Kwanini Serikali inawajengea nyumba walimu?

Kwanini Serikali inawajengea nyumba walimu?

Hata wa milembe huwa wanadhani sisi wazima ndo vichaaa.............

Zamani ilikuwa mtu anaanza kuwa kichaa then anaokota makopo , lakini siku hizi ni kivyume... Watu wanaanza kuokota makopo halafu baadaye wanageuka kuwa vichaa
Wewe usijifanye kujua wakati hujui chochote zaidi ya kusoma na kuandika tu! hizi falsafa zako za kitoto wapelekee watoto wenzio wa mitaani. Wewe sio "moderator" wa JF, huna mamlaka ya kumuamru mtoto yeyote hapa jukwaani. Kaa pembeni uwe msomaji tu kwani huwezi kuchangia chochote cha maana kwa elimu yako duni!
 
jamani kazi ya walimu ni ngumu sana achilia mbali kufundisha ,kuna kupitia madaftali ya wanafuzi wote
assume mwalimu ana wanafunzi 45ktk darasa moja
ana madarasa matatu anayofundisha 3*45=
ana vpindi labda vitatu kila darasa kwa wiki 3*3*45-=
kila siku anahitaji posho au overtime

Ni kweli kabisa. Na ukitaka mwalimu adumu kwenye kazi hiyo cha kwanza ni mazingira bora ya kuishi! Sasa mtoa mada anataka kuturudisha nyuma. Tuwape motisha walimu jamani angalau basi kwa kuwapa makazi bora. Tukumbuke waalimu wanasomea na masomo mengine. Tukumbuke wanasome management kama tusipowamotivate watakimbila kazi nyingine watoto wetu wakose walimu.
 
Lakini ni jambo ambalo haliwezekani kumjengea kila Mwalimu wa nchi nyumba ya kuishi Serikali haiwezi kufanya hilo wataongea tu kila siku lakini Kiuchumi hilo haliwezekani, chukulia tu kwa mfano kwa sasa hivi Tanzania kuna mwalimu mmoja kwa kila watoto 100 kwa hali ya kawaida inapaswa kuwa mwalimu mmoja kwa watoto 40 sasa kama kila mwalimu tutakayeongeza huko mbele ya safari ni lazima ajengewe nyumba hiyo fedha itatoka wapi? hapo hapo tunahitaji watoto wetu wale chakula cha mchana shuleni, wanahitaji madaftari, vitabu, na madawati na vitu vingine muhimu kwao sasa hiyo fedha itatoka wapi?

Na usisahau kuwa siku zote bajeti za Elimu hupangwa kiasi ambacho Serikali husika hutumia kwa kila mtoto wa shule na SIYO Mwalimu, kwa kawaida Mwalimu ni mwajiriwa na anapaswa ajitegemee na ataishi wapi haipaswi kuwa kazi ya Serikali, Serikali inapaswa imlipe fedha za kumtosha kuishi ( Na hii ni kwa Waajiriwa wote na sio walimu tu) ili ajitegemee sasa kujenga nyumba ni kuongeza gharama kwa maan ni lazima pia serikali hiyo hiyo ilipe umeme luku kwenye hizo nyumba, ilipe maji, ikarabati zikiharibika n.k sasa hiyo fedha ni kwa nini tusiwekeze kwa watoto wa shule?

Lakini kusema kwamba kila Mwalimu ajengewe nyumba ya kuishi siyo ukweli na hilo haliwezekani, kama Serikali imeshindwa kuwajengea nyumba Viongozi wakubwa ambao ni wachache itawezaje kuwajengea kila mwalimu hapa nchini?

sorry
ninaomba kufahamu
1. elimu yako na
2. kazi yako kama hutajali tafadhali!!!
 
Wewe usijifanye kujua wakati hujui chochote zaidi ya kusoma na kuandika tu! hizi falsafa zako za kitoto wapelekee watoto wenzio wa mitaani. Wewe sio "moderator" wa JF, huna mamlaka ya kumuamru mtoto yeyote hapa jukwaani. Kaa pembeni uwe msomaji tu kwani huwezi kuchangia chochote cha maana kwa elimu yako duni!
Hongera... ila matusi ni alama nzuri sana ya kuishiwa hoja
 
Hoja yako ilikuwa na msingi ila umeiharibu haswa baada ya kusema kwanini mwalimu anajengewa nyumba. Ungeweza kuitofautisha nyumba za walimu na kuendeleaza mashule na Elimu. Waalim lazima wajengewe nyumba ni kwakuwa haujatembea na kuona wilaya na mashule yalivyo haswa kwa sehemu za vijijini nadhani usingeleta hii hoja ungebadilisha. Cha msingi ni pesa unazotaka ziboreshe mashule na elimu zipatikane nazo.
 
Mleta una kiwango cha juu cha ujinga unashindwa kuhoji mawaziri wanapewa nyumba na serikali unahoji walimu kujengewa nyumbani hivi ulishatembelea vijijini ukaona mazingira yalivyo magumu kama hakuna nyumba mwalimu atakaa wapi?
 
Haujanielewa tatizo ni kwamba Uwezo wa kujenga nyumba serikali HAINA!
Watasema wanavyotaka, watakupeni ahadi wanavyotaka lkn mwisho wa siku UWEZO huo haupo, hiyo Bajeti wataitowa wapi? watabania wapi ili waweze kujenga nyumba za walimu na kuziendesha? [/B]

Wewe ndo unaisemea serikali nani amekwambia uwezo huo haina ficha upumbavu wako.
 
Popote Duniani? Nitajie Nchi moja ambayo Serikali inawajengea wananchi wake nyumba za kuishi!


South Africa Mkuu,nyumba wanazoishi Raia wa kule asilimia karibia 90 ni mali ya Serikali,wananchi wanalipia kodi kama kawa ya Makazi,ukiona mtu binafsi anamiliki nyumba kule ujue huyo atakuwa na kipato kizuri sana,hiyo hali ipo pia karibia kwa nchi zote zilizoendelea,na zenyewe pia nyumba nyingi wanazoishi Raia wao wa kawaida ni za Serikali
 
we mbulula kama unaona wivu walimu kujengewa nyumba za kuishi na serikali kale limao.
 
Hamna cha mkurugenzi wa madini wala balozi.jamaa ni mbumbumbu tu aelewi
 
umeanza vizuri ila umemaliza vibaya,ulikuwasahihi kusema wabunge na mawaziri wanalipwa vizuri lkn kugeneralize kuwa watumishi wengine wa serikali wanalipwa vizuri kuliko walimu na Madaktari hauko sahihi labda tutajie n watumishi wapi hao maana ninachokijua mimi serikalini wote wanalia njaa tu, hakuna cha house allowance wala nini labda kwa wakuu wa idara tu
Alaa kumbe unajua kuna wakuu wa Idara wanaolipwa vizuri hawa sio watumishi au?.
 
Nafikiri haujanielewa sijasema ya kwamba Walimu wanalipwa vizuri bali nilichosema ni kwamba swala kuwajengea nyumba walimu Tanzania kiuchumi ni kwamba haliwezekani tutabaki kudanganyana kila siku na siku zinaenda lakini kiuhalisia halitekelezeki hivyo ni bora kwanza kuukubali huo ukweli na kuwalipa walimu Mishahara ya kuweza kuishi ili wajitegemee lkn kusema kila mmoja ajengewe nyumba huko ni kujidanganya Serikali haina huo uwezo na haitakuja kuwa nao kwa miaka 50 ijayo!

Kwa staili ya serikali hii,inawezekana kabisa,watawakamua wananchi kama walivyofanya wakati wa ujenzi wa shule za kata,na sasa maabara!!
 
Mantiki ya hoja yangu ni kwamba ni kwa nini serikali inapoteza fedha kufanya jambo ambalo kiuhalisia haliwezekani? Yaani kumjengea kila Mwalimu nyumba ya kuishi hizi ni ndoto na Serikali haina huo uwezo hivyo ni kwanini kwa kuwa Mwalimu analipwa mshahara kama mwajiriwa mwingine yoyote yule wa Serikali asijitegmee kwenye makazi?
Yaani Mwalimu ataishi wapi isiwe tatizo la Serikali bali liwe tatizo binafsi la Mwalimu mwenyewe kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine kama manesi, na wengineo ambao wanalipwa mishahara na kupanga chumba!
Tafakari mantiki yako sawasawa. Nyumba za walimu ni nyenzo katika kutoa huduma ya elimu.
ni kama magari kwa watumishi wanaohitaji magari. ni kama computers kwa wale wanaofanya kazi kwa computers
ni kama mashine zote za hospitali kwa ajili ya madaktari n.k.
Swali lako nia kama kuhoji ni kwa nini maafisa wakuu wananunuliwa magari badala ya kununua ya kwao kama watumishi wengine.Na zidi hizo nyuma nia za serikali lakini wanaishi walimu
 
Back
Top Bottom