Kwanini Prof. Baregu amenyimwa kazi UDSM?

Kwanini Prof. Baregu amenyimwa kazi UDSM?

Well done Mrs Ghasia, Baregu is too old to stay . He must go.Unemployment rate is too high to keep his job.

I believe you are not serious. Though he is old, but he is very active and productive. May be TBC wampe one hour kila wiki kwa ajili ya kulifundisha taifa letu elimu ya uraia na masuala ya kimataifa.
 
It is a shame prominent prof like him to fail to comence his own prof baregu university college of whatever. Rest in peace prof DR kairuki. THEY NEED TO BE FREED FROM PENSION IMMUNE DEFICIENCE SYNDROM MBONA WAHINDI HAWANA MPANGO NA NSSF?? PROFESA HAWEZI KUJIAJIRI HII NI HASARA KUBWA SANA KWA TAIFA
 
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, imeshindwa kutoa sababu za kukataa kumwajiri kwa mkataba Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Mwesiga Baregu.
Badala yake, ofisi hiyo imemrushia mpira Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandara kuwa ndiye anayepaswa kuulizwa sababu kwa kuwa anazijua.
Profesa Baregu alistaafu mwaka jana na UDSM ilipeleka majina 23 ya wahadhiri wastaafu kwenye ofisi hiyo likiwemo la Profesa Baregu kuomba waendelee na kazi kutokana na uhaba wa wahadhiri chuoni hapo lakini jina pekee la Profesa Baregu lilikataliwa.
Wanataaluma wa chuo hicho walilalamika na kutishia kuandamana wakisema suala hilo limefanywa kisiasa zaidi kwani Profesa Baregu amekuwa akiikosoa serikali mara kwa mara.
Akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, mmoja wa Wakurugenzi Wasaidizi (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Muhoji Nyakimura, alisema hawezi kuzungumza chochote kuhusu suala hilo kwani ni nyeti na ndiyo analisikia.
Nipashe ilishamwachia maswali hayo kwa muda wa wiki nzima sasa.
Lakini katika hali ya ya kushangaza, Nyakimura alisema mwenye uwezo wa kuzungumzia sababu za Profesa Baregu kukataliwa mkataba wake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandara.
“Mukandara ndiye alileta majina ya kuomba wahadhiri sasa nenda kamuulize yeye sababu za utumishi kukataa jina la Profesa Baregu,” alisisitiza.
Hata hivyo, mwandishi alimweleza Nyakimura kuwa anayeajiri sio Profesa Mukandara bali ni utumishi na ndio wanajua sababu za kuajiri na kutoajiri.
Baada ya kubanwa kwa maswali hayo, Nyakimura alisema atalifanyia uchunguzi suala hilo na kutoa majibu bila kueleza lini uchunguzi huo utakamilika.
“Haya ni mambo nyeti na mazito usidhani naweza kukurupuka kuropoka ropoka tu wacha niwasiliane na wenzangu tujue cha kusema,” alisema.
Nipashe iliacha maswali kwenye ofisi hiyo tangu mwanzoni mwa wiki hii lakini wahusika wamekuwa wakikwepa kutoa majibu.

CHANZO: NIPASHE
 
Nimeshatoa mawazo yangu kwenye hili, sasa kuendelea kubishana tu ilimradi kujaza maneno kwenye forum sio tija. Kama unafikiri mwanasiasa na mwanataaluma workload yao ni sawa hayo pia ni mawazo yako anaeyakubali atayapokea. Unapofananisha Kingunge na Wanataaluma sijui unatumia vigezo gani? Kwani kwenye siasa kumewekwa kikomo cha umri? Unafikiri waliotoa wazo la kuwepo kikomo cha utumishi kwa kutumia umri walikurupuka tu na kuweka? Kwanini kwenye siasa hakuna hicho kikomo...? Mugabe leo ana miaka zaidi ya themanini bado yuko madarakani.....unafikiri hicho ndio kipimo kwa kuwa Mugabe bado yupo kwenye siasa basi hata mwanataaluma mwenye umri huo aendelee kufundisha, kufanya utafiti na kutoa ushauri akiwa mwajiriwa kwenye vyuo vyetu?
Kwa kuwa kwenye siasa hakikuwekwa kikomo cha umri, wewe unaona huo ni kama msahafu na hautakiwi kuguswa ama kuzungumzwa?

Tuache ya wana taaluma, wewe mtazamo wako kwa wanasiasa ni nini? Tuendelee kujadili bro! hatujazi maneno tu, tunatoa hoja! i will be right back...
 
Baregu aponzwa na siasa

Hawa Ghasia amwambia si lazina aajiriwe Tanzania inasikitisha kama si kuhuzunisha hebu fuatilia mwenyewe habari hii..............

na Asha Bani

HATIMAYE serikali imesema imesitisha ajira ya aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Saalam, Profesa Mwesiga Baregu kutokana na kukiuka sheria ya utumishi wa umma.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, alisema Profesa Baregu alikiuka maelekezo ya waraka mkuu namba moja wa Utumishi wa Umma wa mwaka 2000 ambao unakataza kujihusisha na masuala ya siasa.

“Waraka Mkuu wa Utumishi wa Umma namba moja wa mwaka 2000 unatoa maelekezo kuhusu maadili ya watumishi wa umma katika mfumo wa vyama vingi na ushiriki wa watumishi wa umma katika siasa ikiwemo miiko yake. Waraka huo pia unabainisha mambo yanayoruhusiwa na yale yasiyoruhusiwa kwa watumishi wa umma katika kushiriki siasa.

“Baadhi ya mambo yasiyoruhusiwa kwa watumishi wa umma ni kugombea nafasi yoyote chini ya katiba au uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha siasa akiwa mtumishi wa umma,” alisema Ghasia.

Alisema Profesa Baregu akiwa kama mtumishi wa umma amekiuka waraka huo kwa kujihusisha na siasa kutokana na kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Ghasia alisema Baregu amekuwa akishikilia nafasi hiyo kwanza kama mjumbe wa kuteuliwa na mwenyekiti wa CHADEMA na sasa kama mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho baada ya kuchaguliwa na Baraza Kuu la CHADEMA mwezi Septemba mwaka jana.

“Kwa hiyo Profesa Baregu ni kiongozi wa CHADEMA na hivyo kukosa sifa ya kuendelea na utumishi wa umma. Utaratibu huu ni kwa watumishi wote wanaoamua kugombea nyadhifa mbalimbali za uongozi katika vyama vyote vya siasa,” alisema Waziri Ghasia.

Alisema haki ya Profesa Baregu ya kuajiriwa kama ilivyo kwa watumishi wote wa umma, ilikwisha pale alipostaafu kwa lazima na kwa mujibu wa sheria mwaka 1999.

“Akiwa kiongozi wa kisiasa, ajira yake kama mtumishi wa umma ilikuwa sharti ikome kwa mujibu wa kanuni na taratibu za ushiriki wa watumishi wa umma katika siasa,” alisema Ghasia.

Alisema utaratibu wa serikali unaruhusu baada ya mtumishi kustaafu kwa mujibu wa sheria mwajiri wake kulingana na mahitaji na inapothibitika kuwa hawezi kumpata mtumishi mwenye sifa kama hizo katika soko hulazimika kumwombea mstaafu ajira ya mkataba kwenye mamlaka husika.

Ghasia alisema kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma mkataba wa ajira kwa mtumishi wa umma baada ya kustaafu kwa umri na kwa mujibu wa sheria, siyo haki ya mtumishi bali ni utashi na busara (discretion) ya mamlaka.

“Kwa kutumia utaratibu huu, Profesa Baregu alistaafu kazi kwa mujibu wa sheria tangu mwaka 1999 Februari 24 akiwa na umri wa miaka 55. Baada ya kustaafu ameajiriwa kwa mkataba na Chuo Kikuu Dar es Salaam mara tatu, aliajiriwa kwa mkataba wa mwaka mmoja Machi 21 mwaka 2003 baada ya kurejea kutoka Harare, Zimbabwe alikokuwa akifanya kazi tangu alipostaafu kazi,” alieleza Ghasia.

Aliendelea kueleza kama haitoshi alipewa mkataba mwingine wa kipindi cha miaka miwili ambacho kiliisha mwaka 2006 na kuongezewa mkataba mwingine ambao pia ulimalizika Januari 2008.

Waziri Ghasia ambaye hakutaka kuulizwa maswali zaidi ya matatu, akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari aliyetaka kujua kama kuondoka kwa profesa huyo hakutakuwa na pengo katika taaluma na kwamba hakuna mhadhiri aliyeziba nafasi hiyo kwa sasa, alisema hadhani kama chuo hicho kinachojulikana duniani kote kitaanguka ama kushuka kwa kuondoka kwa profesa huyo.

“Kama Baregu ni bidhaa bora inayogombaniwa kwa nini iwe ni UDSM tu na asiende kwingine? Kwani ni lazima awe mhadhiri wa chuo hicho tu,” alihoji Ghasia.

Alipoulizwa kwanini serikali ilimuongezea Baregu mkataba mwaka 2006 huku ikijua fika anajihusisha na masuala ya siasa alisema: “Kosa lililofanyika wakati huo haliwezi kamwe kurudiwa kwa sasa.”

Alisema waraka huo haumbani mwanachama wa CHADEMA pekee bali wa vyama vyote vya siasa huku akitolea mfano kuwa hata Sara Msafiri alivyogombea ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi, aliondolewa katika utumishi wa umma.

Aliwataja makada wengine wa CCM waliobanwa na waraka huo kuwa ni Masauni Yusufu Masauni, aliyelazimika kuacha ajira yake katika Wizara ya Nishati na Madini na kugombea nafasi ya uenyeviti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Alipoulizwa sababu za Waziri Mkuu kuendelea kuchukua pensheni (mafao) mara baada ya kustaafu, alijibu kuwa kama mtumishi wa umma waziri ana haki ya kuchukua pensheni kwa mujibu wa sheria.

“Mwandishi nimesema kuwa leo sitaki kujibu swali lingine zaidi ya kuzungumzia ajira ya Baregu, wewe unataka nikujibu hilo, nakwambia kama Waziri Mkuu ana haki ya kuchukua pensheni kama mtumishi wa umma pia, na usiulize swali jingine… kama umeshawapa na wenzako maswali wakashindwa kukuulizia vizuri utajua mwenyewe,” alijibu Ghasia kwa ukali.

Aidha mwandishi mwingine alipohoji sababu za Dk. Sengodo Mvungi kubakia kwenye ajira wakati anajihusisha kwenye masuala ya siasa, alijibu kuwa hata yeye naye hajaongezewa mkataba wake.

Akizungumzia suala hilo kwa njia ya simu, Profesa Baregu alishangaa kuchelewa kwa serikali kutolea ufafanuzi juu ya suala hilo kwani amekaa miezi sita bila kujua sababu za yeye kunyimwa mkataba tena.

Profesa Baregu alisema waraka huo una utata kutokana na kuwagusa wahadhiri ambao wako katika vyama vya upinzani na kuwaacha wengine waliomo CCM (majina yanahifadhiwa) wanaoendelea kufundisha chuoni hapo.

“Nitatafuta wanasheria ili wauchambue waraka huo kwa kina kwani unaonekana kutumika kibaguzi na kukwaza haki za msingi za raia,” alisema Profesa Baregu.
 
Eti watu wanauliza kwa nini Tanzania hatuendelei, nani kawambia hatuendelei?
 
Kwa nini iwe kwa Baregu pekee? Mvungi si anajihusisha na siasa huko NCCR mbona hatujasikia hii sheria imetumika dhidi yake? Wakili Abdallahah Safari naye vipi mbona hakubanwa? Besides Mkandala, Bana na Wakuu wote wa Mikoa si ni Watumishi wa Umma vipi mbona ni wanachama wa sisiemu?
Kweli hii nji ni ghasia tupu ikiongozwa na ghasia,
 
Gret thinkazz, ili thread inoge, tunauomba waraka wenyewe. Ukisikia sheria zisizotenda haki ndo hizi.
 
Mimi ninataka kuangalia hili suala nje ya siasa, hivi Prof. Baregu hana jambo la kufanya baada ya kustaafu nje ya kuajiriwa na UDSM? Mimi nadhani hana haja ya kung'ang'ania kuajiriwa UDSM anahitaji kujua nini cha kufanya baada ya kustaafu. Baregu hawezi kuwa mwajiriwa wa maisha pale UDSM, after all ni lazima aondoke ili wengine wapate nafasi ya kufanyakazi.
 
Baregu anaponzwa sio na siata tu, bali kuwa mpinzani wa chama tawala. vyuo vikuu si viko vingi? Aende huko akale kuku kwa mrija. Achana na UDSM na mambo yao ya 1947. Baregu ni muhimu kuwapo kwenye Kamati kuu ya chama chochote kwa elimu na uzoefu wake. Au tuamini kwamba wasio na shule ya kutosha ndio pekee wanaotahili siasa?

Pole Baregu, nenda kwa homeboy HKU au Tumaini au cha wahindi, hawa na ghasia zao wasitubabaishe

Leka
 
Mkurugenzi wa AICC Mr Kaale mbona ni mjumbe wa NEC ccm na aliteuliwa na Rais kushika wadhifa huo baada tu ya kuchaguliwa katika NEC kupitia mkoa wa Arusha.Ghasia is playing dirty politics,kama ni waraka uwe kwa watumishi wote kuzingatia maslahi ya Taifa.
 
Wadau naomba tuliangalie hili sakata la Prof. Baregu katika mtazamo wa maslahi ya Taifa. Tumesikia jana waziri Ghasia akizungumzia juu ya serikali kugoma rasmi kumwongezea mkataba na kauli yake eti "kwani lazima afanye kazi UDSM peke yake?".

Wote tunajua jinsi nchi hii ilivyo na uhaba wa wahadhiri vyuoni achilia mbali wahadhiri wa level ya Prof. Baregu na pia tumekuwa tukisikia serikali ikilalamika kuwa wataalam wanakimbilia nje wakiwemo wahadhiri wanaofuata greener pastures huko nje, sasa jamani pamoja na hilo la sijui kukiuka taratibu za utumishi wa umma nionavyo mimi sidhani kama serikali ilipaswa kusitisha ajira ya Prof huyu kama maslahi ya umma yangeongoza utashi wa hao wanaotoa maamuzi, naamini uamuzi uliotangazwa na serikali umechangiwa sana na sababu za kisiasa na hilo la kukiuka maadili ya utumishi wa umma limeletwa tu kujustify maamuzi, besides mbona hapo nyuma walisha-renew mkataba wake wakati tayari akiwa na wadhifa CHADEMA, iweje sasa ndio hilo liibuke..,

nchi hii inanisikitisha sana kwa kweli.
 
nchi hii siasa inaongoza mambo mengi ya msingi, ukitaka kujua kuna tatizo kumbuka yule afisa habari wa Wizara alijibu nini alipoulizwa, alisema kuwa hawajawahi kuiona barua ya Baregu hata mara moja ikiomba kuongezewa muda, sasa imagine ofisa wa Wizara anatoa taarifa ya uwongo kwa UMMA kua mzee Baregu ni mwongo hakuandika barua , na kama aliaandika UDSM hawakuipeleka Utumishi kwa hiyo viongozi wa UDSM ni waongo wa kiwango cha kitaifa ...sasa Hawa anapaswa kuomba radhi mbele ya UMMA kwa kumtuma afisa wake kutudanganya kuwa wizara haina taarifa na swala la Baregu.
BADO naamini tunahitaji mawazo yakinifu katika maswala mazito yakuendesha nnchi, hatuna MAWAZIRI waadilifu hata kidogo, uwezo wao, utashi na uelewa wao juu ya mambo ya kitaifa ni wakutiliwa shaka.
 
Kwa nini iwe kwa Baregu pekee? Mvungi si anajihusisha na siasa huko NCCR mbona hatujasikia hii sheria imetumika dhidi yake? Wakili Abdallahah Safari naye vipi mbona hakubanwa? Besides Mkandala, Bana na Wakuu wote wa Mikoa si ni Watumishi wa Umma vipi mbona ni wanachama wa sisiemu?
Kweli hii nji ni ghasia tupu ikiongozwa na ghasia,

Correction Abdallah Safari, Professor of International Law? alifukuzwa kazi na wizara ya Mambo ya nje akiwa mkufunzi pale CFR - Chuo cha Diplomasia.

Fuatilieni elimu ya ghasia inawezekana ni ghasia kweli kweli-ya kofoji?!!!!!!!!!
 
Mimi ninataka kuangalia hili suala nje ya siasa, hivi Prof. Baregu hana jambo la kufanya baada ya kustaafu nje ya kuajiriwa na UDSM? Mimi nadhani hana haja ya kung'ang'ania kuajiriwa UDSM anahitaji kujua nini cha kufanya baada ya kustaafu. Baregu hawezi kuwa mwajiriwa wa maisha pale UDSM, after all ni lazima aondoke ili wengine wapate nafasi ya kufanyakazi.

Karibu ndani ya nyumba Hawa Ghasia.
wengine wapi hao unaosema? Kama wapo kwa nini bado kuna upungufu?
 
Wakuu naona tatizo si waziri wala Uongozi wa juu wa UDSM tatizo hapa ni sheria zetu na umma na katiba yetu haziendani na mabadiliko halisi ya nchi yetu kisiasa,kiuchumi na hata kijamii.

Sheria inasema na inakataza mtumishi wa umma kushiriki katika siasa, hii tungeiangalia upya kama Proffessor Baregu mwenyewe alivyoeleza nia yake ya kwenda mahakamani kupinga sheria hii.na ndio maana kasema agombei ajira ataka kwenda mahakamani kupinga sheria hiyo inyokinzana na katiba yetu kwa maslahi ya watanzania wote kwa sasa na hata hapo baadaye.
 
nchi hii siasa inaongoza mambo mengi ya msingi, ukitaka kujua kuna tatizo kumbuka yule afisa habari wa Wizara alijibu nini alipoulizwa, alisema kuwa hawajawahi kuiona barua ya Baregu hata mara moja ikiomba kuongezewa muda, sasa imagine ofisa wa Wizara anatoa taarifa ya uwongo kwa UMMA kua mzee Baregu ni mwongo hakuandika barua , na kama aliaandika UDSM hawakuipeleka Utumishi kwa hiyo viongozi wa UDSM ni waongo wa kiwango cha kitaifa ...sasa Hawa anapaswa kuomba radhi mbele ya UMMA kwa kumtuma afisa wake kutudanganya kuwa wizara haina taarifa na swala la Baregu.
BADO naamini tunahitaji mawazo yakinifu katika maswala mazito yakuendesha nnchi, hatuna MAWAZIRI waadilifu hata kidogo, uwezo wao, utashi na uelewa wao juu ya mambo ya kitaifa ni wakutiliwa shaka.
 
Unaongelea suala la uhaba wa wahadhiri vyuo vikuu? Kwanza angalia umaskini wa walioahidiwa maisha bora. Halafu uruhusu akili yako ikumbuke gharama ya nyumba aliyojengewa Gavana!
Na mwisho Usisahau gharama za magari yaliyoagizwa na CCM kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mwaka huu, halafu usubiri mchang wao kwa waliokumbwa na mafuriko morogoro!!

Kisha ujiulize: Ipo haja ya kumwajiri mtu anayepingana na ufisadi au kuikosoa serekali isiyokuwa na mfumo wowote wa kiuongozi?

Nafikiri jibu ni hapana, Msomi wa chuo kikuu hawezi kuhongwa fulana, pilau na pombe za kienyeji akatoa kura yake!! Ujinga wa watanzania ndio mtaji wa wanasiasa walioko madarakani!!
 
Ni ujinga tu! Watanzania tunachinjana wenyewe kwa wenyewe ingawa tunajidai kuwa tuna amani. Haya ni mambo ya ajabu sana. Kuna mifano mingi sana ya wasomi waliojihusisha/wanaojiuhusisha na siasa na bado wanaendelea kufanya kazi ya umma ay kupewa mikataba. Nitatoa mifano kidogo.

1. Prof Mlambiti wa SUA aligombea huko Ulanga Magharibi kwa tiketi ya TLP mwaka 2000 na bado aliendelea kupewa mkataba wa kazi hata baada ya kustaafu! Na hii ilikuwa baada ya kutolewa waraka wa uliotaka mfanyakazi akigombea ubunge basi apewe kiinua mgongo chake (aachishwe kazi) na akitaka kurudi kazini (endapo atashindwa au baada ya kumaliza muda wake wa uongozi) basi aombe upya na atafikiriwa kama nafasi ikiwepo.

2. Prof Mbassa pia wa SUA aligombea jimbo moja huko Shinyanga mwaka 2000 (kwa tiketi ya CCM) baada ya kushindwa alipogombea kupitia upinzani mwaka 1995. Pamoja na huo waraka wa serikali alirudishwa kazini na hadi leo anafundisha.

3. Naamini wapo wengi sana hasa wana CCM waliorejeshwa kazini au wanaondelea na kazi pamoja na kujiingiza kwenye siasa.

Tatizo hapa ni kama mtu ana bifu na wakulu, vinginevyo sioni mantiki hata kidogo kwani hata wanajeshi/polisi wasioruhusiwa kujihusisha na siasa wanafanya siasa kwa kwenda mbele!
 
Back
Top Bottom