Willy,
Mafanikio mema mkuu. Usikatishwe na kelele za haters wa hapa JF.
Muhimu ni conviction yako katika hiyo kazi unayoomba. Ninaamini ukifanikiwa utasaidia kuingiza mtazamo mpya na mawazo mapya huko EA.
Kikubwa tu mkuu ukifanikiwa usituangushe. Watanzania ni mabingwa sana wa maneno lakini vitendo sifuri. Jikite kwenye kutatua matatizo na bahati mbaya kwenye EA yapo mengi sana.
Nimepitia majina ya wagombea na una qualifications zote za kutuwakilisha vizuri kuliko wengi wa hao waliopitishwa maana uzoefu ni mwalimu mzuri kuliko elimu ya madarasa. Inahitaji uwezo kuingia huko kwenye mameli na mpaka ukafika sehemu na kufanya mambo yako bila kubebwa na mtu. Hiyo ndio shule ya maana na ya kweli na sio kuwa na uwezo mkubwa wa kukariri ili kufaulu mitihani.
Wengine tungependa kuona watu wengi ambao wamepikika hapa JF wanachukua nafasi za uongozi kwa faida ya nchi yetu.
Mafanikio mema mkuu,
Mtanzania aka Mwakalinga.
Unafiki wa namna hii ndo umefanya hii nchi kubaki maskini. Kumsema mtu kuwa alifeli form four kuna uhusiano gani na chama. Kumuuliza kuhusu free movement of labor kuna vyama hapo? Yeye kaja hapa kujipima muache akabiliane na changamoto kamwe hatutambembeleza hapa kama unavyotushawishi.Nimesoma post nyingi hapa na nilichobaini Willy anakuwa more attacked kwa sababu ya UCCM na wala sio WILLY as Willy. Jamani ebu tuache party affiliations na tujadili issues badala ya mtu. Willy kwangu mimi is a hero kwani kile kitendo cha kuthubutu kutia mguu katika jukwa la siasa (field) sio jambo jepesi. Willy ni mpambanaji pamoja na madhaifu yake ambayo to me ni madogo. Wengi tupo hapa lakini kusogelea jukwaa live ni pamoto, tutambue katika siasa hizi tunazocheza nazo tunapaswa kutambua no body is perfect (no an angel here despite God alitimua baadhi yao kwa mapungufu pia).
Tukiendelea kuhusudisha vyama hapa na kutumia kigezo cha kumkatisha tamaa mtu kwa sababu ni Magamba haya mambo yatatugharimu in future. Huyu ni Kijana mwenzetu na kiukweli ana moyo wa kupambana japo mwanzoni nilidhani anatania. Tumuunge mkono na kama ana madhaifu yake much better kumuelimisha na sio kumu-insult yeye na hasa familia yake.
Wengi wetu tumetangaza hapa kuwania baadhi ya majimbo kibao, tambueni huko si kwepesi hivyo kwani dhambi hizi tunazoziasisi hapa ndizo tutakazo kutana nazo jukwaani kisiasa. Hakuna atakaye kosa shutuma,skendo ama tusi jukwaani. Narudia tena ni vizuri hapa tujadili issues (ideas) na wala sio mtu (people) ama matukio (events).
mashikolomageni
My profile:
1. Born in Tukuyu.
2. Jamhuri Primary School, Mnazi Mmoja; DSM.
3. Kwiro Secondary School, Mahenge; Morogoro.
4. Kidatu Sugar Instituon, Kilombero; Morogoro.
5. DSM Marine Engineering School (DMTU), DSM.
6. Field Kagera Sugar Factory, Kyaka; Bukoba.
7. Field Mv. Bukoba, Mwanza; Mv. Mwongozo & Liemba; Kigoma.
8. JKT Oljoro/Makuyuni, Camps; Arusha.
9. CMB Marine Engineering Insistute; Antwerpen, Belgium.
10. Field CMB-Belgian Shipping Line ( as Assistant Engineer)
11. Worked Tanzania/Chinese Shipping Company; DSM/Hongkong.
12. Associate Degree in Criminology & Police Science; Westchester College in New York, USA.
13. BA in Political science, Lehman University at New York City, USA.
14. One year Internship at Dominican Republic Permanent Representative to the UN, General Assembly; New York; USA.
15. Worked at Sterycircle Inc, as Class A Haz Mat & Poison at Disposal Facilities. Dealing with (Transportation + Financial Covering the Incinerator)
16. Started CCM branch in New York City, USA.
- Now aspiring to represent our Nation, to the EAC Assembly.
William.
sasa mbona sioni kilichokusukuma kugombea??....
Mkuu Mkama,Mtanzania
Kweli sie watz ni ma haters, lakini hii isiwe kigezo cha kutuzuia kuuliza watu maswali magumu na mepesi, nafikiri wewe ni muumini mzuri unayeamini kwamba kila anayetaka uongozi inabidi awe anaulizwa kwanza aliwahi kufanya nini na anategemea kufanya nini, kama hawezi kujibu hayo kunasababu tena nyingine ya kuongoza?
Mfano, anaongelea common visa ati akiongelea local watakuwa na free movement. Hapo sijamwelewa vizuri.
Je leo ukipata VISA ya UK utaenda UJERUMANI jibu ni hapana
Je raia wa UK anaweza kwenda ujurumani jibu ni ndiyo, anaweza fanya biashara huko jibu ni ndiyo. Na je ukipata VISA/working permit ya UJERUMANI unaweza fanya kazi Poland? jibu ni hapana.
Kuna kitu humo ndani amekielezea naomba nikili sijakielewa labda kama ana mda aje atuelezee tena. Yani hiyo common visa inauhusiano gani na local movement? na pia hiyo common visa itasaidia je kukuza uchumi?
Kingine anaongelea kama umeingia EAC basi usiogope usonge mbele, aa wapi bwana lazima uangalie na interest za nchi, mbona DAUDI KAMERUN alikataa ku sign ile sheria ya EU ya akina Sarkosy na Angela?
Unaposaini kitu ama kukikubali lazima uone nchi itanufaika kivipi? mfano hiyo common visa itawanufaisha wakenya tu, kwa sababu wao wana ndege yao na ni cheap kutua nairobi kuliko kutua Dar. Pili Nairobi ni karibu kwenda serengeti/kilimanjaro kuliko kutoka Dar.
Sasa wabunge lazima tuwaulize watalinda vipi masilahi yetu.
- My Bro we chose to join the EAC so now we need to work towards eliminating Fears, we need to work hard and find a way to balance our economic stand with other EAC members using the best asset in our disposal, I mean our land!
- How do you join the EAC and later claim that you want nothing to do with the EAC Viza, I am reading you right? I mean we need one Viza for EAC in order to Micro-economy, our people must free to move around so that with open policies on trade they can sell and buy products from point one to point B without interruptions, understand that sometimes the markets requires guarantee of movement of the people and security for their products and their lives.
- I do not believe in fear minded policies which you seem to preach and believe in!
William.
Maybe "You can live with that"?- I can leave with that, William.
Mkuu Mkama,
Mimi sina matatizo na mnaomwuliza William maswali, nina tatizo na hao wanaomtukana.
Pia tukumbuke William ni mmoja wapo tu. kama yeye atashinda hapa kujibu maswali wakati wenzake hawapo au hawaulizwi hitasaidia sana maana tutakuwa tunamkaanga William kwasababu tu tunamfahamu.
Kwa muda wote William amekuwa muwazi hapa na wengi tunajua msimamo wake miaka na miaka. Tumsaidie kwa maswali ya kumjenga na sio kumtegea au kumbomoa.
William,
..mimi sikubaliani na suala la kuruhusu watu waingie Tanzania bila passport.
..nasema hivyo kwasababu bado Tanzania haina national IDs wala ssn system.
..pia utalinda vipi ARDHI katika mazingira kama hayo ya kuruhusu Wanyarwanda,Wakenya,Waganda,na Warundi waingie Tanzania?
..pia tutalinda vipi soko letu la AJIRA ambapo unemployment ni kubwa mno?
..zaidi, with one visa to east africa kuna formula gani ya kugawana mapato.
..check this: Kenya has 9% of lake victoria, Uganda has 42%, and Tanzania has 49%. naomba unieleweshe faida tutakazozipata ktk matumizi ya rasilimali za lake victoria ikiwa tutafungua mipaka yake.
..pia Kenyatta Airport inapokea ndege nyingi kuliko KIA na Dar. Kenya imekuwa ikilaghai watalii kwamba vivutio vya Tanzania viko Kenya. Katika mazingira hayo kuna faida gani kuruhusu watalii toka Kenya waingie Tanzania bila malipo yoyote? Pia Tanzania sera yake ni kuwa na watalii wachache wakubwa, wakati Kenya ni mass tourism. Katika mazingira hayo how do we deal with Kenya wanapotu-pressure tufungue mpaka wa Golongoja[mbugani serengeti]??
..unadhani Tanzania itajikwamua namna gani toka kuwa wazalishaji wa malighafi ktk east africa, kwenda kuwa wazalishaji wakubwa wa bidhaa za viwandani?
NB:
..nakushauri uje kwenye International Forum ya JF huko ndiko mijadala ya East African Community imepamba moto.
Lugha gongana hapa.
Kunta Kinte wacha hizo! Kiingereza sio lugha yetu acha ulimbukeni na ushamba. Alichoandika kinaeleweka kabisa. Unajua nini ma-niga wa kuchovya huwa mnafikiri lugha ni elimu. Mbona wazungu wanapokosesea Kiswahili husemi lugha gongana, Wewe ni mtumwa wa hali ya chini sana unayejifanya umegeuka m-amerika mweusi Koma kabisa na elimu yako feki ya kwenye makaratasi.
Mtanzania
Ni kweli unachokiongea, binafsi hatumtegei maana tunauliza kutokana na maelezo yake mwenyewe, hiyo ya kusema wanzake hawapo sioni kama ni kigezo zaidi maana ni yeye mwenyewe ndo ameianzisha. Angeaizisha mwingine kwa kumsema William wala ni singe mhoji na wala sitomhoji kitu ambacho hajakiongelea mwenyewe.
Siku hizi ktk usaili (interview) wa kazi hasa ma engineer huwa wanauliza uliyoandika kwenye cv yako na waliyoolozesha kwenye Job Description (JD) yao. Ukiona wamekuuliza nje ya JD na CV yako basi jua hapo jamaa anakutegeshea, unless labda ktk kujieleza ulienda huko.
Mie sitaki kumtegea wala kumubomoa na uliza tu, ni jinsi gani ama kuna uhusiano gani kati ya common visa na local movements ktk nchi hizi. Na hiyo common visa inauhusiano upi ktk uchumi wa nchi hasa Tanzania.
Na je haoni common viza ni mtego wa wakenya kuchukuwa watalii wote? Si kwa sababu kenya wana utalii mzuri hapana ni kwa sababu kenya wana KENYA AIWAYS, ni ndege nzuri kiungo kikubwa na inamilikiwa na wakenya yeye haoni kuna potentials za kuuwa utalii na si utalii tu hata airport zetu zote.
Kivipi uwanja wa jommo kinyata ni wao na ndege ni yao kwahiyo watacheza na bei ya ticket tu, basi kwisha kazi airport za bongo na utalii kwisha.
Sasa hivi nafikiri wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya visa, maana tunaweza ku-compasate kwa kufanya viza juu na viongilio ktk sehemu za utalii juu, sasa mtalii anaona bora atue bongo. Vinginevyo wakiruhusu tu hiyo mie naona ndo bongo kwisha ktk utalii na hata airports.