Kwanini PCM wengi wanaenda commerce na BAF? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini PCM wengi wanaenda commerce na BAF?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by epigenetics, Feb 15, 2010.

 1. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2010
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 262
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Katika miaka ya karibuni, imekuwa "fashion" kwa wanafunzi waliosoma PCM form 6 kujiunga na vyuo vya biashara, yaani, kusoma B.Comm na BAF (Bachelor of Accounting and Finance). Utakuta hata wale waliopasua form 6 kwa kupata Div I kali (chini ya 6 pts) wanaenda kusoma hayo masomo. Hoja hapa si kuwa masomo haya ni mabaya (au rahisi) bali ni kuuliza, nini chanzo kunichowafanya wachague field hii?

  Ni wanafunzi hawa hawa ambao tunawategemea sana wawe ndio wahandisi na wavumbuzi mahiri ambao wangeweza "kusaidia" taifa katika karne hii ya uvumbuzi (invention and innovation era). Kwanini sio Electrical Engineering, Telecomm, Computer Science, Civil Engineering?
   
 2. m

  mtatifikolo Member

  #2
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo curriculum ya kozi za engineering TZ ni mbovu, na vijana wengi sahivi wanaona ni heri kwenda kusoma biashara na kuanza kushika pesa mapema kuliko kwenda kuumia na ma'ikweshenz na kutokuwa na uhakika na kazi baadaye.
   
 3. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 8,382
  Likes Received: 1,962
  Trophy Points: 280
  Unauliza ndevu kwa Osama,ukweli ni kuwa masomo ya biashara yanalipa ,ukuhitimu unahakika na ulua kwa muda mfupi
   
 4. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,632
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Hili ni tatizo kubwa saba nchini. Taifa letu linajeuzwa la wafanyabiashara na wakati kutoa huduma pia hatuna jadi hiyo. Hatujiandai na wala hatutaki kuwa wavumbuzi tena, tumechagua kuwa wauzaji wa vilivyoundwa nchi za nje. Si salama sana kwa taifa letu la baadaye.
   
 5. Katoma

  Katoma Senior Member

  #5
  Feb 16, 2010
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uhamasishaji unahitajika. Kwani mbona opportunity zipo nyingi kwenye Engineering and Technology? Tusipende vya chapchap.
   
 6. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 363
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nafikiri uchaguzi wa nini unaposoma Chuo Kikuu umebadilika sana!Way back watu walikuwa wanaangalia sana interest yako na pia uwezo wako kwenye eneo fulani kwani suala zima la career lilikuwa muhimu sana kwa individuals...as in mtu angependa kusema nitapenda kuwa Daktari na akafikia hapo.Anapenda kuwa mwalimu na akafikia hapo ila kwa miaka ya hivi karibuni hali imebadilika sana!

  Kutokana na mabadiliko mbalimbali na hasa pesa kuwa mbele basi hata vijana wanaamua kwenda kusoma mambo wanayofikiri ni rahisi zaidi kufaulu na pia wanaweza kupata pesa mapema.Nia si kusema Bcom au BAF ni rahisi lakini ndiyo myth ambayo imejengeka kuamini kuwa masomo ya Natural Science and Engineering huwa yanakuwa magumu zaidi.

  Hivyo unakuta watu wana Div 1 za PCM na PCB kali kabisa wanaenda kusoma hayo masomo ya biashara wakiamini kuwa watapata pesa mapema huku wakisahau kuwa mwisho wa siku kinachokupatia pesa na mafanikio si tu ulichokisoma ila ni ubora wako katika kile ambacho umekisoma!

  Kifupi hata ukisoma Archeology tusema,kama you are very you will stand out...you will an edge kwa hiyo watu wakiangalia Archelogist wazuri wewe wataku-pick tu kwa hiyo hata kama utakosa nafasi locally bado kama huko safi nje ya nchi utatumika...utaalamu wako hauwezi kwenda bure!

  Kimsingi tunahitaji mambo ya career guidance sana kwa vijana kuanzia mapema sana na hii itawasaidia kufanya uamuzi wa busara hapo baadaye hasa inapofika nini wanapenda kusoma!

  Kwa ufupi vijana wanakuwa motivated na pesa....lile suala la satisfaction kwamba unafanya unachopenda linakuwa hakuna na mwisho wake utendaji hata katika yale yanayowapatia pesa unakuwa si mzuri!

  Daamn....nitaandika siku nzima maana hili suala huwa linaniuma sana!
   
 7. k_u_l_i

  k_u_l_i Senior Member

  #7
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni sawa tu - wanaweza kufanya uvumbuzi kwenye field ya financial engineering ambayo ni muhimu sana.

  ┬ČK
   
 8. tgeofrey

  tgeofrey JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 531
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Fuculty of engineeringfoe iliharibiwa na prof ninatubu mathias lema, na kundi lake
   
 9. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,506
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Ndo kitu gani hicho mkuu?
   
 10. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,609
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Unajua kusoma uhandisi ni mchaka mchaka pale UDSM watu wanaumia kwelikweli lakini wakisha maliza hawathaminiwi wanajitafutia kazi na mishahara midogo kweli mtu amehitimu uhandisi analipwa laki mbili au tatu kwa muhindi au muarabu? Hizo opportunity unazozisema ni zipi? Ukiangalia mwenzako aliyesoma uhasibu au Marketing kakuacha mbali kimaisha! Nakumbuka kuna jamaa mmoja alisoma uhandisi na ilikuwa katika Engineers' day 2008 akasema anaapa watoto wake hata wahamasisha wasomee uhandisi maana yeye amesota sana! Hii ERB imeanzishwa vizuri lakini wanafaidika wachache hawatetei wahandisi kabisa zaidi ya kuwakandamiza! Katika wahandisi 10 utakuta 1 au 2 ndio wanapata chance ya kuwa ktk mashirika mazuri na wanapata maisha bora! Hili suala ni la kuliangalia sana ! Na hata wengi waliohitimu Uhandisi still wanaendasoma MBA ambayo ni masters ya Biashara
   
 11. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,609
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Inashangaza sana FOE ambayo sasa ni CoET Haina uharibifu wowote ila imesahauliwa na serikali! Kumbuka juzijuiz kwenye Engineers' day 2009 Prof Katima aliomba kitengo chake kichangiwe pesa wakati ni kitengo muhimu kwelikweli kinachotoa Mining Engineers , Chemical Processing Engineers lakini hakiangaliwi! Huyo lema Kaharibu wapi?
   
 12. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hii inatokana na wanafunzi wengi kuchagua career zao wakishamaliza form 6, huku secondary schools wanafunzi wengi huwa wanafuata mkumbo tu.,kwa aliyesoma secondary school atakuwa anafahamu kuwa kuna ile kasumba ya kufeel prestige kama unasoma masomo ya Science na kuwaona wenzako labda wa Arts kuwa ni vilaza tu.,sasa baada ya kumaliza shule ndipo mtu huwa anajitambua na kuchagua ni kipi sasa asome ambacho kinaweza kumpa maisha anayoyataka.
  Si kweli kwamba kozi za Engineering ni mbaya though zinaweza kuwa ngumu lakini hii si sababu ya kukimbiwa na hawa jamaa wa PCM ambao wengi wao unakuta wamefaulu vizuri tu hiyo form 6.,ni muhimu wanafunzi wakajitambua mapema zaidi kuliko kusubiri ukimaliza form 6.,walimu washirikiane nao kuwaongoza katika kile ambacho kweli kipo mioyoni mwao na waache kukimbilia Combinations kwa ajili ya prestige wafanye kile wanachokiweza na ambacho kitawajengea msingi wa career watakayochagua.
   
 13. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,458
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hizo ndo market forces, kuzizuia ni ngumu, the bottom line is how much you are earning at the end of the day!! Ndo maana vijana wanakacha CoET na kukimbilia Bcom ili waendeshe mikoko town!!

  Nina mdogo wangu wa mwisho yeye alimaliza form six mzumbe sec, akajifanya anataka afanye Civil engineering pale UDSM, nikamzuia na nikamwambia afanye Bcom then later aspecialize Accounting kisha afanye CPA. Akafuata ushauri, sasa anapeta sanaaaaaa!!

  Akinitembelea, huwa ananishukuru sana kwa kumtzuia asisome Engeneering, ananiambia karibu jamaa zake wote wanaganga njaa kwenye vi firm vidogodogo kama quantity surveyors, valuers n.k.
   
 14. m

  mtatifikolo Member

  #14
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  je, wale waliosoma biashara sekondari wanapetaje katika job market ukilinganisha na wa PCM?
   
 15. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kuna tatizo la washauri mfano mimi nilitaka kwenda engineering baada ya kumaliza PCM lakini kakangu aliyesoma accounting akaniambia huko engineering hakuna kazi (yaani viwanda) na accounting kuna lipa..hatimaye nikaishia kusoma commerce!

  Washauri wanabadili talent za watoto wengi sana ...
   
 16. m

  mtatifikolo Member

  #16
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu. in 20 years, hii nchi haitakuwa na wanasayansi au wahandisi. Kwanza hisabati vijana wengi wanafeli? Pili, wale wanaofaulu somo hili na yale mengine muhimu katika fani nilizotaja (Physics, Chemistry, Biology) hawaendelei nayo baada ya form 6. Kwahiyo wanaoweza hisabati na physics wanaenda biashara kujiunga na wale waliokimbia masomo hayo sekondari. Ingawa hii inaleta manufaa binafsi, kiujumla nchi inadidimia. So, we are screwed.....
   
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,427
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Best maisha ya sasa ni kuangalia maslahi asome uhandisi halafu akafanye kazi gani?

  Mwenzenu zamani sisi watu wa HGL tulidhaniwa tunapaswa kusomea Ualimu au Sheria, siku hizi ni mapinduzi mwezenu baada ya kumaliza BA niliunga moja kwa moja Masters na sasa nasoma MBA- Master of Business Administration hivyo hawa jamaa waacheni wakamue biashara best. Maslahi jamani!
   
 18. Katoma

  Katoma Senior Member

  #18
  Feb 16, 2010
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu mwenendo utafika saturation point karibuni tu na wengi wataanza kusoma engineering na technology
   
 19. p

  p53 JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35

  Mkuu nadhani ingekuwa vizuri kama ungekuja na stats na facts hapa useme mwaka fulani wanafunzi(idadi) fulani waliomaliza PCM au PCB na kufaulu vizuri walikwenda kusoma Biashara chuo(vyuo) fulani na fulani.Ninavyofahamu wanafunzi wa high school wanaofanya hii michepuo siyo wengi kama wa arts au biashara labda iwe imebadilika hivi karibuni.Sasa kama unasema wengi wa hawa PCM na PCB wanasoma biashara,na wale wanafunzi wanaosoma biashara wanakwenda vyuo gani?Au tuna vyuo vingi vya biashara siku hizi kiasi kwamba enrollment imeongezeka sana?Ina maana huko engineering intake imepungua sana kwa vile hakuna waombaji manake wengi wanaenda B.com and the likes?Halafu kwa mfano kama mhitimu wa PCM(division one point 5) akaomba B.com pamoja na mhitimu wa ECA(division two point 10) nani atapewa kipaumbele?
  Kifupi lete data kwanza tuone kabla ya kukadiria madhara yake.
   
 20. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe kabisa mkuu. Hii ni sawa na kuobey market forces. Itaenda itafika pahala itageuka tena watu wataenda kule kunakolipa automatically. You don't need to worry about this at all. Mambo tambarare tu babake.
  Hamuwezi kuwalaumu madogo kwa kwenda kufanya B.Com baada ya hizo PCM zao. Nyie kama mna mapenzi na hizo engineering si mkafanye? Kila mtu anafata mapigo ya moyo na taste ya ulimi wake bana! Wai ndio walioteseka na hizo PCM sasa kama wanaona namna ya kunufaika nayo why not?
  Kuna jamaa yangu alisoma PCM lakini alipofika UDSM akaamua kukamua LLB. Kamaliza fresh na sasa hivi mambo mswano! Yote maisha tu. Itakapokuja kuonekana kwamba B.Com hailipi kizazi husika kitajiorient chenyewe kuelekea kule bondeni(FoE/CoET). That much I believe!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...