Inawezekana kabisa Mwalimu Nyerere alikuwa sahihi wakati anaongea mambo aliyoyanukuu MMM. Ila ukweli ni kuwa kuongelea serikali moja kwa sasa ni kupingana na uhalisia wa mambo ulivyo. Mambo yamebadilika sana tangu Nyerere alipoongea. Zanzibar ina katiba mpya ambayo kimsingi imeifanya kuwa nchi kamili yenye rais, bunge, mahakama, jeshi, wimbo wa taifa, utaifa-uzanzibari, na eneo kama lilivyoainishwa kwenye katiba yao. Leo hii muungano ukivunjika wenzetu wa Zanzibar hawana shida kwani tayari wana mfumo wa kiutawala unaofanya kazi. Sasa kuongolea serikali moja ni sawa kabisa na kuwaambia wazanzibari wavunje serikali yao, bunge lao na utaifa wao ambao wamekuwa nao kwa miaka mingi. Hili halitawezekana na utakuwa ni ubeberu mbaya hata kuliko ule wa mkoloni. Kwa watanganyika hakuna shida kwani tayari serikali yetu ilishavunjwa na kugeuzwa kuwa ya kiruhani ambayo ni mali ya wote.
Mfumo wa sasa wa Serikali mbili haubebeki tena kwani umekuwa ni kero kwa muungano hasa kwa wazanzibari ambao wanauona kama kikwazo cha wao kupata uhuru kamili wa kusimamia mambo yao. Lakini pia ni kero kwa watanganyika kwani tunaona wazanzibari wakipata fursa ya kujadili na kusimamia mambo ya Tanganyika kwa kisingizio cha utanzania wao. Tuna kamati za bunge zenye wajumbe wazanzibari ambazo zinajadili taasisi zisizokuwa za muungano na vile vile tuna mzanzibari amepewa uwaziri wa wizara ya afya ambayo ni ya Tanganyika.
Tanganyika haiwezi tena kuendelea na uruhani katika mazingira ya sasa yanayotaka kuwepo kwa uwazi katika uendeshaji wa masuala ya serikali. Hivyo kuna njia mbili tu zenye uhalisia zaidi:ya kwanza ni kuwa na serikali tatu ikiwepo ya Tanganyika inayoonekana wazi na inayojulikana inachosimamia kwenye muungano na Zanzibar na pili kuvunja muungano na kila mmoja achukue hamsini zake ila tuwe na mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi na labda kiulinzi. Kwa kuwa tume ilipewa hadidu za rejea zinazoitaka kulinda muungano basi waliona hii ya kuwepo kwa serikali ya Tanganyika kama option pekee inayofaa na mimi nawaunga mkono kwa asilimia mia moja.