Wakuu,
Nadhani ni vizuri tukawa na mjadala focused. Kuna masuala mawili makubwa, yanayofanya pawe na mijadala miwili tofauti kwa wakati mmoja. Na yote mawili yamechangiwa kwa kauli mbili za Waziri Ghasia kama msingi wa hoja zake.
KAULI YA KWANZA: Kwamba Profesa Baregu haihitajiki tena kwa kuwa kuna uwezekano wa kupata wasomi kama yeye kwenye soko.
Wanaounga mkono hoja hii ya Hawa Ghasia wamejikita wanatumia hoja kadhaa mathalani kusema kuwa maprofesa wazee wasipewe mikataba kupitisha vijana(hawajiulizi je tuna maprofesa vijana wangapi?, kama hatuna wasomi wa kutosha ni wakina nani watawainua vijana mpaka kufikia huo uprofesa wazibe pengo? Au tunataka kwenda kutoa maprofesa toka nje kuwainua vijana wetu wafikie ngazi ya uprofesa?). Lakini suala la msingi la kutafakari ni kuwa Idara yake huko UDSM imetoa kauli kuwa inamhitaji. Sasa nani anayeamua vipaumbele vya mahitaji? Ni chuo au wizara ya utumishi? Tarehe 9 Disemba tulikuwa na Kongamano la Wanavyuo zaidi ya 1000 DDC Dar es salaam, walisema unanimously kuwa anahitajika. Lakini siku hiyo tulizungumzia suala la mfumo mpya wa utawala. Nikizungumzia hii haja ya decentralization. Haiwezekani Wizara ya utumishi ikakiamulia chuo kikuu cha Dar es salaam Profesa yupi auongezewe mkataba yupi usiongezewe. Na hapa ndipo inapozaliwa hoja ya kujiuliza. UDSM wanasema Orodha ya walioomba waongezewe mkataba ilikuwa na wengi, wengine wakakubaliwa, Baregu akakataliwa(sijui kwa kiasi gani haya maelezo yao ni sahihi); hili kama ni kweli maanake ni kwamba sababu ya kwanza ni KISINGIZIO.
Huu ni mjadala ambao nao ni mpana sana kuhusu sekta ya elimu nchini.
KAULI YA PILI: kwamba Baregu amekataliwa kuongezewa mkataba kwa kuwa amejihusisha na siasa.
Kwangu mimi hii ndio hoja inayohitaji mjadala wa kina, kwa kauli ya Hawa Ghasia maanake ni kwamba hata kama Profesa Baregu angekuwa ni kijana kabisa, anayehitajika mwenye sifa zote lakini ajira yake ingesitishwa kwa kuwa tu; ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA. Kwa hiyo, hii inamaanisha kwamba watumishi wote wa umma hawaruhusiwi kuwa wajumbe wa vikao vya vyama. Huu ni mjadala muhimu zaidi kwa kuwa haumuhusu Baregu pekee; kwenye mjadala huu lazima tunapojadili turejee waraka wa watumishi wa umma ambao tulianza kuuchambua hapa:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/34374-ruksa-kwa-watumishi-wa-umma-kushiriki-siasa.html
Ps: wapo wanaojenga hoja kwamba kwanini Baregu asiache tu suala ya UDSM kama anahitajika akaenda Chuo kingine, ama nje ya nchi ama akafanya kazi nyingine au akajikita kwenye CHADEMA. Ukweli ni kuwa fursa zote hizo anazo na yeye analitambua, na kwa kweli vyuo mbalimbali vinamuhitaji. Lakini, nimuhimu tukazingatia kwamba akiliichia hapa, atakuwa tayari ame-set precedence na kufanya malengo ya waliochukua uamuzi huu kutimia. Kama Profesa wa Siasa, anaacha legacy katika taifa kama akisimama kidete katika suala hili mpaka mwisho kulinda haki na misingi ya kisiasa na kiutawala ambayo yeye mwenyewe amekuwa akiifundisha maisha yake yote; na kwa kweli atalisaidia taifa letu katika muktadha mzima wa ushiriki wa watumishi wa umma kwenye siasa kwa kizazi chake na hata vijavyo. Mjadala huu usingefika hapa ulipofika kama mara baada ya kukataliwa angeenda tu nje au chuo kingine au angefanya consultancy zake binafsi. Naamini mjadala huu utafika mbali zaidi na kusaidia katika mabadiliko ya mifumo na mitazamo yetu.
Tuendelee na majadaliano,
JJ