Nimekua nikijiuliza kwa nini kiongozi mkuu wa kanisa katoliki na viongozi wengine wa kidini wana ulinzi mkubwa sana.
Kwa mfano, ulinzi wake nchini marekani ambapo yupo kwa sasa unademekana ndio ulinzi mkubwa kuwahi kutokea katika nchi hiyo toka imeumbwa,walinzi binafsi,swiss guards, secret service,fsderal guards,na walinzi wengine wa majimbo,walenga shabaha,wategua mabomu,mbwa wa kutegua mambomu na mambo mengine.
Sasa najiulza kwa nini kiongozi wa kidini anakua na ulinzi mkubwa hivyo, je ana maadui wengi au nini? Na kama ni maadui wengi wanatoka dini gani kwa maana nchi nyingi anazotembelea kama marekani wengi ni wakristo wenzake.
Je viongozi wa dini kwa nini wanakua na ulinzi mkubwa hivyo, hapa tanzania kuna kina gwajima,mwingira,geo davie na wengine ambao wanatembea na security team kubwa sana. Je mungu kashindwa kutoa ulinzi au ni nini?
http://www.washingtonpost.com/polit...2ca250-5d47-11e5-b38e-06883aacba64_story.html