Suala la Prof. Beregu, limeibukia Bungeni Dodoma leo asubuhi katika kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Viti maalum Chadema, Bi. Halima Mdee, alimuuliza Waziri wa Elimu kuhusu maswali mawili, la kwanza kwanini Prof. Beregu amekataliwa kuongezwa mkataba kwa sababu tuu yeye ni kiongozi Chadema, huku kuna viongozi wengi tuu wa CCM kwenye utumishi wa umma?. La pili, kama Chadema, itampa ushahidi wa majina ya vigogo wa CCM kwenye utumishi wa umma, jee serikali itakuwa tayari kusitisha mikataba yao?.
Waziri wa Elimu, Prof. Magembe kwanza alikwepa swali la kwanza, kwa kutokuzungumzia kabisa sababu za Prof. Beregu kunyimwa mkataba, bali alisema, Prof. Beregu, alishastaafu toka 1999, hivyo mwajiri anao uhuru wa kumuongezea mkataba au hapana. Kwa sasa, mwajiri ameshapata watu wenye uwezo kama wa Beregu, hivyo hahitajiki tena, ndio maana hakupewa mkataba mpya.
Waziri akakaa, Naibu Spika akasema swali linalofuata (Swali jipya), Mdee akasisimama kumwambia Naibu Spika, swali la pili halijajibiwa. Naibu Spika akalazimisha limejibiwa wewe ndio hutaki kukubali. Akamshum dowm Halima Mdee na kuitisha swali linalofuata.