Yusuph Wernery
JF-Expert Member
- Oct 2, 2013
- 316
- 147
Kweli elimu inahitajika sijawahi sikia mwl kajengewa nyumba......!
Hujui mengi sana ndugu na unaonekana hujawahi Fanya kazi serikali ni tambua kuwa hata mawaziri wako wanaolipwa vizuri wamejengewa nyumba na serikali yaani kota za mawaziri kule msasani then watumishi wengine mfano mdogo askari wanalipwa Pesa za kodi ya nyumba hata kama watakuwa wanaishi kwenye nyumba zao mfano baba yangu mm anaishi kwenye nyumba yake ila Pesa anayolipwa tu ya nyumba ni zaidi za mshahara Wangu hapo unasemaje? Walimu nchi hii wanaonewa sawa mfano MWL anayeanza kazi ngazi ya Cheri mshahara wake haufiki 380,000/= na akiupata huo hakuna tenaa atakachokipata hadi mwezi mwingine sasa jiulize kwa mshahara huo hata akikopa Pesa bank wala hawezi kudhidi million 3
Hizo hesabu unazipigaje? kumbuka tuna shule za watu binafsi nao wana mipango yao ya kukulipa walimu, labda ungenambia katika kila shule za serikali, shule moja inahitaji walimu wangapi na nyumba hizo tuna uwezo kiasi gani maana kugharamia mara moja kunaepusha gharama nyingi za kila siku. Kesho mtatazama vitabu na vifaa vya elimu badala ya kuendelea kulipa mishahara mikubwa inayoondoa uwezo wa kugharamia mambo mengine.
Hata wewe mwenyewe unaponunua nyumba unatazama sababu hizo hizo kwa maisha yako ya mbele laa sivyo ungeendelea kuishi nyumba ya kupanga na unaponunua hutazami ndugu ama watoto wako kuwa unahitaji nyumba ngapi kuwatosheleza..Jiulize kwa nini wewe unajenga nyumba badala ya kupanga ili uwe na fedha za ziada kuwasomesha watoto shule za gharama?.
Mkuu hajengewi nyumba kila mwalimu bali kila shule inakuwa na nyumba za walimu kulingana na mahitaji ya shule hiyo. Mwalimu anaweza kuwepo hapo kwa mwaka akaondoka anaingia mwalimu mwingine. Nyumba moja wameingia walimu wawili kwa mwaka.Nafikiri haujanielewa sijasema ya kwamba Walimu wanalipwa vizuri bali nilichosema ni kwamba swala kuwajengea nyumba walimu Tanzania kiuchumi ni kwamba haliwezekani tutabaki kudanganyana kila siku na siku zinaenda lakini kiuhalisia halitekelezeki hivyo ni bora kwanza kuukubali huo ukweli na kuwalipa walimu Mishahara ya kuweza kuishi ili wajitegemee lkn kusema kila mmoja ajengewe nyumba huko ni kujidanganya Serikali haina huo uwezo na haitakuja kuwa nao kwa miaka 50 ijayo!
wewe ndiyo kichaa. watalipwaje night na hawafanyi kazi usiku? watalipwaje posho na hawana safari wala smina?. kubeba kazi nyumbani ni uvivu wao. masaa 8 kwa siku yanatosha kusahisha, kuandaa somo, lesson plan, scheme of work, kuchapa na kufundisha.We Unakichaa, Umejiuliza Kwanini Waalimu Hawalipwi POSHO WALA NIGHT NA WAFANYAKAZI WENGINE WANALIPWA WAKATI KAZI WANAZOZIFANYA HADI KULIPWA POSHO WANALIPWA MSHAHARA? Kwanini Hizo Posho Zisiende Kwenye Ujenzi Wa Barabara Vijijini? Umewahi Kujiuliza Mwalimu Wa Digrii Anapoanza Kazi Analipwa Laki Sita Na Daktari Anaeanza Kazi Mwenye Digrii Hy Hy Analipwa Milioni Moja Na Laki Tano? Kwanini Na Wao Walipwe Pesa Zote Hz?Kwanini Wasilipwe Viwango Sawa Na Waalimu? FICHA UJINGA WAKO.
Ubunge.na UraisUnaweza ukanitajia kazi rahisi..??
Shida kuna watu toka wazaliwe hawajui shida humu. Nafikiri mtoa mada hajui vizuri mazingira halisi ya mwalimu. Toka azaliwe "baba mkurugenzi wa madini kanda ya .., mama barozi wa tanzania . "Mtu kama huyu hawezi jua shida inayompata mwalimu wa kitanzania anayefundisha Kantalampa, namanyele, Tanganyika masgati, kibungo juu, na lindi vijijini.Nafikiri haujanielewa sijasema ya kwamba Walimu wanalipwa vizuri bali nilichosema ni kwamba swala kuwajengea nyumba walimu Tanzania kiuchumi ni kwamba haliwezekani tutabaki kudanganyana kila siku na siku zinaenda lakini kiuhalisia halitekelezeki hivyo ni bora kwanza kuukubali huo ukweli na kuwalipa walimu Mishahara ya kuweza kuishi ili wajitegemee lkn kusema kila mmoja ajengewe nyumba huko ni kujidanganya Serikali haina huo uwezo na haitakuja kuwa nao kwa miaka 50 ijayo!
Shida kuna watu toka wazaliwe hawajui shida humu. Nafikiri mtoa mada hajui vizuri mazingira halisi ya mwalimu. Toka azaliwe "baba mkurugenzi wa madini kanda ya……….., mama barozi wa tanzania………. "Mtu kama huyu hawezi jua shida inayompata mwalimu wa kitanzania anayefundisha Kantalampa, namanyele, Tanganyika masgati, kibungo juu, na lindi vijijini.
Unapokosa la kuongea jf tulia comment za wenzako f.ala we.
Nani alikudanganya kuwa ukichanganya lugha utaeleweka au utaonekana kama msomi? Hovyo kabisa! hayo ndio madhara ya elimu duni mliyookoteza katika shule za kata.How you present your strong opinion.. destroys maana nzima iliyobeba ujumbe wako...
Kwanza mtoa mada hayuko sawasawa kichwani, katika kazi inayo ongoza kwa kuhamiswa ni Uwalimu, sasa kila Mwalimu ahamishiwapo ajenge? Ningekuona unaakili kama ungeshauri serikali ijenge nyumba za kutosha ili iwapangishe Walimu lwa bei nafuu.
Popote duniani serikali hujenga nyumba na kuwauzia/kodishia wananchi kwa gharama nafuu ili kuwakwamua kiuchumi.
Na kwa kawaida kuna pa kuanzia. Inaweza kuanzia kwa walimu, wanajeshi, nk.
Mkuu nadhani wewe ndio huelewi maaa tumekwambia serikali inajenga SHULE na moja ya majengo yake ni pamoja na nyumba za walimu, hawatazami tuna walimu wangapi bali shule inahitaji walimu wangapi. Mbona Jeshi lina nyumba za wanajeshi? serikali na mawaziri wake hata nchi za magharibi wana nyumba zao?Haujanielewa tatizo ni kwamba Uwezo wa kujenga nyumba serikali HAINA!
Watasema wanavyotaka, watakupeni ahadi wanavyotaka lkn mwisho wa siku UWEZO huo haupo, hiyo Bajeti wataitowa wapi? watabania wapi ili waweze kujenga nyumba za walimu na kuziendesha?
Kumbuka Bajeti ya Elimu haina Nyumba za Walimu hivyo ni lazima hilo fungu litoke mahali sasa ni wapi?
Ni wapi ktk nchi yetu ambako kunafaa au kunastahili kukatwa bajeti yake ili kujengwa nyumba za Walimu? Unaweza kuniambia?
Na isitoshe nilichosema ni kwamba swala Mwalimu atakaa wapi halipaswi kuwa la Mwajili bali la Mwalimu mwenyewe alipwe Mshahara wa kumtosha kuishi halafu atakapoishi atajua mwenyewe ila cha muhimu muda wa kazi awepo atalala wapi haipaswi kuwa tatizo la Serikali kama walivyo wengine!