kuitwa Tanzania visiwani au sehemu ya Tanzania siku za (ilikataa vipi msome Mchambuzi huko nyuma)

Maana nzima ya suala la hilo ni kutambua Tanganyika ipo njiani na namna pekee ya ukaribu nayo ni jina Tanzania. Kwa jinsi Wazanzibar walivyofundishwa kuwachukia Watanganyika hilo neno Tanzania ni haramu ni najisi inayohitaji tohara kubwa. Inapofikia mahali wanakubali passport yao iwe na Tanzania lipo jambo zito

Juzi Jusa Ismaili ametaka sarafu iondolewe katika muungano. Mh alikwenda aliita sarafu ya sasa haina baraka. Wakati wanachukua biioni 32 hakuna aliyesema ni pesa haramu.Dr Magoti amesimamia chuo kilichogharim bilioni 5 za muungano hakukuwa na uharamu.Tanganyika ikirudi kila mmoja atasimamia haramu na halali zake.

Tanganyika irudi ili iwepo na kura ya maoni kuamua haja ya muungano tena.
Kama ipo basi kila mmoja aje mezani na mchango, siyo jina au sheria za ajira.

Bila Tanganyika kusimamia Watanganyika tutabaki kulipa kodi, zinakusanywa na kwenda kusikotarajiwa.
Zanzibar imepata mgao mkubwa wa bajeti ya muungano kuliko Singida!

Nani wa kuwaongelea Watanganyika wa Singida na wao watalalamika wapi ikiwa wao ndio muungano? Kwanini hatutaki kutoa fursa kwa Watanganyika kupanga mipango yao kama Zanzibar?
 
Nguruvi3,

..Watanganyika tutapata serikali yetu.

..Hiyo itatupa nafasi ya kuwa na chombo kinachotusemea kuhusu masuala ya muungano.

..Wazanzibari wakidai wapewe 21% ya ajira za muungano, basi atakuwepo Mtanganyika atakayeuliza kwanini iwe hivyo.

..sasa hivi Makamu wa Raisi ni Mzanzibari. Ofisi yake ndiyo inashughulika na kero za muungano. Waziri wa nchi mwenye portfolio ya muungano naye anatokea Zanzibar. Sasa unategemea wa-Tanganyika tutatendewa haki hapo??

cc Mzee Mwanakijiji, Mchambuzi

Katiba ya JMT (1977) ili establish a constitutional court ya kukabiliana na disputes za muungano ambazo zingeweza kujitokeza; Lakini mahakama hii haikuwahi kuketi hata siku moja kujaribu kutatua kero za muungano kwani ni upande mmoja tu wa muungano uliopatiwa fursa hiyo lakini haukufanya hivyo; badala yake zikajitokeza tume baada ya tume na pia wizara ya masuala ya muungano ikaja kuundwa, lakini hakuna cha maana kilichofanyika zaidi ya kutengenezea tu watu vyeo, vichaka vya ulaji na perception kwamba wana umuhimu katika muungano;

Kero za muungano kiini chake imekuwa ni uchakachaji wa mkataba wa muungano wa 1964;Baada ya kuchoshwa na kero zilizopo ambazo zilichochewa na ccm, mwaka 1983-84, rais wa wa znz kwa wakati ule, mzee aboud jumbe aliamua kujitoa mhanga and brief mawakili husika juu ya kero zilizopo pamoja na implications kwa znz na kuwaomba mawakili husika waandae papers to submit kwenye mahakama ya katiba kuhusiana na breaches za articles of the union zilizokuwa zikiendelea; ingawa hatua ya Jumbe was purely constitutional, kiongozi huyu akaishia kukumbwa na matatizo ambayo hatoyasahau kwa maisha yake yote yaliyosalia duniani; kufuatia tukio hili, sasa ikawa dhahiri kwamba hakuna kiongozi wa Tanzania (including Mwalimu) who took the constitution or constitutional court seriously; kwa maana nyingine we had a constitution, but we lacked constitutionalism; its about time that we begin constitutionalism process in Tanganyika;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hawaii ilipojiunga na marekani (August 21 1969) haikuona haja ya kuwa na uwakilishi sawa ktk muungano huo. hatuoni uwakilishi wa hawaii ktk senate wa 50-50 unaodaiwa na znz hapa tanzania.

Mie bado naona muharobaini wa muungano na matatizo mengine hapa bongo ni kuwa na majimbo tunaogopa nini?
 
Mkuu Nguruvi3, naomba nitoke nje kidogo ya mada; Kuna mtu mmoja wa idara ya takwimu alikuwa ananieleza juzi kwamba Tanzania inafaidika zaidi na uhusiano wa kiuchumi na visiwa vya comoro kupitia biashara ya mbuzi na n'gombe pekee kuliko uhusiano wa kibiashara na visiwa vya zanzibar; sikupenda kuamini taarifa hii, wewe unaionaje? Kama ni kweli, basi Kwa kweli ndugu wetu wanzanzibari kazi wanayo;
Sina shaka kabisa kuhusu hilo. Si mara moja au mbili yametokea madhara makubwa baharini meli zao zikitoka Tanzania.

Kuna wakati wacomoro walikuwa wanatafuta njia ya kuwa na uhusiano mkubwa sana na Tanzania zaidi ya uliopo.Wengi safari zao za nje na za kibiashara huanzia Tanzania.

Tunasema kuwa Tanganyika irudi kwanza, kura ya maoni ifuate kila mmoja ajipime kama ana umuhimu na upande wa pili. Hilo ndilo muhimu kabisa!

Ninachokiona mbeleni ni kuwa hata rasimu ikipitishwa kwa nguvu za kisiasa na bunge la kisiasa na kutiwa saini na viongozi wa kisiasa bado tatizo ni kubwa sana. Watanganyika ambao sasa wanauchungu na utaifa wao watauliza , kwanza lini walishirikishwa katika kuandika katiba.

Pili wakati katiba inaandikwa wao walikuwa wapi kutoa maoni. Na kwanini maoni ya nchi ya Zanzibar yawe maoni ya Tanzania. Nani alisimama kutetea masilahi ya Tanganyika na kwanini rasilimali za Tanganyika ziwe za muungano. Ni donda bichi kabisa litakaloleta matatizo makubwa.

Hivi kwanini haya mambo yasimalizwe kiistaarabu na kwa mantiki iwe muungano au kuvunja?

 
Hueleweki,kam kweli mwatubeba kip mnachongangania serikali MOJA minaona ili kuthibitisha usemi wenu wakutubeba vunjeni MUUNGANO nasis tushaanza kupitia AMAN KARUME Nyinyi malizeni,tafuta mtu akusomeshe ukoloni
 
Hueleweki,kam kweli mwatubeba kip mnachongangania serikali MOJA minaona ili kuthibitisha usemi wenu wakutubeba vunjeni MUUNGANO nasis tushaanza kupitia AMAN KARUME Nyinyi malizeni,tafuta mtu akusomeshe ukoloni
Hamjafanya hivyo hata mara moja. Tuliwaambia msiteue wajumbe wa tume kwanza kabla ya kura ya maoni.
Hamkufanya hivyo. Tukawaambia pelekeni mswaada BLW na BLM, hamkufanya hivyo. Tukawaambia mwiteni makamu wa rais na mzuie wabunge kuja Dodoma hamkufanya hivyo. Sasa wapi mnapata nguvu ya kusema 'mlianza' na wengine wamalize?

Kama mnataka kuvunja muungano, mbona mnataka muungano wa ulinzi na usalama?

Tanganyika inatakiwa irudi kwanza halafu mambo mengine yatakuwa mezani. Watanganyika wataamua kama muungano huu una faida yoyote kwao. Watakapopata jibu watalitoa kwa wazanzibar ambao wataamua hatima yao.
Ndio maana tunasem ngojeni Tanganyika irudi kwanza, mambo ya kugawana vyeo na nafasi za ajira 21% siyo muhimu na yenye masilahi kwetu. Masilahi yetu yapo ndani ya Tanganyika na wakati huo ukifika kila jambo na kila option itakuwa mezani.
 
Mzee Mwanakijiji, Kobello, na wengine wote mnaopendelea serikali moja:Kwanza niseme kwamba kwa kweli tupo wengi sana tunaopendelea Tanzania ifuate mfumo wa serikali moja lakini nadhani tofauti yetu na yenu zipo katika maeneo makuu mawili: ·

Kwanza, kwa upande wetu, tunaangalia zaidi ‘practice’ kuliko ‘theory’, na katika hili, tunaona wale wote wenye kupendelea mfumo wa serikali moja katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni ‘wishful thinkers’.
·
Cc Nguruvi3, Jasusi, joka kuu, Pasco, MTAZAMO
Mkuu Mchambuzi, kwanza naomba kukupongeza sana kwa bandiko lako hili kuhusu hoja ya serikali tatu.
Pili nakupongeza sana!... sana!... sana...! kwa kuwa very practical!. Mimi nilibahatika kusoma enzi za kuchukua masomo yote, arts na science, hivyo nimekumbuka kuhusu "theory" na "practical" ni vitu viwili tofauti!. Tuna watu wazuri kwa theory nzuri sana ila haziko practical!. Nyerere mwenyewe na ile siasa yake ya Ujamaa na Kujitegemea ilikuwa ni "theory" nzuri sana!, mwanzo alipolitangaza Azimio la Arusha, alisema itaichukua Tanzania miaka 30, kuwa nchi ya Ujamaa kamili!. Baada ya miaka 30!, akakiri kuwa ujenzi wa ujamaa utachukua muda mrefu zaidi!, na kukiri kuwa huko nyuma tulifanya makosa! "Kufanya kosa sii kosa!, kosa ni kurudia kosa!". Yule Mzee mpaka anakwenda kaburini, amekiri kuwa amekuwa anakwenda na vitabu viwili tuu kila andako, Biblia na Azimio la Arusha!, amekuwa akilisoma na kulisoma, hakuona kosa popote kwenye theory!, tatizo ni kwenye practical na ndiko lilikofia!.

Humu jf, tunadadili hoja nyingi, ila nakiri ni watu wachache sana wa calbre yako Mkuu Mchambuzi ambao wako practical!, mmoja wa cabre hii ni Mkuu Nguruvi 3 nadhani kuna wengine wachache, the rest ni "wishful thinkers!".
Kuna baadhi ya mada zangu humu, mimi huwa najitanaibasha kuwa ni "realist!" kuufuata ukweli halisi ule wa "is" and not "ought to be!".

Sehemu kubwa ya badiko hili ni kuijibu hoja ya Mzee Mwanakijiji kuhusu serikali moja!. Ukaamua kumpiga darasa la ukweli kuhusu hoja hii!. Nilipolisoma tuu bandiko hili, nilisema Mzee Mwanakijiji ni very intelligent fellow!. Wengi mlidhani anaandika ili kuitetea serikali moja!, no!, no way!. Ukilisoma bandiko hili with reference ya bandiko jingine la Mzee Mwanakijiji, la Let Zanzibar Go! utagundua "the motive behind!".

Katika bandiko hili, hayo mengine yote aliyoyaandika Mzee Mwanakijiji ni mazungumzo tuu baada ya habari, ujumbe rasmi wa Mzee Mwanakijiji katika hoja ya Serikali moja ni huu kwenye para yake ya mwisho
Mimi napinga serikali tatu - naamini kama kweli watu wanataka tuimarishe Muungano basi ni kuunda nchi moja, serikali moja mifumo mbalimbali au utengano! Kwani nani kasema ni lazima tuungane? Hatutakuwa nchi ya kwanza duniani kuvunjika na watu kuendelea kuishi pamoja na ujirani mwema.

Huu ni muyendelezo tuu wa "Let Zanzibar Go!", kuitumia hoja ya serikali moja to kick them out!. Japo Mzee Mwanakijiji ni theorist mzuri, anayetest practicabilities ya baadhi ya theories zake!, naamini katika hili la Muungano, anaelewa fika "practicability ya theory ya serikali moja!. Kiukweli naamini sio kweli kuwa anaamini katika serikali moja, kwa vile anaishi katika nchi ambayo inatumia fedaral system, anachotaka sio serikali moja, bali matokeo ya serikali moja katika muungano wetu adhimu!.
Pasco.
 
Katiba ya JMT (1977) ili establish a constitutional court ya kukabiliana na disputes za muungano ambazo zingeweza kujitokeza; Lakini mahakama hii haikuwahi kuketi hata siku moja kujaribu kutatua kero za muungano kwani ni upande mmoja tu wa muungano uliopatiwa fursa hiyo lakini haukufanya hivyo
Mkuu Mchambuzi, Katiba ya JMT, haikuestablish, bali ili provide kipengele cha kui constitute hiyo mahakama!. Haijawa constitituted kwa sababu hakujawa na kesi yoyote ya kikatiba ambayo wanasheria wameomba hiyo mahakama iwe constituted!. Kuna baadhi ya hoja Mahakama ina weza ku act on its own volition, lakini kuna issues mahakama haiwezi ku act, mpaka iwe propmted to act!.
 
una uhakika wanataka serikali yao? au wanataka nchi yao? kwenye nchi sasa na serikali ya sasa wao wamekosa nini hasa ambacho watakipata ikija Tanganyika?
Autonomy na sovoreignity wanayoitaka Wazanzibari in ring sentiments sawasawa kabisa kwa Watanganyika!

Tatizo kubwa la Wazanzibari ni kwamba wamepiga kelele nyingi na kwa muda mrefu kutaka hatimae kujitoa muungano, na hili ni dhahiri ama sivyo kusingekuwepo na underground movements kama za uamsho.

Whats good for the goose is also good for the gender!
Kilio cha wanzanzibar kimeeleweka vyema na Watanganyika, na wengi tumegutuka sasa tuna wabebea nini?
Kuna mambo mengi ya kiuchumi tunayowabeba kwa mfano TANESCO hawalipi,wako kwenye Bunge la Muungano na huku wakilipiwa na serikali ya muungano.
Wanalo Bunge lao-Baraza la Wawakilishi.

Hapa ndipo wengi tulio na roho ndogo twasema kila mundu ave na kwao!!
Bora kila watu wajitawale vyema na kubeba mizigo yao wenyewe.
 
Autonomy na sovoreignity wanayoitaka Wazanzibari in ring sentiments sawasawa kabisa kwa Watanganyika!

Tatizo kubwa la Wazanzibari ni kwamba wamepiga kelele nyingi na kwa muda mrefu kutaka hatimae kujitoa muungano, na hili ni dhahiri ama sivyo kusingekuwepo na underground movements kama za uamsho.

Whats good for the goose is also good for the gender!
Kilio cha wanzanzibar kimeeleweka vyema na Watanganyika, na wengi tumegutuka sasa tuna wabebea nini?
Kuna mambo mengi ya kiuchumi tunayowabeba kwa mfano TANESCO hawalipi,wako kwenye Bunge la Muungano na huku wakilipiwa na serikali ya muungano.
Wanalo Bunge lao-Baraza la Wawakilishi.

Hapa ndipo wengi tulio na roho ndogo twasema kila mundu ave na kwao!!
Bora kila watu wajitawale vyema na kubeba mizigo yao wenyewe.
Kuna hoja moja kaitoa JokaKuu hapo juu kuhusu 'unfairness' wanayopata Watanganyika.

Natafakari, kunapokuwepo kikao cha suala la muungano Zanzibar inakuja kupitia SMZ.
Katika kikao kuna Makamu wa Rais, mawaziri na hata makatibu wakuu ni wazanzibar.

Kundi hilo la makamu wa rais linabadilika hapo hapo na kuwa viongozi wa muungano.
Tayari znz inakuwa ina uwakilishi kama SMZ na kukimbia upande wa pili kuwa referee
Sasa linapotokea suala linalohusu Tanganyika nani anasimama na kutetea?

No wonder wznz wanaweza kuja na formula ya kile wanachotaka, hakuna wa kuuliza ni kwanini, aliyepaswa kuuliza ni Tanganyika ambaye yupo mkutanoni lakini kama kivuli.Anahitajika tu katika mchango na ni wakati huo znz inageuka kivuli!!

Mambo kama haya yanawapa kiburi cha kutaka 21% ya ajira au 11% ya mgao wa pato la taifa bila haya.
Aliyepaswa kuuliza mchango znz ni mshirika mwenza Tanganyika ambaye ni kivuli tu.
Hapo unaona jinsi Tanganyika ilivyonyimwa fursa.

Bungeni wznz wanaamua jambo linalowahusu Watanganyika,kwa mfano kupitia waziri wa afya ambaye si Mtanganyika ku-move agenda zao. Hakuna Mtanganyika anayeingia BLW. Nani atasimama kutetea masilahi ya afya za Watanganyika na kwa uzalendo gani? Waziri aliyepo ni mznz anayetaka mamlaka kamili,atasimama vipi kumtetea 'mkoloni mweusi'

Kwa msingi huo tunasema Tanganyika irudi kwanza ili itetee masilahi yake na kama kuna ulazima wa muungano ambao mimi siuoni! basi Tanganyika ikae na mshirika wake znz kila mmoja akilinda masilahi yake.

Wakati znz wakitaka mamlaka kamili, Tanganyika nayo ipewe fursa ya kumiliki na kudhibiti rasilimali zake ambazo ndizo nguzo ya muungano. Katika usawa huo kutakuwa na adabu na maelewano.

Kurudi kwa Tanganyika ni haki.
Kura ya maoni kwa znz kuamua hatima yake na Tanganyika kutathmini umuhimu wa muungano vitafuata kila mmoja kivyake
 
Habari Wakuu wangu! Japo nimechelewa lakini si mbaya nami nikaweka hili.
Kwanza napenda kuweka wazi imani yangu, kwamba katika UMOJA mimi ni muumini, na katika aina yoyote ya UMIMI mimi si muumini hata kwa ukaribu. Katika Utaifa mimi ni muotaji wa AFRIKAMOJA, lakini ni katika Ustawi wa mtu mweusi si kujifurahisha! Hivyo katika hili jambo, muhimu kwangu si kuendeleza Muungano , bali ni kufikia USTAWI wa mwanaafrika wa mipaka hii ya kwetu(TZ). Ni kuhakikisha UENDELEVU wa elements BORA na SAHIHI za mtu mweusi, kiuchumi, kisiasa na kitamaduni hayo ndio MAENDELEO. Hivyo tunapojadili aina bora ya Muungano si ile ambayo itafanya udumu bali ni ile itakayo-guarantee UENDELEVU tajwa, kama hakuna namna hiyo basi HAKUNA HAJA YA KUUNG'ANG'ANIA MUUNGANO! Binafsi ninaamini katika Nchi 1, Taifa na Serikali 1. Kama alivyosema Mkuu notradamme, kwamba serikali 1 ni suluhisho sahihi la kuleta ustawi wetu na kuudumisha Muungano, lakini ni ngumu haswa kuifikia, naungana naye moja kwa moja. Ngumu sana kufikia lakini INAWEZEKANA, muhimu ni kutokukwepa gharama sahihi za Umoja kwa vigezo batili vya kulinda Demokrasia, kama hatuwezi kumudu gharama hizo basi tusilazimishe kuungana kwa namna isiyofaa, HAITATUSAIDIA zaidi ya kupoteza muda. Tusimame leo tupaze sauti zetu kushawishi raia kuvunja muungano, maana wote namna sahihi ya muungano tunayoiona ni impractical 'just a wishful thought', sasa kufumba macho na kugeukia nyingine kwani Kuungana nani kasema lazima!? Lengo ni kulinda Muungano au kuleta Ustawi wa mtu mweusi?
Ikumbukwe kuwa tunaposema Nchi Taifa na Serikali Moja si kuwaunganisha wazanzibar na watanganyika kiutawala tu, bali ni kuwa na Imani moja, Dira moja-FIKRA MOJA katika kuhakikisha ustawi wa TANZANIA. (Mkuu wangu Mchambuzi anaita ni wishful thoughts, nachofurahi hata yeye anazo, ila tu hajaona uwezekano wa kuwa hai, ni hatua nzuri kuwa nazo tu, nikutie moyo Mkuu wangu you are not thinking in vain-those wishful thoughts are real/practical) Aina nyingine ya Umoja mbali na hii ni Unafiki. Tunataka tuzike Utanganyika wetu na Uzanzibari wetu chini (imani, itikadi, historia, desturi, mienendo, mitazamo) uzaliwe UTANZANIA, zao la Uzanzibar na Utanganyika kwa mujibu wa Nyakati na Mazingira yetu mahususi, ni ngumu sana lakini zaidi ya hilo ni Unafiki, ni bora kuvunja kilichopo!
Mkuu wangu Mchambuzi anataja baadhi ya faida za Serikali 3 over 2 nadhani na 1 katika uzi wake. Ningependa kuziongelea hapa, kwa kuhusisha na practical na wishful thoughts iliyoibuka katika uzi huu!
(a) Kupata Fursa ya Ushindani. Hivi kweli tunaweza ku-guarantee good katika ushindani wa Utanganyika na Uzanzibari chini ya kivuli chepesi cha Utanzania? Kwanini hli ndio lisiwe impractical? Only 7 union affairs, ni kwa namna gani yanaweza kumfanya mzanzibari kumbeba mtanganyika akamuacha mzanzibari mwenzake? Kwa namna gani Utanzania unaweza kuubeba Uzanzibari na Utanganyika? Mkuu Fundi Mchundo amegusia hili, Utanzania haiwezekanni kusimama mbele ya uzanzibari na utanganyika. Tena chini ya fikra hizi hizi za wao makafiri, wao waarabu, wao wakoloni, wao tunawabeba,n.k(hakuna anayekataa uwepo wake) ni ushindani gani tunaouona unawezekana? Gharama za kuondoa hilo ni kuwa na FIKRA/IMANI/ITIKADI MOJA ya kujenga Taifa moja katika kila kitu chake. Tukishndwa hilo, Je, haitotokea kama alivyosema Mkuu Nguruvi3, serikali tatu means mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama!? Undava-Undava! Nani atakula na nani atashindwa? Kwenye ushindani aina hiyo kula nyama kwa kisu chako kikali si kulitumia jasho la mwenzako? Tuko tayari kujenga matabaka ya namna hiyo, kwa gharama gani? Je, kufikia Ustawi wetu hapo ni practical ama wishful thoughts? Kwanini tuamue bora liende tu badala ya kuuvunja kabisa Muungano?
....nitarudi.....
"(b) Kupata Fursa ya kubadilishana uzoefu. (c) Kupata nafasi ya kuishi Self Rule pamoja wakati huo huo kuishi Shared Rule. (d) Kuruhusu Demokrasia. (e) Kulinda right of people to self determination, kwa hoja kuwa hakuna upande uliotayari kupoteza their identities and autonomy. (f) Kupata Ufanisi. Kupunguza kodi na gharama nyinginezo!"
 
Last edited by a moderator:
basi na tuuvunje, kwanini nyinyi watanganyika munahofia kuvunjika kwa muungano....? Mbona hatukueleweni,
 
Siamini kuwa NYERERE alikuwa ni zaidi ya BINADAMU....
Wala siamini kuwa HAKUWA MKOSEFU....
Ila naamini kwa dhati kwamba alikuwa anafikiria kwa mapana saaana kuliko waafrika wengi wa kizazi chake na hata kizazi cha sasa.
Maono na misimamo yake juu ya muungano yatabaki kuwa sahihi na TUKIYAPUUZA NA KUYAONA YAMEPITWA NA WAKATI,,, nina hakika tutajuta.
Huu ubinafsi wa kisiasa wa kuangalia faida za watu/vyama badala ya maslahi mapana ya taifa utakuja kutuangamiza.
Naipenda tanzania
Nawaona wazanzibar ksma watanzania
Na nitasikitika wakituacha/tukiwaacha.
I stand with nyerere no matter what
 
.....inaendelea.....
(b) Kupata fursa ya Kubadilishana uzoefu. (Zanzibar-Tanganyika) Hapa sielewi ni uzoefu gani tulioukosa, na nafasi yake katika kumnyanyua mwanaafrika wa mipaka hii. Hatari iliyopo ya Uhasama, inaweza kubebwa vipi na sake ya Uzoefu? Tunashindwa nini kuwa kitu kimoja, tukautafuta kwa Wazambia ama Kenya na Msumbiji. Kwanini ni lazima iwe ni Tngnyka na Z'bar?
(c) Kuishi Self Rule wakati huo huo Shared Rule! Inawezekanaje? Je, si kwa hisia tu? Ili kuleta heshima na utaratibu sahihi kwa watu dhidi ya tawala zao, ni lazima kuwe utawala Mkuu utakao-shape mengine yote. Sasa, ipi iwe msingi? Je, ni ile ya Jamuhuri chini ya mambo 7 tu!? Itawezaje ku-shape mbili salia? Yaani mambo saba yataathiri vipi Utanganyika hadi mimi niusahau na niugeukie Utanzania? HILO HALIPO! Wishful thoughts! Hili linaambatana na hoja ya kwamba...
(d) Serikali 3, italinda Right of People to Self Determination! Ili iwe nini kwanza!? Yaani kusema mimi ni Mzanzibari na Wewe ni Mtanganyika tena bila aibu ni ndani ya Tanzania, bado nayo tuite Haki inayopaswa kulindwa!? Kwani Utanzania hauwezi kuwa ndio Self Determination yetu? Niliwahi kusema hivi, kadri unavyomfundisha Mtanzania kuwa mzalendo wa nchi yake, ndivyo unavyokuza uadui kati yake na yule wa Kenya, Rwanda, na Burundu! Inatusaidia nini? Uzanzibari unapokomaa ndani ya Utanzania, athari ya kwanza ni kwa Utanganyika si kwa Uburundi ama Ughana! Kwanini tunaona huko kunafaa? Je, ku-guarantee maendeleo si Kiini macho?
(e) Kuruhusu Demokrasia. Sipendi kulizungumzia sana, lakini hili liko wazi kabisa, kufikiri kwamba kwa Nyakati na Mazingira yaliyopo ya nchi za kiafrika Tunaweza kuishi Demokrosia, these are wishful thoughts indeed! Niseme pia hili, gharama ya (kuifanya hai) kuubeba mzigo mzito wa Demokrasia kule Amerika na Ulaya, inabebwa na nchi nyingi za kiafrika. Sisi tunaitaka, ni nani atakayetulipia gharama hzo? Kwanini ngumu kuelewa hapa? Tumempata wapi? Demokrasia sio kitu cha kujivunia hata kidogo!
(f) Kuleta Ufanisi. Mimi naamini wazi kabisa, Ufanisi katika chochote kile unaletwa kwa watu kufanya kazi kwa pamoja kushirikiana na kushikamana kama timu! Kukishakuwa na wa kuvuta kushoto mwingine kulia, Ufanisi ni wishful thoughts! Uzanzibar+Utanganyika chini ya kivuli batili cha Utanzania, ni Majanga!
Kama atuwezi kuupigania Ukweli tunaouona leo, tusitaraji heshima toka kwa wajukuu zetu! Tusiangukie Ubatili kwa kukwepa gharama za Ukweli! HATUTAFIKA!
Mungu yu tayari kutupigania vitani. Anaita sasa!
 
Back
Top Bottom