Pona
JF-Expert Member
- May 26, 2014
- 1,099
- 647
Huoni ungekuwa umefanya jambo la maana endapo ungejibu maswali yangu? Kwa upande mwingine, hudhani huo ushauri ulionipa ungeutekeleza wewe mwenyewe ili ujionee ni namna gani huku bara tulivyo na umaskini wa kutisha? Narudia, ni ujinga Tanzania hii watu wa upande mmoja kujiona wapo juu wakati si lolote si chochote na kuwaona watu wa upande mwingine ndio hoe hae wasio na mbele wala nyuma wakati karibu wote hali zao zinafanana!! Watu wa bara (Tanganyika excluding mikoa ya pwani) ni hodari sana kuwasemanga watu wa Pwani na Zanzibar kwamba wanakesha vibarazani kunywa kahawa huku wao wakisahau kwamba wanakesha kwenye vilabu vya komoni, mbege, wanzuki, ulanzi na n.k... what's the difference!? Nafahamu, wengi wenu mnasumbuliwa na chuki, tena wengine chuki za kidini... nothing else! Kuna wengine wanakosa ujasiri wa kuelezea chuki zao za kidini wazi wazi na badala yake wanaamua kutumia mgongo wa Zanzibar au watu wa Pwani!
100% unasema kweli!
Mwengine anakuja na maneno ambayo hata mwendawazimu hawezi kuyatamka! Eti wazanzibar wengi hawana kazi hivyo wanategemea ndugu zao walioko ulaya kuwaletea Michele, maharage na mambo mengine!!! Huku mchangiaji wa hoja hii akisahau kuwa katanguliza neno "NDUGU ZAO" sasa suala ni hili:- Kama asiponisaidia ndugu zangu wakati nina shida sasa ninani mwengine atakaenisaidia!?? Au anataka tuwe na udugu Wa Samaki kujuana ndani ya sufuria!!!???
Kumbuka Zanzibar haina raslimali kama ambazo watanganyika wanazo! Lakini hiyo raslimali chache zilizopo Zanzibar "karafuu, mwani na utalii" basi maisha ya mzanzibari yako afadhali kulinganisha na ya mtanganyika!! Tembelea vijiji vyote vya Zanzibar huwezi kumkuta mzanzibar anaishi kwenye nyumba ambayo ni full suti ya udongo a.k.a TEMBE.