Unajua kusoma uhandisi ni mchaka mchaka pale UDSM watu wanaumia kwelikweli lakini wakisha maliza hawathaminiwi wanajitafutia kazi na mishahara midogo kweli mtu amehitimu uhandisi analipwa laki mbili au tatu kwa muhindi au muarabu? Hizo opportunity unazozisema ni zipi? Ukiangalia mwenzako aliyesoma uhasibu au Marketing kakuacha mbali kimaisha! Nakumbuka kuna jamaa mmoja alisoma uhandisi na ilikuwa katika Engineers' day 2008 akasema anaapa watoto wake hata wahamasisha wasomee uhandisi maana yeye amesota sana! Hii ERB imeanzishwa vizuri lakini wanafaidika wachache hawatetei wahandisi kabisa zaidi ya kuwakandamiza! Katika wahandisi 10 utakuta 1 au 2 ndio wanapata chance ya kuwa ktk mashirika mazuri na wanapata maisha bora! Hili suala ni la kuliangalia sana ! Na hata wengi waliohitimu Uhandisi still wanaendasoma MBA ambayo ni masters ya Biashara
Kwa kuwa sekta zote Tanzania zinatawaliwa na wanasiasa na ili ufanikiwe huhitaji kwenda kusomea uhandisi ambayo ni njia ndefu kwanini wasitafute njia fupi na inayokupeleka kimoja jikoni?
Sekta ya kuuza na kununua imepanuka haraka na ndiyo inayotajisha haraka na imekuwa sehemu ya siasa Tz
Hakuna utashi wa kisiasa kufanya watu wajenge utaalamu wao katika fani wanayoitaka.
Nakumbuka wakati nasoma o-level kazi nyingi zilikuwa zikionyesha viwango vya mishahara kulingana na fani mtu aliyosoma. Ni aghalabu ungemkuta katibu wa siasa wa chama anapata mshahara mkubwa kuliko daktari, lkn leo katibu wa ccm wilaya anamlipa mshahara Daktari anayeanza kazi na bado anabakiwa na mlo wa mwezi.
Fuculty of engineeringfoe iliharibiwa na prof ninatubu mathias lema, na kundi lake
Kwanza jamani ukisoma hiyo Engineering ni lazima ufanye kazi bongo tu??Kwanza engineering unaweza kwenda popote duniani na ukapata kazi je hayo masomo yenu B.Comm na BAF (Bachelor of Accounting and Finance) pia yanakuwaje??Maana mfano Dubai sasa engineering inalipa sana tena sana,ila kila mtu na mtazamo wake,Nadhani ukiwa shule ukichukua masomo nadhani ni vizuri kufikiria je hii kazi nitaipata hapa hapa Tanzania au popote pale??Nadhani hiyo ndio point,zaidi ya hapo mambo ya kusoma masomo kila mtu anasoma hayo hayo inakuwa kuwaste time na kupoteza mda sana yaani!!
fuculty of engineeringfoe iliharibiwa na prof ninatubu mathias lema, na kundi lake
Mkuu nadhani ingekuwa vizuri kama ungekuja na stats na facts hapa useme mwaka fulani wanafunzi(idadi) fulani waliomaliza PCM au PCB na kufaulu vizuri walikwenda kusoma Biashara chuo(vyuo) fulani na fulani.Ninavyofahamu wanafunzi wa high school wanaofanya hii michepuo siyo wengi kama wa arts au biashara labda iwe imebadilika hivi karibuni.Sasa kama unasema wengi wa hawa PCM na PCB wanasoma biashara,na wale wanafunzi wanaosoma biashara wanakwenda vyuo gani?Au tuna vyuo vingi vya biashara siku hizi kiasi kwamba enrollment imeongezeka sana?Ina maana huko engineering intake imepungua sana kwa vile hakuna waombaji manake wengi wanaenda B.com and the likes?Halafu kwa mfano kama mhitimu wa PCM(division one point 5) akaomba B.com pamoja na mhitimu wa ECA(division two point 10) nani atapewa kipaumbele?
Kifupi lete data kwanza tuone kabla ya kukadiria madhara yake.