Kwanini Serikali inawajengea nyumba walimu?

Kwanini Serikali inawajengea nyumba walimu?

Sio lazima mpaka nawe utoe hoja hili tukujuwe .tutakujuwa tu atakama ukichangia hoja babu
 
Huko vijijini hata nyumba za kupanga hamna. Zilizopo hazina staha kwa walimu.
 
Mkuu nadhani wewe ndio huelewi maaa tumekwambia serikali inajenga SHULE na moja ya majengo yake ni pamoja na nyumba za walimu, hawatazami tuna walimu wangapi bali shule inahitaji walimu wangapi. Mbona Jeshi lina nyumba za wanajeshi? serikali na mawaziri wake hata nchi za magharibi wana nyumba zao?

Na kama unaamini serikali haina uwezo wa kujenga nyumba hizo, mbona unailalamikia serikali kujenga nyumba za walimu kwani wameshindwa kuzijenga? Hilo fungu unalozungumzia wewe ni la mwaka ule nyumba inajengwa baada ya hapo kuna fedha zinabakia kuweza timiza mengine sema tu serikali yetu inavipa vipaumbele vitu vingine wanaacha ELIMU. Fedha ya serikali inatokana na kodi yako kila mwaka hivyo sio mtaji unaokwisha.

Sababu ni kwamba Serikali haina uwezo wa kuzijenga na kuzihudumia hizo nyumba na tunaweza tukapiga hesabu rahisi tu, tuchukulie shule moja ya Msingi ina wanafunzi yenye darasa la kwanza mpaka la saba kwa kila darasa kuna watoto 100 mara 7 ni watoto 700 sasa shule hii itahitaji kama walimu 30 hivi sasa kama Serikali inabidi kumjengea au kumpa kila Mwalimu sehemu ya kukaa na hawa walimu wana familia zao familia moja ya Kitz ina watoto wanne hivyo 30 *4 = 120 ina maana kwa hii shule moja serikali ijenge nyumba ya kuhudumia watu 120 na hii ni shule moja tu tena ya msingi bado kuna walimu wa sekondari na kidato cha tano na sita pia wanakuja na kila siku watoto wenye mahitaji ya kusoma yanaongeza na hivyo walimu pia sasa kwa Tanzania nzima utaona ya kwamba hii ni gharama kubwa sana Serikali HAIWEZI kuilipia bila kunyima sehemu nyingine sasa ni sehemu gani hiyo?

Yaani Serikali itatowa wapi fedha? Angalia tu kwa mfano Shule nyingi za Kata zilizojengwa nchini kote hazikujengwa kwa sababu ya bajeti ya serikali tu bali ziliweza kujengwa kwa sababu Wahisani waliifutia serikali madeni na hivyo kuiambia serikali badala ya kulipa deni ijenge shule lkn kama wahisani wasingesema hivyo na kusamehe deni ina maana hizi shule zisingejengwa, sasa swali linabaki hizo fedha za kujenga Nyumba za walimu zitatoka wapi kama hata za kujenga shule tulipewa? Kwa maana nyingine ni kwamba Serikali yetu kwa kifupi haiwezi kujenga Shule za watoto wetu kwa maana hizi za kata ni za Msaada, sasa fedha za kujenga na nyumba za Walimu zitatoka wapi? ndio swali langu!
 
Imekuwa tena kesi: Italy, Ujerumani, Ufaransa, nk.

Siyo kweli hizo nchi zote ulizozitaja hakuna moja inayowajengea walimu wake nyumba bali walimu wanalipwa mishahara kama Wafanyakazi wengine na wanajitegemea mahali pa kuishi!
 
Siyo kweli hizo nchi zote ulizozitaja hakuna moja inayowajengea walimu wake nyumba bali walimu wanalipwa mishahara kama Wafanyakazi wengine na wanajitegemea mahali pa kuishi!
Endelea kubisha, umeomba mifano ya nini? Sijakuambia walimu tu, ila nimekuambia wananchi wake kwa awamu. Inaweza kuanzia kwa walimu, wanajeshi, au kundi lolote fulani katika jamii. Lakini serikali inajenga nyumba na kuwauzia au kuwapangishia kwa bei nafuu, na inafanya kwa kukata kutoka mshahara wake, wala sio taslimu.
 
HAKI YA MUNGU NCHI HII VICHAA NA MAZEZETA WAPO WENGI!.. Hivi wewe ulizaliwa Asubuhi au Mchana? Ktk Mahospitali kuna nyumba za watumishi (madaktar na manec) Nyumba za Polisi, na baadhi ya watumishi wa serikali hupewa posho kwa ajili ya Nyumba ie, Wanajeshi... Almost 50% ya watumishi wengi wanakua accomodated na nyumba za serikali na sio lazima ziwe ktk Sehem ya Kazi... ACHAA KULA MAHARAGE YA MBEYA UPUNGUZE KUROPOKA,,, pia Hakikisha unalala mapema kila siku ili ukue sawa Binti!
 
Endelea kubisha, umeomba mifano ya nini? Sijakuambia walimu tu, ila nimekuambia wananchi wake kwa awamu. Inaweza kuanzia kwa walimu, wanajeshi, au kundi lolote fulani katika jamii. Lakini serikali inajenga nyumba na kuwauzia au kuwapangishia kwa bei nafuu, na inafanya kwa kukata kutoka mshahara wake, wala sio taslimu.

Siyo kweli hizo nchi hazijengi Nyumba kwa wananchi wake bali nyumba hujengwa na makampuni binafsi na wananchi huchukua mikopo benki na kununua nyumba, isipokuwa kuna nyumba chache kama sisi ilivyo kwa msajili hapo zamani ambapo Serikali inamiliki lkn ni kwa Watu masikini tu ndio wanaruhusiwa kuishi kwenye hizo nyumba na haziuzwi lkn wengine wote kuanzia walimu, manesi n. wanajichanganya kama raia wa kawaida na hupanga au kununua nyumba kibinafsi!
 
Sababu ni kwamba Serikali haina uwezo wa kuzijenga na kuzihudumia hizo nyumba na tunaweza tukapiga hesabu rahisi tu, tuchukulie shule moja ya Msingi ina wanafunzi yenye darasa la kwanza mpaka la saba kwa kila darasa kuna watoto 100 mara 7 ni watoto 700 sasa shule hii itahitaji kama walimu 30 hivi sasa kama Serikali inabidi kumjengea au kumpa kila Mwalimu sehemu ya kukaa na hawa walimu wana familia zao familia moja ya Kitz ina watoto wanne hivyo 30 *4 = 120 ina maana kwa hii shule moja serikali ijenge nyumba ya kuhudumia watu 120 na hii ni shule moja tu tena ya msingi bado kuna walimu wa sekondari na kidato cha tano na sita pia wanakuja na kila siku watoto wenye mahitaji ya kusoma yanaongeza na hivyo walimu pia sasa kwa Tanzania nzima utaona ya kwamba hii ni gharama kubwa sana Serikali HAIWEZI kuilipia bila kunyima sehemu nyingine sasa ni sehemu gani hiyo?

Yaani Serikali itatowa wapi fedha? Angalia tu kwa mfano Shule nyingi za kata zilizojengwa nchini kote hazikujengwa kwa sababu ya bajeti ya serikali tu bali ziweza kujengwa kwa sababu Wahisani waliifutia serikali madeni na hivyo kuiambia serikali badala ya kulipa deni ijenge shule lkn kama wahisani wasingesema hivyo na kusamehe deni ina maan hizi shule zisingejengwa, sasa swali linabaki hizo fedha za kujenga Nyumba za walimu zitatoka wapi kama hata za kujenga shule tulipewa?
Mshikaji kinachohesabiwa hapa ni nyumba za walimu 30 haitazami mwalimu na watoto wake maana sii wakazi wa kudumu. Tuseme serikali inajenga nyumba za walimu za chumba kimoja, viwili, vitatu na vinne ambazo zina gharama ya wastani ya Tsh mil. 600 zote 30 ni jumla ya Tsh. bil.18 gharama ya mara moja. Hii ni miundombinu yaani vitu vya kudumu kama vile serikali inapojenga bomba la maji kwa gharama kubwa kuwahudumia watu mil. 1 badala ya kuwagawia wananchi ndoo za maji mil 1 wakateke maji wenyewe ziwani.

Kwa fikra za kawaida utaona hakuna umuhimu wa bomba za maji ikiwa kuna ziwa karibu..
 
Ok... Na kwa nini wanajeshi wananunua vitu kwa bei rahisi wakati nao wanalipwa mshahara kama wengine..?? Na kwa nini wawe na maduka yao makambini..??

Swali litabaki kuwa la kijinga kama tu halitaulizwa..

umesahau nauli hawalipi pia
 
Hata mie sishauri serikali kujenga nyumba kwa baadhi ya walimu kwa sababu haileti haki,kuna shule zina nyumba na kuna shule hazina nyumba.Ninachoshauri wote wapewe housing Allowance ili kubalance.

Cha msingi sanaa hiyoo wanawadanganya tuu walimu ni wengi mnoo kwani kuwajengea wote haitowezekana wapewe tuu kwa ajili ya nyumba kwa wale wasio na nyumbaa
 
Siyo kweli hizo nchi zote ulizozitaja hakuna moja inayowajengea walimu wake nyumba bali walimu wanalipwa mishahara kama Wafanyakazi wengine na wanajitegemea mahali pa kuishi!
Wewe unabisha kitu usichokijua! . Shule ni pamoja na nyumba za walimu za kuishi. Hivyo unaposema kuwa ''hutaki serikali ijenge nyumba za walimu'' ni sawa na kusema hutaki serikali ijenge shule! Kuna sehemu kama vijijini kwa mfano ambapo hakuna nyumba za kupanga karibu na shule! Walimu wa shule hizi watalala wapi? Usi-set mawazo yako Dar tu. Tembea uone!
 
Siyo kweli hizo nchi hazijengi Nyumba kwa wananchi wake bali nyumba hujengwa na makampuni binafsi na wananchi huchukua mikopo benki na kununua nyumba, isipokuwa kuna nyumba chache kama sisi ilivyo kwa msajili hapo zamani ambapo Serikali inamiliki lkn ni kwa Watu masikini tu ndio wanaruhusiwa kuishi kwenye hizo nyumba na haziuzwi lkn wengine wote kuanzia walimu, manesi n. wanajichanganya kama raia wa kawaida na hupanga au kununua nyumba kibinafsi!

mkuu mwisho tutakutukana umeambiwa kada nyingine wanapewa house allowance ila mwalimu hapewi hiyo allowance pia umeambiwa waalimu wanahama mara kwa mara sasa unataka uniambie kila anakohamia ajenge nyumba usisahau hata nyumba wanazojengewa hazina hadhi ya mwalimu kuishi.
kuhusu nchi ambayo serikali inawajengea walimu wao nyumba miye nimeshuhudia zambia tena kule kila mwalimu ana nyumba yenye service zote
 
Walimu wanalipwa mshahara mdogo sana.......wanaishi kwa kuungaunga tu.....hakuna posho wala allowance yoyote....anategemea mshahara 100%...hakuna night wala safari ya kikazi.....ni chaki mwanzo mwisho.......Ualimu ni issue asikwambie mtu
 
Siyo kweli hizo nchi hazijengi Nyumba kwa wananchi wake bali nyumba hujengwa na makampuni binafsi na wananchi huchukua mikopo benki na kununua nyumba, isipokuwa kuna nyumba chache kama sisi ilivyo kwa msajili hapo zamani ambapo Serikali inamiliki lkn ni kwa Watu masikini tu ndio wanaruhusiwa kuishi kwenye hizo nyumba na haziuzwi lkn wengine wote kuanzia walimu, manesi n. wanajichanganya kama raia wa kawaida na hupanga au kununua nyumba kibinafsi!
Mkuu nyumba za serikali hata nchi za magharibi ni kwa wenye kipato cha chini sio maskini. maskini wana nyumba zao zikiitwa Shelters ambazo hutunzwa kama wasojiweza. Wao ndio waloanzisha mpango wa ujenzi wa shule za walimu makwao walipoanza kujenga mfumo wa elimu zao na kuboresha hali za wananchi wake. Sisi hapa hatujafika robo ya maendeleo yao ktk sekta hiyo, mtoto anayetambaa huwezi kulazimisha atembee kwa sababu wa jirani anatembea..

Ujenzi wa nyumba kwa serikali una lengo na mara zote ni kutosheleza mahitaji ya mkakati husika ikiwa ni ELIMU basi jambo bora kwanza ni kuwa na shule walimu na makazi ya walimu kisha ndio vifaa vya kufundishia ambalo ni jambo la kila siku daily expenses hivyo panakuwa na invetory turnover.

Huwezi kupinga ujenzi wa nyumba za walimu wakati kuna vijiji ambavyo hata nyumba za kupangisha hakuna, ama shule zipo kijijini kabisa mbali na mji, hapo hujazungumzia adha ya usafiri na kadhalika. Unapolitazama swala la ELIMU usichukulie tu mambo unayoyaona kufaa wakati jambo moja linaweza haribu kabisa mpango mzima. Sio shule zote ziko mijini tena naweza sema tuna shule nyingi vijijini kuliko mijini, hivyo tazama swala hili kwa mapana zaidi.
 
Sasa huu ndio wivu wa kike hehehe. Haya mambo ya unazaliwa magomeni halafu ajira gongo la mboto kwenye kiwanda cha nguo cha sungura. Unahisi kama kuna vyumba vya kupanga vya elfu kumi na tano. Mtu kaajiriwa nsyuka huko anajengaje nyumba?
 
Kwanza hili sio jukwaa la mada kama hiyo.kutupia thread hiyo humu kunanithibitishia kuwa wewe ni mkurupukaji yani hufanyi mambo bila kufikiri.hoja yako pia inaudhaifu mkubwa wa kuandika bila kufikiri au kujiuliza.polis je? jwtz je?
 
Back
Top Bottom