Zanzibar huwa kuna "Waziri wa Nchi" ........ Hapo kwenye "nchi" wanakuwa wanamaanisha nchi gani?
Kwa mfano, kuhusiana na Zanzibar, nitakuwa sahihi kama nikisema
Waziri wa Tanzania, Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora.
Waziri wa Tanzania, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum
Waziri wa Tanzania, Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma
Waziri wa Tanzania, Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar
EMT
Tanzania ni Muungano wa nini? Nchi, majimbo, wilaya, vijiji?
Tanzania ina wanachama wangapi?
Kama hadhi ya nchi zilizoungana zilibadilika, zilichukua hadhi ipi? Majimbo? Mikoa? Wilaya au?
Tunajaribu kuhalalisha ukiini macho lakini huwa hatufiki mbali.
Serikali ya Muungano inafanya kazi za mamlaka mbili, mamlaka ya mambo ya muungano na mamlaka ya mambo yasiyo ya muungano ya Tanganyika(kama ni mshabiki wa mazingaombwe, Tanganyika isomeke Tanzania bara)
Tafuta mambo ambayo si ya muungano kwa upande wa Tanganyika baadae jaribu kuuhakiki mchango wako, mfano Uwe Tanganyika aka (Tanzania bara) badala ya Zanzibar ndio utaelewa kuwa wadanganyika tuna matatizo. Tunajifanya mbuni kuzika kichwa ardhini wakati mwili wote unaonekana. Wanaona wale tu wenye macho!