Kwanini Prof. Baregu amenyimwa kazi UDSM?

Kwanini Prof. Baregu amenyimwa kazi UDSM?

C'mon mkuu,maandamano ya nini tena??,kwa sababu tu Baregu kakataliwa kuongezewa mkataba!!!!,lol,binafsi namshauri Baregu aangalie tu ustaarabu mwingine maana sidhani kama atakaa UDSM daima(kama kufundisha anaweza kufundisha hata kwenye vyuo vingine so sioni sababu ya yeye kung'ang'ania kuendelea kuwepo UDSM)

Kwa mujibu wa Waziri Ghasia:- "Kwa kutumia utaratibu huu, Baregu alistaafu kazi kwa mujibu wa sheria Februari 24 mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka 55 na baada ya kustaafu, aliajiriwa kwa mkataba na UDSM mara tatu na mkataba wa mwisho ulimalizika Januari mwaka 2008," alisema Ghasia....Prof Baregu keshaongezewa mkataba mara tatu sasa,mi namshauri kama vp atafute tu sehemu nyingine(chuo) maana siku hizi vyo viko vingi tu(na vingi vina matawi Dar),kuna life baada ya UDSM....Kimsingi mtu unapoomba kitu(kama kuongezewa mkataba) kuna mawili kukubaliwa ama kukataliwa,inabidi ujiandae kupata jibu la Yes ama No

he kumbe baregu kibabu namna hii? kikapumzike sasa. hongere mh. ghasia. hivi vibabu visipopumzika siye makinda tukimaliza skuli tutafanya kazi wapi? udsm kunono ati, lakini, wakati ukuta ng'atuka sasa mzee kwa heshima bila kulalamika. miaka 70+!!!!!!!!!!!!!!!!! bado unaalilia ajira!

ghasia oyeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!! maisha bora kwa kila kinda hayoooooooooooooooo!
 
Mkuu,
Hili swala si jepesi kama unavyotaka kulifanya wewe.

Nafikiri tatizo hapa si BEREGU. Angelikuwa Beregu ni tatizo basi tungelisema kuwa Tanzania au UDSM bila Beregu hakiwezi kuwa na hilo si kweli.

Hapa tatizo ni lazima tufahamu MISINGI ikoje ya WANYAKAZI WA UMMA. Kesho watapindisha mistari ili kufanikisha mambo yao jambo ambalo mtu wa kawaida anaweza kuliona si muhimu sana.

Mwisho nafikiri NIMSHUKURU Baregu kwa kukomaa nao hadi kieleweke. Ningelishauri Baregu apigane hadi ashinde na akishinda adai iwekwe wazi kwenye sheria. Kama atashindwa basi tufahamu ni Wafanyakazi gani wa umma kisheria hawawezi kuwa WANASIASA. Tukishapata hapo, tutaanza sasa kulia na hao wa CCM walioko kwenye utumishi wa UMMA. Na Mwisho kabisa kwangu mie ni kuwa Baregu hata kama ukishinda basi na UDSM usirudi ili wenye Madonge yao wajinyonge. Ila hii itakuwa imeweka njia kwa wafanyakazi wengine wa umma wanaotaka kugombea basi na wafanye hivyo bila woga na au wasifanye hivyo.
Sikonge,

nakubaliana na wewe, suala si jepesi kabisa!!

Ila mtazamo wangu ni kwamba, kwa taratibu na siasa dhalimu kama za Tanzania the two wrongs wont make it right!! Yes, Baregu ana rights zake na anakomaa kuambana... very good

... lakini tunasau kitu muhimu sana hapa umri, angekuwa ana 45 mimi ningebeba bango lakini alishatumikia taifa na kupewa mkono, na mkono, na mkono, na mkono!!!a good system inaandaa watu wakurithi

Hapo ndipo ninapopinga mimi!!!

Kwenye kuchanganya siasa na utumishi wa umma, hilo ni jingine kabisa kwani angebaki tungenyamaza... remembr two wrongs wont make it right, sio kwasababu CCM wanakosea kuwekana madarakani kinyume na taratibu za utumishi wa Umma basi na wengine wawepo... kwani utakuwa unabariki kosa kwasababu wote tumekosea (ni kama vile mke akitoka nje basi na wewe utoke)

NAUNGA MKONO HOJA YA KUPATA LIST YA WANASIASA [BILA KUJALI CHAMA KWANI WAPO HATA VYAMA VINGINE KWENYE UTUMISHI] WALIO KWENYE UTUMISHI NA TUWAOMBE WAONDOKE TUPATE HIZO AJIRA NA SIE AKINA KAJAMBANANI!!!
 
he kumbe baregu kibabu namna hii? kikapumzike sasa. hongere mh. ghasia. hivi vibabu visipopumzika siye makinda tukimaliza skuli tutafanya kazi wapi? udsm kunono ati, lakini, wakati ukuta ng'atuka sasa mzee kwa heshima bila kulalamika. miaka 70+!!!!!!!!!!!!!!!!! bado unaalilia ajira!

ghasia oyeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!! maisha bora kwa kila kinda hayoooooooooooooooo!

Dogo una matatizo makubwa sana!!!
 
Kuna mchango nilioutoa leo asubuhi kutofautisha kati ya watumishi wa umma na wanasiasa naona imeondolewa sijui kwa nini. Kaaya yes anazo sifa kama za Baregu kwa maana hiyo ni muhimu Ghasia afafanue. Japokuwa Baregu hastahili kuendelea kuwa mtumishi wa umma kwa sababu ameishastaafu wakati Kaaya bado ni kijana. Kwani Naregu kuwa mjumbe wa CC Chadema ndiyo kumesababisha asiajiriwe au uzee? Kama ndiyo aliyoyasema Ghasia basi kachemsha.

By definition watumishi wa umma yaani Public Service as opposed to politicians ni kuanzia Chief Secretary hadi mhudumu wa ofisi. Hao ni permanent and pensionable. Wakati Rais, VP, PM, Mawaziri, MaRcs, MaDCs. Hawa ni political leaders and they are not pensionable but are paid gratuities. Kwa hiyo Membe na Rugimbana are not public civil servants. No. Ila Kaaya is kwa sababu he is governed by the Public Service Act.

Nashukuru sana mkuu... hebu urudie tu huo mchango kwa faida ya wote!!! JF ni nzuri sana kwa kutoa two sides of the story na siamini kama wameutoa..
 
Benard Membe- Waziri wa Mambo ya Nje; Mjumbe wa NEC na Katibu wa CCM wa idara(huyu ni mtumishi kabisa wa chama kwa nafasi yake ya ujumbe wa sekretariati ya CCM)

Nimetaja Membe kama mfano tu, lakini wapo wengine wengi tu wakina Chiligati, Mkuchika nk.

JJ

Mnyika:
Tafadhali usichanganye mambo. Wewe ni mwansiasa unajua fika kuwa vyeo vya ukuu wa wilaya, mkoa, uwaziri ni vya kisiasa. Ni dhahiri mtu kama membe, chiligati, mkuchika na mkuu wa wilaya ya kinondoni hawa ni wanasiasa na vyeo vyao ni vya kisiasa. Watu kama makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi n.k ni watu wasiopaswa kuwa wanasiasa.

Naomba wana JF mjue hilo.
 
he kumbe baregu kibabu namna hii? kikapumzike sasa. hongere mh. ghasia. hivi vibabu visipopumzika siye makinda tukimaliza skuli tutafanya kazi wapi? udsm kunono ati, lakini, wakati ukuta ng'atuka sasa mzee kwa heshima bila kulalamika. miaka 70+!!!!!!!!!!!!!!!!! bado unaalilia ajira!

ghasia oyeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!! maisha bora kwa kila kinda hayoooooooooooooooo!

Ninavyofahamu mie ni kuwa UDSM na UDOM kuna nafasi za kazi wanatangaza. Kijana kama wewe ni Professor au hata una Phd kama aliyonayo Baregu basi kachamkie kazi hiyo iko wazi maana nasikia hadi masomo yake wameyaondoa pale UDSM ili isije ikaonekana pengo la Baregu ni kubwa.

Pili ni kuwa yeye kuajiriwa kwake ni kwa mkataba. Mwaka huu alikuwa kaomba wa mwaka mmoja. Jamani kama mtu anaona bado ana nguvu, na nafasi yake ipo wazi kwa nini mumuondoe? Wengine wakifikisha miaka 80 ndiyo wanaenda kufunga ndoa na wewe unamuita kibabu. Hebu mpeleke Mkeo au mpenzi wako kwa huyu Kibabu uone kazi. Na kama wewe ni mwanamke, nenda kahakikishe UBABU wa huyu mzee. Vinginevyo hizo unazosema ni namba tu na si ubabu.
 
jamani kishapewa mikataba mitatu hamshukuru, kunyimwa mmoja ndio iwe ishu kwani ilikuwa lazima apewe? yeye nanai kwani? si mtanzania wa kawaida? watanzania wangapi wananyimwa mambo kibao wanalubali yaishe?

tubadilike wajameni, umri ukifika pazuri kubali kustaafu, usisubiri upigwe mawe!

mi naona anajidhalilisha kulilia kazi zinazoweza kufanywa na wajukuu zake, apumzike na sie tutese,

huyu ghasia ana visheni kali sana, anafaa kuwa waziri mkuu
 
Mkuu,
Hili swala si jepesi kama unavyotaka kulifanya wewe.

Nafikiri tatizo hapa si BEREGU. Angelikuwa Beregu ni tatizo basi tungelisema kuwa Tanzania au UDSM bila Beregu hakiwezi kuwa na hilo si kweli.

Hapa tatizo ni lazima tufahamu MISINGI ikoje ya WANYAKAZI WA UMMA. Kesho watapindisha mistari ili kufanikisha mambo yao jambo ambalo mtu wa kawaida anaweza kuliona si muhimu sana.

Mwisho nafikiri NIMSHUKURU Baregu kwa kukomaa nao hadi kieleweke. Ningelishauri Baregu apigane hadi ashinde na akishinda adai iwekwe wazi kwenye sheria. Kama atashindwa basi tufahamu ni Wafanyakazi gani wa umma kisheria hawawezi kuwa WANASIASA. Tukishapata hapo, tutaanza sasa kulia na hao wa CCM walioko kwenye utumishi wa UMMA. Na Mwisho kabisa kwangu mie ni kuwa Baregu hata kama ukishinda basi na UDSM usirudi ili wenye Madonge yao wajinyonge. Ila hii itakuwa imeweka njia kwa wafanyakazi wengine wa umma wanaotaka kugombea basi na wafanye hivyo bila woga na au wasifanye hivyo.

Kwakweli you said it well than I could have. Hili jambo ni lamsingi sana kama halitakua personalised. Taking Baregu as a concept and not a personality kuna michanganyiko na matatizo mengi sana yanajitokeza kupitia hii concept ya Baregu.

Kwanza Baregu speaks on behalf of every academician in public university; kwamba kwanini ang'ang'anie kubakia na ajira kwa mkataba hata baada ya umri wake wa ajira kufikia kikomo? Think of how many years he has spent mpaka kufikia hiyo rank and what is he rewarded kama pension na gratuity in comparison to wanasiasa? Je ni Baregu tu ndo ameendelea kutaka ku renew mkataba wa ajira katika public universities. Ni % ngapi ya hao waliostaafu bado wako katika ajira and why? Je kama swala ni kuhusu uhaba wa wanataaluma where was the government until that happened na je forecasting ya human resources in public university inafanywa inavyo takikana? Si hiyo hiyo wizara ya utumishi ndiyo mtuhumiwa mkuu katika hii kesi?

Pili Baregu anawakilisha vile vile wanataaluma wa Tanzania tulionao. Wao kama think tank ya Taifa hili, wamechangiaje katika hili tatizo kutokea na je aliwezaje kuwa persuade wenzake ili hayo yanayompata (ya kung'ang'ania kubaki katika ajira hata baada ya umri kukoma na kama academician atakua upande wa kuipinga serikali ni sheria zipi zitamlinda) yasitokee kwa kuzingatia profession yake katika mambo ya politics na hivyo kwakutumia taaluma yake kushirikiana na wenzake kuishauri vizuri serikali hasa kwa ku avoid comfrotations na kutumia negotiation and lobying skills?

So kwakweli ukiitafakari vizuri utaona hii ni issue ambayo ni muhimu kwa kila mmoja katika Taifa hili katika kurekebisha attitudes na behaviours zetu na hata planning and programming kwa maendeleo ya nchi yetu.

Kuna mengi ya kujifunza kupitia hii concept na tukiwa positive badala ya kuwa negative na kupersonalise hii issue basi ni platform nzuri ya kubadilisha mambo yaendane na wakati ili kusukuma maendeleo na kujenga jamii inayozingatia usawa na demokrasia.
 
jamani kishapewa mikataba mitatu hamshukuru, kunyimwa mmoja ndio iwe ishu kwani ilikuwa lazima apewe? yeye nanai kwani? si mtanzania wa kawaida? watanzania wangapi wananyimwa mambo kibao wanalubali yaishe?

tubadilike wajameni, umri ukifika pazuri kubali kustaafu, usisubiri upigwe mawe!

mi naona anajidhalilisha kulilia kazi zinazoweza kufanywa na wajukuu zake, apumzike na sie tutese,

huyu ghasia ana visheni kali sana, anafaa kuwa waziri mkuu

Tatizo siyo kunyimwa kwa sababu ya UZEE.

Tatizo ni kunyimwa kwa sababu ya KISIASA. Nafasi yake hadi sasa iko wazi na hakuna mtu wa kuziba. Wao badala ya kuendelea naye hadi watakapopata (narudia tena pale watakapopata) mtu wa kuziba hilo pengo lake. Ila wivu wa kisiasa wako tayari wanafunzi wakose mwalimu na masomo yao yafutwe, kisa tu kumkomoa Beregu. Kibaya zaidi ni kuwa Beregu yuko pale zaidi kama msaada kuliko kimaslahi. Kama kazi nzuri nafikiri anaweza kuzipata nyingi tu ndani na nje ya nchi. Sasa hapa kama mtu ana akili zake anaweza kufahamu anachopigania Beregu na Waalimu wa UDSM.

Kuna watu wanaweza maslahi yao ya CHAMA mbele na nchi wanaiweka nyuma. Kibaya zaidi ni pale watu wanakuja na kumsifu huyu Mama Ghasia. Siku wakija kugeuza kibao, nyie wenyewe mtakuwa wa kwanza kulalamika.
 
Tuko pamoja... tatizo kinara wa vita hiyo anaqualify mfumo wa voucher, angekuwa bado yuko kewnye payroll kabla ya kuagwa vita ingekuwa tamu zaidi... ni wangapi hawajaongezewa mikataba jamani??

Lets take personal maters aside... vita anayopigana baregu ni sahihi na takatifu, tatizo ni kwamba yeye hatakiwi kuwa jemedari kwani silaha alizonazo ni mkopo, alishamaliza muda halali

Ah
 
unajua kuna mgongano wa tafsiri hapa,. ndo maana naamini suluhu ya kwanza hapa ni mtu mwenye waraka tajwa ( rejea waraka alioutaja Hawa Ghasia ) atubandikie hapa, ili tuweze kuusoma kwa kina na kisha tuone tunapata tafsiri ipi ya mtumishi asiepaswa kuwa na wadhifa wa kisiasa, ama kushiriki siasa.
bila kuusoma huo waraka kuchangia kwetu ni bure maana tunachangia jambo ambalo hatujawahi kuliona zaidi ya kuhadithiwa.
nitoe wito kama kna mtumishi wa UMMA yeyete miongoni mwetu atuwekee huo waraka ili tuweze kujadili kwa mwelekeo sahihi na bora zaidi.
 
Kwangu mimi swali ni kuwa je bado ana cha kuchangia Chuo Kikuu? Kwa wenzetu kuna vibabu na vibibi ambavyo ni ma Profesa Emeritus na hakuna anayethubutu kuwawazia wastaafu! Swali, jee Profesa Baregu ni kichwa? Kama ndio, wamwache aendelee kuwapa watoto wetu matunda ya fikra zake. Kama anatelezea u-profesa basi ampishe mwingine. Academia hapatakiwi kuwa na siasa. Kinachothaminiwa ni mchango wa mtu katika dunia ya kufikiri!

Amandla......
 
Naona watu wengi wanachangia kwa hisia zaidi bila Kujiuliza maswali ya Msingi

Baregu anapigania nini? Nini madhara kama hii ishu ikaachwa ipite hivi hivi? Leo kwa Baregu jee kesho kwa nani? Kwamba Baregu hawezi kuishi asipokuwa Lecturer?
 
Baregu ni Mwalimu wangu na namheshimu kwa hilo, nafahamu ni jinsi gani alivyogubikwa na uelewa mpana katika masomo aliyokua akifundisha.Kila mmoja aliyepita katika mikono ya mwalimu huyu angependa na wengine wapate wasaa wa kusikia na kupata elimu bora kutoka kwake.

Lakini pamoja na hayo ya ubora wake na pia weledi alionao katika nyanja hii muhimu kabisa ya elimu, nisingependa kuweka ushabiki bila kuangalia sheria inasemaje katika hili. Kama ilivyosemwa hapo kabla, kwa kuwa tu kumefanyika makosa huko nyuma basi tusirudie tena makosa kama hayo kwa vile tu tuna watu kama akina Baregu ambao wako katika siasa na vile vile ni waajiriwa serikalini.

Kitu cha muhimu ni kuona kuwa sheria na iwaguse wale wote ambao wako katika ajira serikalini lakini pia wamo katika siasa kama viongozi n.k.. na hawa kama walivyotajwa hapa kabla ni namna ya akina Mvungi na wenzao. Ninachokisimamia hapa, ni kuwa makosa ya wengine yasiwe sababu ya kumrudisha Baregu kazini, ila hao wengine nao wenye makosa wawajibishwe au kuwe na mabadiliko ya sheria ambayo yataruhusu yale yaliyokatazwa sasa.
 
Tatizo siyo kunyimwa kwa sababu ya UZEE.

Tatizo ni kunyimwa kwa sababu ya KISIASA. Nafasi yake hadi sasa iko wazi na hakuna mtu wa kuziba. Wao badala ya kuendelea naye hadi watakapopata (narudia tena pale watakapopata) mtu wa kuziba hilo pengo lake. Ila wivu wa kisiasa wako tayari wanafunzi wakose mwalimu na masomo yao yafutwe, kisa tu kumkomoa Beregu. Kibaya zaidi ni kuwa Beregu yuko pale zaidi kama msaada kuliko kimaslahi. Kama kazi nzuri nafikiri anaweza kuzipata nyingi tu ndani na nje ya nchi. Sasa hapa kama mtu ana akili zake anaweza kufahamu anachopigania Beregu na Waalimu wa UDSM.

Kuna watu wanaweza maslahi yao ya CHAMA mbele na nchi wanaiweka nyuma. Kibaya zaidi ni pale watu wanakuja na kumsifu huyu Mama Ghasia. Siku wakija kugeuza kibao, nyie wenyewe mtakuwa wa kwanza kulalamika.

nani kakwambia pengo lake halizibiki? la nyerere lilizibwa sembuse la baregu?

hakuna msaada pale angekuwa halipwi unafikiri ungemuona pale? hayo ya chama ni hisia zenu tu wakereketwa. ghasia kafuata misingi ya sheria na haki za binadamu (ajira kwa wote si kwa wakongwe pekee)

hawa ndio wachapakazi tuaotaka!!!!!!!!!!!! big up ghasia!!!!!!
 
Kwa maana nyingine mtumishi wa umma hastaafu mpaka umri wa 55/60/65 lakini political appointee anastaafu mara tu aliyemteua anapoacha kumteua tena.

Mkuu wa Wilaya waweza kaa kwa siku moja au mbili!

Mkurugenzi wa Idara ya XXX huwa anaingia hapa anatokea kule, etc. etc. mpaka umri ufikie kutoka kwenye daftari la ulaji.

Mh. Mnyika mtunga sheria a.k.a Mbunge mtarajiwa anatufanyia mambo ya ajabu kusema vitu ambavyo havina maana kabisa.
 
Benard Membe- Waziri wa Mambo ya Nje; Mjumbe wa NEC na Katibu wa CCM wa idara(huyu ni mtumishi kabisa wa chama kwa nafasi yake ya ujumbe wa sekretariati ya CCM)

Nimetaja Membe kama mfano tu, lakini wapo wengine wengi tu wakina Chiligati, Mkuchika nk.

JJ

Mnyika,

Are you really serious on this issue? Membe atakuwaje civil servant wakati ni mbunge na waziri?

Tusifanye utani kwenye mjadala muhimu kama huu. Badala yake tusaidieni kuleta sheria husika ili tujadili kwa faida ya taifa letu.

Baregu hapa ni victim na sheria mbovu zitawakumba victims wengine wengi. Lakini hata sisi katika kujadili tuache mapenzi ya kisiasa.

Tutoe definition kamili ya civil servant na kisha ndio tuangalie wangapi pia ni viongozi wa siasa?

Hivi kweli mwalimu chuo kikuu anakatazwa kuwa mwanasiasa?

Mbona upinzani kuna watu kama Kitila ni walimu na bado ni viongozi kwenye vyama vyao?
 
Mnyika,

Are you really serious on this issue? Membe atakuwaje civil servant wakati ni mbunge na waziri?

Tutoe definition kamili ya civil servant na kisha ndio tuangalie wangapi pia ni viongozi wa siasa?

Mkuu tupe definition halisi ya Mtumishi wa Umma Tanzania
 
nani kakwambia pengo lake halizibiki? la nyerere lilizibwa sembuse la baregu?

hakuna msaada pale angekuwa halipwi unafikiri ungemuona pale? hayo ya chama ni hisia zenu tu wakereketwa. ghasia kafuata misingi ya sheria na haki za binadamu (ajira kwa wote si kwa wakongwe pekee)

hawa ndio wachapakazi tuaotaka!!!!!!!!!!!! big up ghasia!!!!!!

Hata Membe si inasemekana ni Usalama wa Taifa (wenye habari kamili washushe).

Ngoja na yeye kibao kimgeukie. Mambo ni kama msumeno.

Mwaka huu kitaeleweka tu hapa Tanzania.

Tatizo siyo Baregu hapa. Kama wewe unafikiri hivyo basi akili zako ni finyu kama za kobe.

Mnyika tuwekee hiyo sheria nzima ili tuweze kujadili kwa kutumia reference.

Mwisho ni kuwa mtu anayeajiriwa kwa Mkataba, na huo ni wa muda mfupi (kama wa Baregu ilikuwa uwe wa mwaka mmoja), sheria na miiko yake ikoje? Maana mie nafikiri kuajiriwa kwa mkataba si kama kuajiriwa permanent.
 
Back
Top Bottom