Kwanini Prof. Baregu amenyimwa kazi UDSM?

Kwanini Prof. Baregu amenyimwa kazi UDSM?

The red part is a lie, mara ngapi tunaambiwa kuna uhaba wa lecturers Tanzania hadi wanaajiri wahindi na wakenya wenye vyeti fake? its time we decide to be serious on education, hii habari ya kuchanganya issue muhimu na siasa zinatupeleka pabaya, no wonder jana tu matokeo ya form four yametangazwa na kuonekana kiwango cha failures kimeongezeka sana, bila kusahau kwamba darasa la saba mwaka uliopita pia nusu yao walifeli. Sasa your stupid waziri anasema anaunda kamati itembelee shule ili kujua tatizo ,what a shame! Hii yote ni sababu ya kuchanganya siasa na elimu, matokeo yake tunajenga nchi ya vilaza kama walivyo vilaza hao mawaziri , i hate uongozi wa hii nchi.😡

ya form two..
thanks
 
Kwa nini iwe kwa Baregu pekee? Mvungi si anajihusisha na siasa huko NCCR mbona hatujasikia hii sheria imetumika dhidi yake? Wakili Abdallahah Safari naye vipi mbona hakubanwa? Besides Mkandala, Bana na Wakuu wote wa Mikoa si ni Watumishi wa Umma vipi mbona ni wanachama wa sisiemu?
Kweli hii nji ni ghasia tupu ikiongozwa na ghasia,
Cpt I feel your anger my brother
Mimi si mtaalamu sana wa mambo haya but nadhani kuna tofauti kati ya kujihusisha na siasa na kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Serikali yetu tukuru ndo inaweza kututofautishia mahali hapa!!

Ninavyoelewa mimi au nilivyoelewa baada ya kuisikiliza hadithi hii ya serikali ni kuwa mtumishi wa Uma ana ruhusiwa kuwa mwanachama wa chama fulai bila kutake part kwa maana ya kuwa na cheo chamani au kugombea wadhifa kichama na mara anapoona ana mwelekeo huu huwa anashauriwa aache kazi. Nafikiri ni kama alivyofanya Marehemu Prof. Shayo wa Democrasia Makini kama sikosei.

Wakisema mtumishi wa Umma asiwe mwanachama ina maana hata kura si watakosa? Its the same hata katika nchi nyingine nafikiri kwani nilishaona hata kule Ghana inatumika sheria hii.

Kuhusu Dr. Mvungi Sengodo hapa napata kigugumizi kwani sina uhakika na extent ya involvement yake wkenye siasa. Kama nilivyosema hapo awali mimi si mjuvi kiiiivyo
 
simuelewi muhashimiwa waziri anapokataa mkataba wa baregu kwa kigezo cha utumishi wa umma na siasa ...anasemaje kuhusu wakuu wa mikoa ambao ni watumishi wa umma kimsingi kama muhamed abdulaziz ,monica mbega et al ambao ni wajumbe wa halmashauri kuu ..ngazi mbali mbali [vyeo vya kisiasa], ni wabunge, na ni wakuu wa mikoa....

nadhani hii ni kuwaonea maprofesa ..kama watakaa kimya basi watakuwa wananyimwa uhuru wao wa kikatiba huku ndani ya ccm wakiachiwa tu ...nakumbuka hata profesa SAFARI alishaingia matatani na sijui imefika wapi... na sasa wengine kama kina dr SENGODO MVUNGI inabidi nao wajiandae kunyolewa.......mwenzao dr masumbuko lamwai...walimfukuza chuo ..alipoamua kujiunga nao wakampa kazi haraka haraka na ubunge juu....na hata sasa anafundisha kwa mikataba mzumbe,,,zanzibar university...na vyuo vingine [binafsi]....

ni sheria ndio lakini inaonekana hii sheria ina double standard!!! ma profesa wameona na wamesikia ....wamefungwa luku!!..kama watakuwa wapinzani!!!
 
Cpt I feel your anger my brother
Mimi si mtaalamu sana wa mambo haya but nadhani kuna tofauti kati ya kujihusisha na siasa na kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Serikali yetu tukuru ndo inaweza kututofautishia mahali hapa!!

Ninavyoelewa mimi au nilivyoelewa baada ya kuisikiliza hadithi hii ya serikali ni kuwa mtumishi wa Uma ana ruhusiwa kuwa mwanachama wa chama fulai bila kutake part kwa maana ya kuwa na cheo chamani au kugombea wadhifa kichama na mara anapoona ana mwelekeo huu huwa anashauriwa aache kazi. Nafikiri ni kama alivyofanya Marehemu Prof. Shayo wa Democrasia Makini kama sikosei.

Wakisema mtumishi wa Umma asiwe mwanachama ina maana hata kura si watakosa? Its the same hata katika nchi nyingine nafikiri kwani nilishaona hata kule Ghana inatumika sheria hii.

Kuhusu Dr. Mvungi Sengodo hapa napata kigugumizi kwani sina uhakika na extent ya involvement yake wkenye siasa. Kama nilivyosema hapo awali mimi si mjuvi kiiiivyo

Mwanajamiione

Suala hili la watumishi wa umma kushiriki kwenye siasa tuliwahi kulijadili hapa na kuurejea waraka husika. Unaweza kuingie kwenye hii thread utapata majibu ya baadhi ya masuala ambayo umeonyesha mashaka nayo: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/34374-ruksa-kwa-watumishi-wa-umma-kushiriki-siasa.html

Nawatakia mjadala mwema


JJ
 
Baregu aponzwa na siasa

Hawa Ghasia amwambia si lazina aajiriwe Tanzania inasikitisha kama si kuhuzunisha hebu fuatilia mwenyewe habari hii..............

“Waraka Mkuu wa Utumishi wa Umma namba moja wa mwaka 2000 unatoa maelekezo kuhusu maadili ya watumishi wa umma katika mfumo wa vyama vingi na ushiriki wa watumishi wa umma katika siasa ikiwemo miiko yake. Waraka huo pia unabainisha mambo yanayoruhusiwa na yale yasiyoruhusiwa kwa watumishi wa umma katika kushiriki siasa.
“Baadhi ya mambo yasiyoruhusiwa kwa watumishi wa umma ni kugombea nafasi yoyote chini ya katiba au uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha siasa akiwa mtumishi wa umma,” alisema Ghasia.

Kama waraka huo unakataza mbona wafanyakazi wengi wa umma wanagombea nafasi za siasa hasa ubunge na wapowashindwa wanarejea kazini kama kawaida? mfano iko mingi tu?
 
Mimi ninataka kuangalia hili suala nje ya siasa, hivi Prof. Baregu hana jambo la kufanya baada ya kustaafu nje ya kuajiriwa na UDSM? Mimi nadhani hana haja ya kung'ang'ania kuajiriwa UDSM anahitaji kujua nini cha kufanya baada ya kustaafu. Baregu hawezi kuwa mwajiriwa wa maisha pale UDSM, after all ni lazima aondoke ili wengine wapate nafasi ya kufanyakazi.

Mkuu Pundamilia ingekuwa ni vema kama tusingekuwa personal kwenye jambo hili. Kama Baragu ana qualify basi hakukuwa na sababu ya kupiga politiki. Unaweza kumuuliza Kingunge swali hilo hilo, kwani lazima siasa? kwa nini asiangalie mambo mengine? sio yeye tu. Panga lililomfyeka Lamwai sasa linataka kumpitia Baregu, unaweza kusema ni kwanini academicians wanakimbilia siasa? ni kasumba tu, na kwanini wanasiasa uchwara wanaogopa academicians? utaona kuwa kama kweli unataka kuchuma pesa Tanzania ni vema ukiwa mwanasiasa, na wanasiasa uchwara ambao uwezo wao ni kupiga domo tu wanatishiwa na uwepo wa academicians kwenye siasa. Na bahati mbaya ukiangalia academicians mahiri wa Tanzania, na civil servant karibu wote wameingia kwenye siasa, sababu ni kuwa that is where they can make easy money, au huko ndio rahisi kuiba.
 
Sidhani km prof baregu hana kazi nyingine ya kufanya tofauti na kufundisha UDSM anazo nyingi,lakini je katika hili ametendewa haki?Je watanzania tunajifunza nini?Tukae kimya au tupaze sauti zetu?


waziri Ghasia ....haoni umuhimu wa msomi kama prof baregu ..pamoja na kina dr bana kusema kuwa fani ya baregu inahitajika sana pale mlimani na kwenye vyuo vingi...Ghasia amesema kuwa pROF baregu HANA SOKO na AMEPITWA NA WAKATI!!!!
 
Jamani tuache siasa katika mambo ya msingi Elimu ni issue ya msingi soni sababu ya kumzuia Prof. Baregu kufundisha pale UDSM kwani anafundisha siasa za Chadema? mnasema amekiuka taratibu za serikali zipi? yeye ni mwanajeshi aua Polisi na Magereza? hao ndio najua kuwa hawtakiwi kujihusisha na siasa jamani viongozi badilikeni anglia maslahi ya nchi kwanza na sio kuweka siasa Mbele ya yote, kwani kwa kumnyima Baregu ajira hapo UDSM mnafikiri mnaweza kubadilisha mtizamo wa Watanzania? sisi ndio wapiga kura na tunaowaweka madarakani na dnio tutakaoamua nani anatufaa na nani asyetufaa, binafsi sioni kosa la Baregu na hali kama hii ikiendelea itaigharimu serikali inayoongozwa na CCM, inaonyesha mnalazimisha watu wakubaliane na CCM hata kama kuna uozo ndani yake.
 
waraka wa watumishi wa umma kutojihusisha na siasa upo. ndio maana hata maprofesa wengine wanaotaka kugombea ubunge wanaachana na kufundisha ndipo wanaenda kugombea. wateuliwa wa Rais hawahusiki na waraka huu

labda cha msingi hapa ni kuupinga waraka huu
ingawa kwa upande mwingine mtumishi wa umma akishiriki kwenye siasa kuna upande fulani huenda akavuruga kazi zake hivyo tuangalie pande zote.

wapo wengi walioacha kazi na kwenda kugombea uongozi, kama akina Prof. mwalyosi, Prof. mgombero ambaye aliomba tena baada ya kuacha siasa. na wengine wengi.

kwanini wengine wanaendelea, Two wrongs don't make a right. Meaning if someone does something wrong, doesn't mean someone else can do another wrong to make it right. ni vizuri tukajikita kwenye mzizi wa tatizo kuliko kumwona Hawa Ghasia kama au mawaziri kama kituko wakati wanatekeleza sheria zilivyopo.
 
waraka wa watumishi wa umma kutojihusisha na siasa upo. ndio maana hata maprofesa wengine wanaotaka kugombea ubunge wanaachana na kufundisha ndipo wanaenda kugombea. wateuliwa wa Rais hawahusiki na waraka huu

labda cha msingi hapa ni kuupinga waraka huu
ingawa kwa upande mwingine mtumishi wa umma akishiriki kwenye siasa kuna upande fulani huenda akavuruga kazi zake hivyo tuangalie pande zote.

wapo wengi walioacha kazi na kwenda kugombea uongozi, kama akina Prof. mwalyosi, Prof. mgombero ambaye aliomba tena baada ya kuacha siasa. na wengine wengi.

kwanini wengine wanaendelea, Two wrongs don't make a right. Meaning if someone does something wrong, doesn't mean someone else can do another wrong to make it right. ni vizuri tukajikita kwenye mzizi wa tatizo kuliko kumwona Hawa Ghasia kama au mawaziri kama kituko wakati wanatekeleza sheria zilivyopo.

Umeusoma waraka wote?

Si kwamba wanaachana na kufundisha, labda waache kwa hiyari yao. Waraka unawataka kuchukua likizo, na wakishinda ubunge wanapaswa kuomba likizo ya muda mrefu au kujiuzulu. Lakini hapa hatuzungumzii kugombea ubunge, kwa kuwa baregu hakuwa mbunge wa CHADEMA bali mjumbe wa Kamati kuu ya chama. Naomba kifungu kinachokataza hao maprofesa kuwa wajumbe kwenye vikao vya vyama

JJ
 
Tatizo la wahadiri wengi wanaogopa maisha ya uswahilini, wamezoea mishahara tu, kwani hao vijana mnaowafundisha mnataka waende wapi kama si kuwapokea ninyi wahadhiri pindi mnapostaafu, au mwadhiri lazima afundishe mpaka afe?
 
Wacha waondoke hawa wazee wamezidi kungangania madaraka. eti bado ni muhimu katika fani yake, basi mtu wanamna hii toka aanze kufundisha hadi leo kama hakuna wakumrithi basi alikuwa hawajengi wanafunzi katika kujua kama yeye ili baadae waendeleze na kubudi mazuri zaidi ya yakwake.
 
Hi isiishie tu kwa prf Baregu mheshimiwa waziri angalia wale wote waliokwisha staafu na kuadha kuajiriwa kwa mikataba waondoke kwani vijana tupo mtaani hatuna kazi tuna madegree na ma GPA makubwa kuanzia 4.1 hadi 5
 
Duh! jinsi unavyojenga hoja kiovyoovyo hata hilo li GPA lako litakuwa la kudesa tu.

Hi isiishie tu kwa prf Baregu mheshimiwa waziri angalia wale wote waliokwisha staafu na kuadha kuajiriwa kwa mikataba waondoke kwani vijana tupo mtaani hatuna kazi tuna madegree na ma GPA makubwa kuanzia 4.1 hadi 5
 
Mimi sitaki kusikia tena serikali ikilalamika kuwa wahadhiri wetu wanakimbilia nje LET THEM GO AND DO NOT DISTURB THEM ANY MORE, hili la Baregu liwe symbolic kwa ma-lecturer wote walio ndani na nje na serikali. Serikali yetu hufanya kazi kwa kukomoa hujifanya kuzingatia waraka pale tu inapoona inataka kufanya hivyo na si kwa mujibu wa sheria kama wanavyotuambia, baada ya hapo waraka unafungiwa kabatini. Haya mambo ndiyo wananchi wanayalalamikia, tukisema wazi waziri fulani hafai wanasema tuna wivu hapana na rais mwenyewe anamwangalia tu this is very serious.
 
VIONGOZI VILAZA, SERA WANAZO ZISIMAMIA NI VILAZA, UPUMBAVU NA UJINGA KIASI NASEMA TAIFA HILI LAITAJI KUMPATA ROLEN WA GHANA KUWA ADABISHA MAPUMBAVU KTK SYSTEM, HALI NIINGI AKILIN WALA HALIPATI NAFAS KTK AKIL YANGU ETI PROF BAREGU AMEINGIA KTK SIASA HVYO HAFAI KUENDELEA KUWA MHADHIRI, JAMAN TUNAENDA WAPI TENA MIM NASEMA HAWA MAWAZIR WAKIKE NI TAFARANI KTK TAIFA WANAMANENO YAKIAJABU AJABU UKIANZIA SOFIA SIMBA NA HUYA GHASI ALAFU WAMEPEWA VITENGO NYETI, JAMAN JAMAN KWELI LEO PROF ANA AMBIWA AMECHUJA WAKATI AMELISAIDIA TAIFA HL KWA KIAS KIKUBWA HALAFU RAISI KAUCHUNA KIMYA! JAMAN TUNAENDA WAPI, MBONA ELIMU HAIJATUSAIDIA HV NI LINI SERIKAL ITAJUWA UMUHIMU NA THAMAN YA HAWA PROF TULIO NAO? NI VILE SERA ZETU NA KATIBA NI MBOVU MTU KAMA PROF BAREGU ALIPASWA KUWA WAZIRI KTK MOJA YA WIZARA NYETI NA KWA HAKIKA TAIFA LINGEKUWA JUU. NALAANI KITENDO HK NA LAANI MANENO ALIYO SEMA WAZIR NAKUMWAMBIA WENYE NCHI TUNAKUJA NA HAKIKA HISTORIA ZAO ZITABAK KAMA MAWE YA MAKABURI KWA VILE TULIPO WAPA NAFASI WAO WALITUMIA KÚUWA VIPAJI. PROF ATA NG'AA KAMA NYOTA NA VIJANA TUPO NYUMA YAKE NA MUNGU ATUSAIDIE, GOD BLESS JAMAA FORUM AND GOD BLESS TANZANIA. Thank u
 
Hi isiishie tu kwa prf Baregu mheshimiwa waziri angalia wale wote waliokwisha staafu na kuadha kuajiriwa kwa mikataba waondoke kwani vijana tupo mtaani hatuna kazi tuna madegree na ma GPA makubwa kuanzia 4.1 hadi 5


Hizo GPA za 4.1-5 ni za kweli? Enzi zetu watu wa namna hiyo walikuwa ni lulu. Hata hivyo hao wata TA hawawezi kuingia College na kuwa maprofesa leo. Pia suala la kutoajiri watu hadi vyuo vinahaha sasa haikuwa sera ya Baregu. Ilikuwa ni ujinga wa watawala wetu kusikiliza ushauri wa WB na IMF na kushindwa kutumia common sense pale walipositisha ajira hadi vyuoni mwanzoni mwa miaka ya 90. Issue unayoongelea ni topic nyingine inayojitegemea. Naomba tuache kuchanganya mada.
 
Dr Mvungi yule wa NCCR-MAGEUZI bado yupo hapo UDSM? Yeye aligombea Urais kabisa mwaka 2005 na ana nafasi huko kwenye chama chake.

Jamani let us not all be blind nani asiyejua mahusiano ya NCCR na CCM? kama bado unafikiri NCCR ni chama cha upinzani umepotea kidogo it is a CCM B per se, NCCR ilikuwa ile ya 1995 baada ya hapo ikavurugwa vurugwa ili isije kusumbua tena, tutapiga kelele sana na kina Mvungi wao wanajua wanachokifanya waacheni wafanye wanachotaka nyie kama mmegundua hilo mnaachana naye, lakini mkiendelea kupiga kelele mbona mbona Mvungi CCM ndio wanapenda hilo kuwaona mna loose direction.
 
Wakuu,

Nadhani ni vizuri tukawa na mjadala focused. Kuna masuala mawili makubwa, yanayofanya pawe na mijadala miwili tofauti kwa wakati mmoja. Na yote mawili yamechangiwa kwa kauli mbili za Waziri Ghasia kama msingi wa hoja zake.

KAULI YA KWANZA: Kwamba Profesa Baregu haihitajiki tena kwa kuwa kuna uwezekano wa kupata wasomi kama yeye kwenye soko.

Wanaounga mkono hoja hii ya Hawa Ghasia wamejikita wanatumia hoja kadhaa mathalani kusema kuwa maprofesa wazee wasipewe mikataba kupitisha vijana(hawajiulizi je tuna maprofesa vijana wangapi?, kama hatuna wasomi wa kutosha ni wakina nani watawainua vijana mpaka kufikia huo uprofesa wazibe pengo? Au tunataka kwenda kutoa maprofesa toka nje kuwainua vijana wetu wafikie ngazi ya uprofesa?). Lakini suala la msingi la kutafakari ni kuwa Idara yake huko UDSM imetoa kauli kuwa inamhitaji. Sasa nani anayeamua vipaumbele vya mahitaji? Ni chuo au wizara ya utumishi? Tarehe 9 Disemba tulikuwa na Kongamano la Wanavyuo zaidi ya 1000 DDC Dar es salaam, walisema unanimously kuwa anahitajika. Lakini siku hiyo tulizungumzia suala la mfumo mpya wa utawala. Nikizungumzia hii haja ya decentralization. Haiwezekani Wizara ya utumishi ikakiamulia chuo kikuu cha Dar es salaam Profesa yupi auongezewe mkataba yupi usiongezewe. Na hapa ndipo inapozaliwa hoja ya kujiuliza. UDSM wanasema Orodha ya walioomba waongezewe mkataba ilikuwa na wengi, wengine wakakubaliwa, Baregu akakataliwa(sijui kwa kiasi gani haya maelezo yao ni sahihi); hili kama ni kweli maanake ni kwamba sababu ya kwanza ni KISINGIZIO.

Huu ni mjadala ambao nao ni mpana sana kuhusu sekta ya elimu nchini.

KAULI YA PILI: kwamba Baregu amekataliwa kuongezewa mkataba kwa kuwa amejihusisha na siasa.

Kwangu mimi hii ndio hoja inayohitaji mjadala wa kina, kwa kauli ya Hawa Ghasia maanake ni kwamba hata kama Profesa Baregu angekuwa ni kijana kabisa, anayehitajika mwenye sifa zote lakini ajira yake ingesitishwa kwa kuwa tu; ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA. Kwa hiyo, hii inamaanisha kwamba watumishi wote wa umma hawaruhusiwi kuwa wajumbe wa vikao vya vyama. Huu ni mjadala muhimu zaidi kwa kuwa haumuhusu Baregu pekee; kwenye mjadala huu lazima tunapojadili turejee waraka wa watumishi wa umma ambao tulianza kuuchambua hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/34374-ruksa-kwa-watumishi-wa-umma-kushiriki-siasa.html


Ps: wapo wanaojenga hoja kwamba kwanini Baregu asiache tu suala ya UDSM kama anahitajika akaenda Chuo kingine, ama nje ya nchi ama akafanya kazi nyingine au akajikita kwenye CHADEMA. Ukweli ni kuwa fursa zote hizo anazo na yeye analitambua, na kwa kweli vyuo mbalimbali vinamuhitaji. Lakini, nimuhimu tukazingatia kwamba akiliichia hapa, atakuwa tayari ame-set precedence na kufanya malengo ya waliochukua uamuzi huu kutimia. Kama Profesa wa Siasa, anaacha legacy katika taifa kama akisimama kidete katika suala hili mpaka mwisho kulinda haki na misingi ya kisiasa na kiutawala ambayo yeye mwenyewe amekuwa akiifundisha maisha yake yote; na kwa kweli atalisaidia taifa letu katika muktadha mzima wa ushiriki wa watumishi wa umma kwenye siasa kwa kizazi chake na hata vijavyo. Mjadala huu usingefika hapa ulipofika kama mara baada ya kukataliwa angeenda tu nje au chuo kingine au angefanya consultancy zake binafsi. Naamini mjadala huu utafika mbali zaidi na kusaidia katika mabadiliko ya mifumo na mitazamo yetu.

Tuendelee na majadaliano,

JJ
 
Back
Top Bottom